Mgombea wa CHADEMA Arusha,atishiwa bastola na kupokonywa fomu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Arusha kimelalamikia wagombea wake katika uchaguzi mdogo wa serikali za mtaa ,kuporwa fomu za kugombea,kutekwa huku baadhi ya maeneo watendaji wa kata kufunga ofisi pindi wagombea hao wa upinzani wanaporejesha fomu za kugombea

Aidha chama hicho katika jimbo la Longido, Namanga na Loliondo kimedai kwamba watendaji wa kata hizo tangu jana wamafunga ofisi huku baadhi ya wagombea wake wakinyang'anywa fomu na watu wasiojulikana ambao huwa wamejificha katika ofisi hizo kuvizia wagombea wa upinzani wanapokuwa wakirejesha

Akiongea na vyombo vya habari katika kikao cha wagombea mbalimbali wa serikali za mtaa,jimbo la Arusha Mjini ,Katibu wa chadema Mkoa wa Arusha,Elisa Mungule amesema kuwa chama hicho kinahujumiwa na viongozi wa serikali ya Mkoa, wilaya, polisi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ili wagombea wao wakose sifa za kushiriki uchaguzi huo kutokana na hofu walionayo chama cha mapinduzi

"Baada ya kutoa fomu kwa wagombea wa chadema ofisi zote za kata zilifungwa hadi Leo ili wagombea wetu washindwe kuzirejesha huku wagombea wa ccm wakipelekewa fomu nyumbani ,hii si demokrasia hata kidogo" Amesema Mungure

Kwa upande wake mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ameiambia serikali kupitia wingi wa wabunge wa ccm kutoa mapendekezo ya kufuta vyama vyingi ili kibaki chama kimoja cha mapinduzi kuliko manyanyaso ya dhati wanayofanyiwa wapinzani

Lema ametoa kauli hiyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa zoezi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kufuatia vitendo vya utekaji dhidi ya wagombea wa chadema huku wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wakishiriki hujuma dhidi ya chadema

"Wagombea wetu wanatekwa kwa silaha ,wanaporwa fomu za kugombea, wananyimwa fomu ,wanapigwa na wanapoenda kulalamika polisi wanaambiwa mnachezeana wenyewe kwa wenyewe" Amesema Lema na kuongeza kuwa

"Mimi ningekuwa na mamlaka ningewaambia wagombea waachane na uchaguzi huu "

Baadhi ya wagombea mbalimbali wa mitaa,ambao wameeleza kunyanyaswa kwa kuchanwa kwa fomu zao wakati wakirejesha ,kutekwa ,kutishiwa maisha na kupigwa wamedai kwamba licha ya kupeleka malalamiko yao katika vituo kadhaa vya polisi na kupatiwa hati ya mashtaka,lakini hakuna msaada wowote wanaopatiwa na hivyo kuhofia kupoteza sifa za kugombea nafasi hizo

Baadhi ya wagombea hao waliokumbwa na kadhia hiyo Clotilda Aloyce ambaye ni mgombea wa mtaa wa Olmuriaki kata ya Sombetini amesema wakiwa katika ofisi ya afisa mtendaji walivamiwa na watu wasiojulika wakawa wanawashambulia kwa kipigo na kumtaka awapatie fomu

Naye Renatus Kimario mgombea wa mtaa wa kijenge Kaskazini kata ya Kimandolu alisema kuwa juzi wakiwa wanahakiki fomu majira ya saa saba mchana walivamiwa na watu watatu wakiwa na gari nyeupe aliyoitambua kwa namba T329 ASK ambao waliwatishia kwa bastola na kumtaka awapatie fomu na baada ya kuzichukua waliondoka kwa kasi

Naye katibu wa chadema wilaya ya Arusha Innocent Kisanyage ameitaja mitaa katika jiji la Arusha ambayo wagombea wake wamekumbwa na kadhia hiyo kuwa ni mtaa wa Sokoni One,Muriet,Olmoriaki na Longdong na kulitaka jeshi la polisi mkoani hapa kutotumika na wanasiasa ili kuepuka kuvuruga uchaguzi huo.

Akizungumzia kadhia hizo msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Arusha Mjini,Msena Binna amekiri kupokea malalamiko juu ya watendaji kutoonekana kwenye ofisi zao na kudai kuwa suala hilo wamelishughukia kikamilifu

"Kwa upande wangu sina taarifa za mgombea kutekwa ila kama kuna MTU ametekwa anapaswa kutoa malalamiko polisi kwa sababu ni kosa la jinai"

Ameongeza "malalamiko hayo nimeyashughulikia kwa kiwango kikubwa na kama kuna mgombea amepata shida anipigie simu mimi sina shida nitashughulikia" Amesema Binna.

Ends.....


IMG_20191102_131858.jpeg
IMG_20191102_123916.jpeg
IMG_20191102_130052.jpeg
 
Nashauri tuwaachie ccm uchaguzi huu wapite bila kupigwa kama hatuna mbinu nyingine zaidi ya sanduku la kura.
 
Chadema kuweni macho.kuna taarifa Kuna wagombea wenu

Wanachukua pesa kwa wagombea wa CCM halafu hawarudishi fomu halafu wanakuja na visingizio kuwa wameporwa fomu nk ili msije mkawashughulikia Kama wasaliti

Msiwaamni Sana hao watu wenu.
 
Huu ni ushetani ila dawa ya moto ni moto, kama hii amani ni yetu sote na tunashindwa kuilinda kwa haki hivi nani atasaidia kuilinda ? Kuna muda Afrika huwa tunalaumu sana wazungu kwamba wanatuvurugia amani na kutuletea machafuko ila ukweli wa mambo sisi ndio tunasababisha hayo, sijui huwa hatuoni au mpaka moto uwake. Viongozi watambue hizi sio zama za 1980's wanachokipanda kitatucost wote.
 
.... CCM siku zote bila msaada wa polisi hamuwezi shinda chaguzi kihalali, jengeni flyovers, nunua ndege hata 50, kama hampendwi, ni hampendwi tu....!
 
Kufanya haya lazima uwe na roho chafu kuliko shetani mwenyewe, anyway, kuna kikundi walishaamua kuwa na undugu na shetani ila kwa uweza wa Mungu Baba wataangamia.
 
Chadema kuweni macho.kuna taarifa Kuna wagombea wenu
wanachukua pesa kwa wagombea wa CCM halafu hawarudishi fomu halafu wanakuja na visingizio kuwa wameporwa fomu nk ili msije mkawashughulikia Kama wasaliti

Msiwaamni Sana hao watu wenu.
Kwa hiyo chama kinacho jinasibu kukubalika na kushinda kwa kishindo kinatoa Rushwa?
Haya asante kwa taarifa yako ya uhakika. Ila sijui MTU anayekubalika kwa nini atoe rushwa?
 
Hii ni trela tu bado picha kamili linakuja la uchaguzi wa Rais, wabunge, ma diwani

ova
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom