Mgomo Baridi kuhusu kutumia miamala ya simu. Huko mtaani kwenu hali ikoje?

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
6,305
10,580
Wakuu Kwema!

Hapa mtaani kwetu kumekuwa na kamgomo baridi kuhusu utumiaji wa mihamala ya simu.

Watu wamegoma kutuma wala kutoa pesa kupitia mihamala kwenye simu.
Madai makuu ni kusema makato ni makubwa Sana.

Je, huko mtaani kwenu Hali ikoje?
 
Mgomo wakutotumia hautasaidia.
Mgomo uwe kama ule wakigoma mwezi uliopita,hakuna MTU kufungua biashara hadi madelu atoke
 
Mimi tangu jana bado sijafanya muamala wowote. Nilijiwekea kasalio mapema tangu juzi kwa ajili ya vifurushi na mambo mengine madogo madogo.

Labda baada ya siku kadhaa mbele ndipo na mimi nitaanza kusikilizia maumivu.
 
Mimi tangu jana bado sijafanya muamala wowote. Nilijiwekea kasalio mapema tangu juzi kwa ajili ya vifurushi na mambo mengine madogo madogo.

Labda baada ya siku kadhaa mbele ndipo na mimi nitaanza kusikilizia maumivu.
Maeneo ya Mwanza: Nimepita maeneo ya Mwanza hotel, eneo ambalo huwa kuna akina mama wengi wenye miavula na meza, ambao huwa wanatoa hizo huduma za fedha kupitia mitandao ya simu, sikuona mteja hata mmoja kwenye meza hata moja. Jambo ambalo siyo la kawaida.

Mara nyingi ukipita maeneo hayo, akina mama hao huwa wanakukimbilia na kukuuliza kama unataka kuweka au kutoa, leo hiyo hali hakuna. Wengi wameonekana kuchoka na kulalisha vichwa vyao kwenye meza.

Hili jambo la ongezeko dhulumati la kodi, sikufikiria kuwa limewafikia kiasi hiki. Kina kijana yupo Tabora, ilikuwa nimlipe shilingi laki 2, amesema niache kwanza ili atafute namna, atanijulisha nimtumie kwa njia gani. Anasema amesikia kuwa ukituma hela, Serikali inqchukua nusu ya pesa yote!
 
Wakuu Kwema!

Hapa mtaani kwetu kumekuwa na kamgomo baridi kuhusu utumiaji wa mihamala ya simu...
Nikikumbuka lile suala la vifurushi kupandishwa bei watu wakasema wanagomea kununua bando ila kilichotokea wananunua huku wanalalamika, hili nalo ni suala la mda tu watu wata adapt situation na wataendelea kutumia huduma za hela kimitandao.

Serikali itabidi iwe na vyanzo vingi vya mapato hii mambo ya kusema solidarity fund wakati wabunge wanalipana posho nyingi kwa kikao sio sawa wangepunguza kwanza za wabunge ili wachangie hoja bungeni wakiwa na akili sawa sawa.
 
Wakuu Kwema!

Hapa mtaani kwetu kumekuwa na kamgomo baridi kuhusu utumiaji wa mihamala ya simu..
Wakutotumia unatosha sana. Huo unakuhusu wewe, mimi na yule.

Kwanini watanzania tunataka afanye fulani? Mchango wewe ni upi?

Tupige chini miamala hii watanyooka tu.
 
Wakuu Kwema!

Hapa mtaani kwetu kumekuwa na kamgomo baridi kuhusu utumiaji wa mihamala ya simu...
Unaposema unamsaidia mtz wa hali ya chini alafu unajisaulisha ulichosema, uwe unajua au hujui wewe ni _____
 
Hii issue iwe iwavyo, lazima wateja wa hii biashara ya kutuma na kutoa pesa itapungua na kuwaumiza waliojiajiri kwa kazi hiyo.
 
Kuna mtu nilikuwa namdai laki4 jana akaniambia anazo kwenye simu, nikamwambia anitumie hivyo hivyo. Nitqziwacha hizo kwa kununulia vocha na DSTV. CCM sio watu aisee!
 
Back
Top Bottom