Mgombea wa CUF, Diwani wa CHADEMA almanusura watwangane

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
MGOMBEA Udiwani Kata ya Erelai, Jimbo la Arusha kupitia CUF, John Bayo na Diwani wa Kata ya Daraja Mbili (CHADEMA), Prosper Msofe, wametunishiana misuli na kunusurika kuzichapa kavukavu mbele ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi (SSP) Gilles Muroto. Tukio hilo lilitokea juzi ofisini kwa OCD Muroto, wakati akiendelea na kikao cha kutathimini hali ya uchaguzi wa madiwani wa Jimbo la Arusha, baada ya kuwapo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani.


Taarifa zilizolifikia MTANZANIA Jumapili zinadai kuwa OCD Muroto Saa 4 asubuhi alikuwa ofisini akiendelea na kikao cha wagombea udiwani, viongozi wa vyama vilivyosimamisha wagombea na wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata kwa ajili ya kujadili na kuangalia suala zima la kudumisha amani.


Kwamba wakiwa katika kikao hicho kilichomhusisha pia Bayo kama mgombea wa Erelai, nje ya ofisi hiyo aliwasili Diwani wa Kata ya Daraja Mbili.


“Diwani Msofe alifika kwenye korido ya ofisi ya OCD na kukuta wafuasi wake waliokuwa wamemtangulia tayari kumsubiri, baada ya kufika pale alianza kuwasalimia kwa salamu ya chama ya Peoples.


“Kutokana na eneo lenyewe la ofisi kuwa dogo, Diwani huyo alipita katikati yao akiwa anawasalimia akielekea kufungua mlango wa ofisi ya OCD, sasa akiwa mlangoni tayari ndipo alipokuta ndani kuna kikao.


“Akiwa mlangoni aliwaona viongozi wa chama kwenye kikao hicho na aliwasalimia salamu ya chama, hatua hiyo ilimfanya Bayo kuchukia na kuona kama Diwani huyo ana ajenda ya kuharibu kikao chao,” kilidai chanzo cha habari.


Habari zinaeleza kuwa wakati Diwani Msofe akiwa bado mlangoni hapo, ghafla Bayo alionyesha kupaniki na kujaribu kumfuata, hatua iliyosababisha kikao kusimama kwa muda na OCD kumtaka Msofe kutoka nje.


MTANZANIA Jumapili lilipomtafuta Bayo kuzungumzia sakata hilo hakuwa tayari kutoa maelezo yoyote na kumuambia mwandishi wa habari hizi amuache.


Hata hivyo kwa upande wake Diwani Msofe, alipopigiwa simu na kuulizwa juu ya sakata hilo la kutunishiana misuli mbele ya OCD, alisema hakuwa na taarifa yoyote ya kuwapo kwa kikao kama hicho ndani ya ofisi za OCD.


“Mimi nilikuwa na appointment (miadi) na OCD saa 4, kwa hiyo hata hizo taarifa za kikao sikuzifahamu, vijana wangu wa chama kutoka kwenye Kata walitangulia pale ofisini.


“Nilipofika pale tukawa tunasalimia salamu ya chama, Peoples, Peoples, nikiwa naelekea kufungua mlango huku najibu salamu za chama ndipo nilipokuta kumbe kuna kikao kinaendelea.


“Nikiwa nimesimama mlangoni huku nawasalimia pia viongozi wenzangu wa chama waliokuwa kwenye kikao hicho ndipo Bayo alipoanza kurusha matusi makali dhidi yangu akisimama kuelekea nilipokuwa nimesimama.


“Pamoja na kusimama kunifuata OCD alifanikiwa kumzuia, Bayo hana uwezo wa kunipiga,” alisema Diwani Msofe.


Wakati hayo yakijiri, kampeni za vyama vilivyosimamisha wagombea zinaendelea kupamba moto jijini hapa kwa kufanya mikutano na kampeni za nyumba kwa nyumba.


Jana katika Kata ya Kaloleni, mgombea Udiwani wa CCM alifanya kampeni zake kwa kutembea nyumba kwa nyumba katika eneo la Kaloleni, Mita 200 akiomba kupigiwa kura.
 
Bayo tunamjua ametusaliti sana wanaelerai na sasa amekuja kugawa kura za CCM akidanganywa na CCM atapunguza za CHADEMA!
 
anapoteza muda wake huyo chadema watashinda tena kwa kishindo cha hali ya juu sana....
 
Wangezichapa tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Bayo ni zumbukuku mwenye kujifikiria yeye tu.,Amejisahau na kujiona yeye ni maarufu lakini akumbuke alishagombea mara ngapi na hakushinda mpaka pale alipobebwa kwa mbeleko ya CHADEMA!!!Eti ndiye huyo leo anapambana kupitia liberal!!!Mh.
 
Back
Top Bottom