Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Mbunge wangu uyu maana 2010 nilimpigia kura na ananiongozo, kiukweli uongozi wa jamaa hata hapa jimboni kwake kwa sasa yupo fair, jamaa amekuwa na utu wa kupitiliza,

Kiukweli watu wake anawajali sana kama anavyojali barabara za maeneo yenu zitengenezwe

Anapenda maendeleo ya kila mfanyakazi wa halmashauri yake, kwa sasa ameshauri kila mfanyakazi kwa kutumia mshahara wake ahakikishe anajenga nyumba ya kisasa na kununua gari kwa kutumia mikopo ya nmb bank maana aliongea na manager wa nmb kila mfanyakazi anayekiz vigezo hasinyimwe fulusa ya kukopa,

Chato ameigeuza kama masaki katika utawala wake n.b kama mbunge wako kashindwa basi husilaum magufuri

Kwasasa umeme unapelekwa kila kijiji n.b hapa n ushawishi wa kila mbunge

Haingilii utendaji wa halmashauri kama wabunge wengine mamlaka yote yapo kwa DED

Mpaka kata za wapinzani kajenga barabara na anapeleka umeme, feza za jimbo anazigawa equally kwa madiwani wote awe ccm au chadema

Ameamua kufufua chama cha ushirika cha kusindika pamba kilichokufa kabla hajawa mbunge

Barabara za chato mjini zote anaweka mabaki ya lami inayobakia kwa wakandarasi may b anawaomba wamsaidie kuileta katika jimbo lake, nyumbani n nyumbani

Ni mbunge ambae kajenga kwao na mara nyingi yupo kwao kwa mapunziko tofauti na wabunge wengine wanaoishi ukimbizini a.k.a dsm

Hata kama yeye aliuza nyumba za serikali kumbuka yeye hakuwa mtu wa mwisho kuamua, alikuwepo waziri mkuu na rais wenye maamzi juu yake. Na alikuwa anatekeleza ilani ya chama. Kwaiyo hapo ilaumiwe ccm nzima na baraza la mawaziri na siyo magufuri pekee,

Hata kama ana mapungufu, ya magufuru n ya kibinadamu maana yeye c malaika, pia ukilinganisha yeye na wengine wa ccm, yeye n afadhari mara 10000.

Kutoka moyoni, pia nadekrea interest magufuri ni mbunge wangu na amefanya wonders katka jimbo lake, na kufikia january asilimia 60 ya watu wa chato watakuwa wanakunywa maji safi na salama, namuunga mkono magufuri for presidential candidate 2015

NB kutokuwa na maendeleo jimboni kwako n uzembe na umbumbu wa mbunge wako

Mungu ibariki Tanganyika Mungu mbariki rais mtarajiwa Mh Magufuri mbunge wetu wa ukweli.
mkuuu bado upo JF????? unakumnuka kuwa umewahi kuchangia kitu kama hiki????? how do u feel???????
 
Tunahitaji rais kama magufuli,nchi hii imechoshwa na siasa na sasa inataka utendaji na vitu vionekane kwa mipango,watu wanafanya nchi kama idara ya zimamoto, nchi imekuwa na slogani nyingi,mara ari mpya,maisha bora,kilimo kwanza, big result now,mabilioni ya kikwete...magufuli hana upuuzi huo,yeye anafanya kazi japo ana mapungufu, mapungufu hayo yanafunikwa na utendaji,usimamiaji.KAMA HAMTAMPA WA MUUNGANO,NI BORA TANGANYIKA IRUDI TUTAMPA URAIS WA HUKU
Mkuu Ipara, wewe ndio ulikuwa mchangiaji wa kwanza wa uzi huu, na leo nimetokea tuu kupita humu kufanya rejea haswa kwa kuzingatia ulisema nini na lini, na kulinganisha na kilichotokea na kinachotokea sasa haswa kwenye hoja ya mapungufu.

Ila pia nimekutana na uzushi huu wa Pangolin kukuhusu wewe. Kumbe ID ya Ipara iliwahi kupigwa ban ndio ikabidi yule ... wa Mama aokoe Jahazi!. Anyway hapa ulichangia mchango wa maana sana ambao ni ukweli mtupu wa kilichopo na kinachotokea!. Asante.
Pasco naona ulikuwa na nia ya kuwasiliana na mke wa magufuli naona kaingia hapa na id nyingine baada ya ile ya iparamasa kupigwa ban
Mkuu Precise Pangolin, please futa uzushi huu wa kuwasingizia watu ni wake za watu!.
P.
 
Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tuliomfuatilia Magufuli utendaji kazi wake kwa kauli na matendo tangu akiwa waziri, huyu mtu ameonyesha sio mzima sana kichwani in terms of stability in decision making!, amefanya maamuzi mengi very rational kwa baadhi ya maamuzi kwa jazba, papara na kukurupuka mtindo wa liwalo liwe, mwisho wa siku yanakuja kutu cost sisi kama taifa, mifano ipo, ikiwemo kuvunjwa ile Petro Station Mwanza, Uuzaji wa nyumba za serikali, Samaki wa Magufuli, just to mention but few, hivyo akipita na kuwa rais wa nchi, you can just imagine, atafanya maamuzi mangapi ambayo yatatucost kama taifa, ila pia kwa hulka yake, ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had!. Tuombe Mungu asaidie, hili likitimia, huyu mtu abadilike, vinginevyo.. !.
Paskali, pamoja na kuwa ULIACHA kuzitaja sababu za INNER sosi wako, miye naamini kuwa alisema ya Kweli (au angalau yanayokaribiana na ukweli). Ulo"TABIRI" hapa (soma penye rangi), ndiyo hasaa yanatokea!
 
Paskali, pamoja na kuwa ULIACHA kuzitaja sababu za INNER sosi wako, miye naamini kuwa alisema ya Kweli (au angalau yanayokaribiana na ukweli). Ulo"TABIRI" hapa (soma penye rangi), ndiyo hasaa yanatokea!
Mkuu vitu vingine usiwe unaquote, si unajua wakati wenyewe huu? Usiwape Urahisi wa
Kurejea, we hujui Pasco aliitwa kwenye kamati? Na kaahidiwa kama sio Ukatibu Wizarani
basi ukuu wa Mkoa.
 
Mkuu vitu vingine usiwe unaquote, si unajua wakati wenyewe huu? Usiwape Urahisi wa
Kurejea, we hujui Pasco aliitwa kwenye kamati? Na kaahidiwa kama sio Ukatibu Wizarani
basi ukuu wa Mkoa.
Duh!, ulijuaje?!, maana mimi mwenyewe niliyeitwa bado sijajulishwa matokeo!, kumbe kuna watu humu hadi kilichoahidiwa?!.
Basi na tusubiri...
P
 
Baada ya Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni super man, nimemkumbuka naomba nimdurusu kidogo, niliwaji kusema nini humu kumhusu mtu huyu.

P.
 
"Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tuliomfuatilia utendaji kazi wa Magufuli kwa kauli na matendo tangu akiwa waziri, mtu huyu ameonyesha wazi sio mtu mzima sana kichwani in terms of stability in decision making!, amefanya baadhi ya maamuzi mengi tuu kwa jazba, pupa, papara na kukurupuka kwa mtindo wa nimeamua mimi na liwalo liwe!, mwisho wa siku baadhi ya maamuzi yake ambayo mengine ni very national yanakuja kutu cost sisi kama taifa, mifano ipo, ikiwemo kuvunjwa ile Petro Station Mwanza, Uuzaji wa nyumba za serikali, Samaki wa Magufuli, just to mention but few, hivyo akipita na kuwa rais wa nchi hii, kama huu ndio mfumo wake wa kufikia maamizi, then you can just imagine, akiwa rais, atafanya maamuzi mangapi ambayo yatatucost kama taifa, ila pia kwa hulka yake, ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had!. Tuombe Mungu asaidie, hili likitimia, huyu mtu abadilike, vinginevyo.. !."
 
Wanabodi,

Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye kipindi kirefu nyuma, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha, zimenisikitisha, kunihuzunisha, kuniogopesha, kunisononesha na kuninyongonyeza!, kuwa eti imeishaamuliwa (sitaji imeamuliwa na nani), kuwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.

Kilichonistua, kunitisha, kunihuzunisha, kunisikitisha, kunisononesha, kunigopesha na kuninyongoneza ni the reasons behind alizonitajia kada huyu za why mgombea wa CCM ni Magufuli, ambazo ndizo zimepelekea the inner core ya CCM kuamua mgombea wake wa urais wa 2015 ni lazima awe John Pombe Magufuli tuu, and no one else!.

Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi kweli ni sababu za msingi na ziko justifiable kwa any reasonable man, sababu nyingine alizonitajia sio tuu ni unreasonable, bali pia ni unjustifiable! na hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!.

Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza hizo sababu nilizotajiwa za kwa nini ni Magufuli, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia juu juu tuu tena from just a single source, hivyo nahitaji kwanza kujiridhisha kwa kufanya verification kwa ku double check, na ku cross check ikiwemo kupata a collaborative verification na attribution ya third parties ili nijiridhishe kuwa hii ni habari za kweli na kuthibitisha kuwa kumbe hivyo ndivyo the inner core ya CCM inavyoweza kufikia maamuzi ya mgombea wake wa urais based on sababu nilizo tajiwa!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za kwa nini CCM imeamua mgombea wake wa urais kwa uchaguzi wa 2015 lazima awe ni John Pombe Magufuli tuu na sio mtu mwingine yoyote!, na kiukweli mkizisikia hizo sababu nilizotahiwa, naamini hata nyinyi mtashangaa!.

Kwa kawaida sisi waandishi wa habari, ukipata taarifa kama hii, huwa inaitwa "a news tip", haukimbilii kuiandika mbio mbio mpaka kwanza uifanyie verification kwa kui double check na kui cross check ili kujiridhisha kwa kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe, baada ya kuthibitisha na kujiridhisha kuwa ni kweli, ndipo unaiandika.

Lakini kwa vile sasa tunaishi kwenye dunia ya taarifa moto moto, "the world of information age", ukipokea tuu taarifa, unashare na wenzio, ndio maana na mimi nimeamua kuileta humu jf hii "news tip" hivi hivi ilivyo ikiwa kwenye hatua ya "tip" kabla hata ya verification, ili wewe kama mwana JF, uipate ile "JF advantage" ya "be the first to know!", yaani ukiwa mwana jf, unakuwa wa kwanza kujua, hivyo nawaombeni tuu sasa wana jf mkae mkijua kuwa "Mgombea wa urais wa CCM kwa mwaka 2015 ni John Pombe Magufuli!".

Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tuliomfuatilia utendaji kazi wa Magufuli kwa kauli na matendo tangu akiwa waziri, mtu huyu ameonyesha wazi sio mtu mzima sana kichwani in terms of stability in decision making!, amefanya baadhi ya maamuzi mengi tuu kwa jazba, pupa, papara na kukurupuka kwa mtindo wa nimeamua mimi na liwalo liwe!, mwisho wa siku baadhi ya maamuzi yake ambayo mengine ni very national yanakuja kutu cost sisi kama taifa, mifano ipo, ikiwemo kuvunjwa ile Petro Station Mwanza, Uuzaji wa nyumba za serikali, Samaki wa Magufuli, just to mention but few, hivyo akipita na kuwa rais wa nchi hii, kama huu ndio mfumo wake wa kufikia maamizi, then you can just imagine, akiwa rais, atafanya maamuzi mangapi ambayo yatatucost kama taifa, ila pia kwa hulka yake, ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had!. Tuombe Mungu asaidie, hili likitimia, huyu mtu abadilike, vinginevyo.. !.

Nikiisha "confirm" neno "tetesi" litaondolewa na kuwa replaced na neno "confirmed!", na nitaziweka hizo sababu nilizotajiwa ili sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za huyo kada wa CCM alizonipa kwa nini ni Magufuli!, na nyinyi pia zitawashitua, zitawatisha, zitawaogopesha, kuwahuzunisha, kuwasikitisha, kuwasononesha na kuwanyongonyeza!.

Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari kwa ma source inayoitwa "The Confidentiality of the source", na hapa wakati naileta taarifa hii humu jf, kwa vile zoezi la kumteua mgombea wa CCM bado liko mbali hadi mwaka ujao, unaweza kukuta hata Magufuli mwenyewe bado hajui kuwa ni yeye ndie atakuwa mgombea wa CCM, kwa sababu walio amua kuwa ni Magufuli sio kikao chochote rasmi na halali cha Chama Cha Mapinduzi, CCM bali ni "The Inner Circle" hivyo hii ni tip from the deep inside ya "the inner circle", na bahati mbaya sana, Magufuli mwenyewe hayuko kwenye hiyo "the inner circle!".

NB. Sio kila thread ni lazima ichangiwe, saa nyingine itoshe kujisomea tuu na kujipitia bila kuchangia chochote!. Hii ni just a news tip, kwa vile nimewaahidi naifanyia verification kuithibitisha, nawaombeni msiniulize swali lolote at this stage, kwa sababu sitajibu chochote!, and if possible nawashauri na nyingi msome FYE only na sio lazime mchangie kwa sasa na badala yake mvute subira kusubiria verification.

Sababu ya kuiwahisha humu JF kabla ya verification ni ili tuu wewe kama mwana JF to be the first to know!. Information is power!, if you are the first to know, then you'll have the powers to make good things happen or not to happen if they are bad things!.

Asante.
Paskali


Update: 12/07/2015

Leo hili limetimia ni kweli aliyepita ni Magufuli, nimezitafakari sababu nilizotajiwa ile siku napewa tetesi hii, na kuzipima na hiki kilichotokea, nimejikuta nimelazimika kutoziamini kuwa zile nilizosikia ndizo sababu zenyewe halisi.

Kwa sisi waandishi tuna kanuni ya kuandika only the truth, yaani kuandika nothing but the truth, sasa ili uweze kuandika jambo lolote, ni lazima jambo hili uwe umelishuhudia na kujiridhisha kuwa ni la kweli, ndipo unaliandika.

Ikitokea ukilisikia jambo la mashaka mashaka, unapaswa ulipime kwanza, ujiridhishe na ukweli wake, ukiisha ridhika ndipo uliamini na ndio uliandike.

Kama ikitokea wewe kama mwandishi wa habari, ukasikia jambo lolote ambalo ni la mashaka huliamini, then hupaswi kuliandika, tena hata ikibidi usiliseme wala kuliandika ili lisijulikane.

Hivyo hizo sababu nilizotajiwa siku hiyo napewa tetesi hii kuwa mgombea urais wa CCM atakuwa ni John Magufuli, and why he has to John Pombe Magufuli only and nobody else, kwa sasa mimi siziamini, na kwa vile siziamini, naomba nisizitaje wala nisiziseme kabisa humu.

Hivyo naomba sasa tuchukulie bandiko hili kuwa ni mwana JF mmoja kwa jina la Paskali, nilijiandikia tuu kuwa mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015 atakuwa ni Dr. John Pombe Magufuli, na ikatokea tuu kuwa mgombea urais wa CCM kwa 2015 kweli akawa ni John Pombe Magufuli.

Nawaombeni sana tuchukulie kupitishwa kwa jina la Dr. John Pombe Magufuli, kuwa mgombea urais wa CCM, has just happened tuu na has nothing to do bandiko hili wala na sababu nilizotajiwa, bali kuhesabike tuu kuwa kumetokea tuu naturally, by chance, bila any pre meditated moves, na hili bandiko lichukuliwe tuu kama just a coincidence, kuwa mwana jf mmoja nilisema mgombea wa CCM kwa mwaka 2015 atakuwa ni John Pombe Magufuli na kweli ikatokea tuu coincidentally, mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015 kweli akawa ni Dr. John Pombe Magufuli.

Kwa mtakaonielewa asanteni kwa kunielewa, na kwa wale ambao ni wazito kuelewa mambo ya kufikirika tuu au ambao msio nielewa poleni na samahanini sana!.

Hongera sana Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi, CCM.

Paskali
Nimeisoma tena hii thread yako.
You are such a prophet. At least kwa case hii.
Ulichosema nini tutarajie akiwa Rais kwa wakati ule, ndivyo imekuwa. Your words have come to pass.
Congratulations Paskali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom