Mgombea wa CHADEMA aenguliwa,mgombea wa CCM aenguliwa na kurudishwa

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
11,497
8,313
Habari nilizo zipata kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya CCM na CHADEMA wilaya ya Momba mkoa wa Mbeya. Mgombea wa nafasi ya kijiji cha kamsamba wilayani Momba kupitia chama cha CHADEMA anayejulikana kwa jina la Kamwili Nzala ameondolewa baada ya kugunduliwa kuwa hajui kusoma na kuandika.

Mgombea wa CHADEMA aliondolewa baada mgombea wa CCM kukata rufaa ya kumlalamikia mpinzani wake kuwahajui kusoma na kuandika. Taarifa iliyokuja kuthibitika kuwa ni kweli mgombea haijui kusoma na kuandika baada ya kuitwa na kuhojiwa na tume ya uchaguzi.

Awali ya hapo ilielezwa kuwa mgombea huyo alikuwa ni mtumishi wa kujitolea katika mahakama ya mwanzo kama askari mgambo ambaye alikuja kufukuzwa baadaye kutokana na tatizo hilohilo la kutokujua kusoma na kuandika.

Wananchi wa eneo hilo wamewatupia lawama watumishi wa mhakama ya mwanzo kuwa ndio waliotoboa siri ya kutojua kusoma na kuandika kwa mgombea wao ambaye walitegemea kuwa angeweza kumshinda mpinzani wake baada ya kuteuliwa na chama chake bila kujua kuwa mgombea waliyemteua hajui kusoma na kuandika huku mpinzani akiwa hajui kuwa mtu wanaye shindana naye ni mtu asiye jua kusoma na kuandika.

Wakati huo huo mgombea wa kijiji cha jirani na hicho kupitia CCM amerudishwa kwenye nafasi ya ugombea baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo kwa kutokujua kusoma na kuandika.

Imeelezwa kuwa mgombea wa CCM ndugu Salvatory Kalipesa alimlamikia mgombea wa CHADEMA ndugu January Mwanakatwe kuwa hajui kusoma na kuandika.

Mgombea wa CHADEMA ambaye alikuwa na taarifa za kutosha kuwa mpinzani wake ndiye hajui kusoma na kuandika baada ya kupata taarifa kuwa mwenzake kamlalamikia,naye alipeleka malalamiko yake.

Wote 2 waliitwa na kuhojiwa na ikabainika kuwa mgombea wa CCM ndiye hajui kusoma na kuandika hivyo akawa ameondolewa kwa kukosa sifa.

Viongozi wa CCM wilaya walipopata taarifa kuwa mgombea wao kaondolewa kwa kukosa sifa walikuja juu na kurudisha jina la mgombea wao kwa kudai kuwa hawako tayari kijiji hicho kiongozwe na CHADEMA na huo ukawa ndio mwisho wa CHADEMA kupita bila kupingwa.
 
Kweli habari haipo sawa ajaribu tena kuhariri kwani haipo sawa

Nyie hamjamuelewa nini mleta mada? Hapo amesema kuna kijji kimoja mgombea wa Chadema ameenguliwa kwa kutokujua kusoma na kuandika,LAKINI kijiji cha jirani na hicho kuna mwingine CCM pia alienguliwa kwa kutokujua kusoma na kuandika hivyo akabaki mgombea wa Chadema,baada ya Ccm wilaya kuona hilo walitumia nguvu zao kumrudisha huyo mgombea wa Ccm japo hajui kusoma wala kuandika.USHAURI,mgombea wa Chadema na viongozi wake waende mahakamani mapema kwa huyo mgombea aliyerudishwa ili aondolewe na mahakama,lakini kule ambako mgombea wa Chadema hajui kusoma na kuandika wanaweza kusamehe!
 

Karne ya 21 mtu mzima mwenye akili timamu hajui kusoma na kuandika halafu anahenyesha makende yake kuchukua fomu za kugombea uongozi wa wanaojua kusoma na kuandika!!!

Hivi kwa nini vilaza huwa wanajiamini sana?

Unajua huna sifa ila uwezo wa kuzipata hizo sifa unao lakini hujishughulishi just from no where unataka u-chairman.

Walipaswa watandikwe viboko kwa usumbufu tena asubuhi kabla hawajasukutua meno ili liwe fundisho kwa wengine.
 
mtu ambaye hajui kusoma na kuandika siwezi kumtetea hatakama mimi ni chadema tukubali tumefanya upuuzi kumuweka mjinga kwenye nafasi hiyo

hatahivyo hakikisheni huyo njinga mwingine wa ccm anaondolewa
 
Back
Top Bottom