Mgombea wa Chadema kurudusha fomu kesho kwa Maandamano Makubwa Zanzibar

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Mgombea nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya Chadema katika jimbo la Uzini Zanzibar anatarajia kurudisha fomu yake ya kuomba kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ili awe Mgombea wa Chadema katika uchaguzi huo. Zoezi hilo litafanyika majira ya saa 4 asubuhi ambapo mgombea huyo atarudisha fomu hiyo kwa maandamano makubwa ya Wananchama wa Chadema walio Zanzibar wakiongozwa na Fuso la matangazo pamoja na msafara wa magari na pikipiki na baiskeli. Mpaka sasa Makamanda wa kikosi maalum wa Chadema wameshafungua matawi 20 katika jimbo hilo yenye jumla ya wanachama 1236. Mgombea huyo wa Chadema alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa 2010 akifuatiwa na mgombea wa CUF
 
Naamini uchaguzi huu ndio mazishi ya CUF iliyofia Igunga na Kifo cha CCM iliyojeruhiwa vibaya Igunga na ambayo itazikwa rasmi Arumeru Mashariki miezi michache ijayo
 
Hii ni kukuza tu mambo rejeao kura za sifuri walizopata chadema uchaguzi mkuu uliyopita, hayo maanadamano makubwa yanatoka wapi?
 
Back
Top Bottom