Mgombea wa CCM adai ameleta televisheni Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea wa CCM adai ameleta televisheni Mbeya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jibaba Bonge, Oct 1, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Thursday, 30 September 2010 19:57 0diggsdigg

  Brandy Nelson, Mbeya
  MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbeya mjini kupitia CCM, Benson Mpesya amewasihi wakazi wa jimbo hilo wamchague kwa mara nyingine kwani ndiye aliyeleta Telesheni ya TBC1 na Star TV katika uongozi wake wa kipindi kilichopita.

  Akizungumza katika moja mikutano yake ya kampeni juzi katika eneo la Uhindini jijini Mbeya alisema anashangazwa na watu wanaosema kuwa katika kipindi cha uongozi wake hakuna alichokifanya huku kukiwa na mambo mengi ambayo ameyafanya.

  “Nataka niwaeleze mambo niliyoyafanya katika kipindi cha miaka 10 kwamba ni mengi, lakini kikubwa nimeweza kuwaletea televisheni ya TBC na Star TV kwani huko nyuma hivi vitu havikuwepo,”alisema.

  Mpesya alisema pamoja na kuleta televisheni hizo ameweza kujenga ukumbi wa kisasa wa Benjamini Mkapa ambapo mmiliki wa ukumbi huo ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

  Mbunge huyo alisema mambo ambayo amefanya katika kipindi hicho,ni pamoja na kubadilisha Chuo cha Ufundi Mbeya (MTC) na kuwa Taasisi ya Sayansi na Tekonolojia (MIST) na kujenga Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo tayari amemuomba Mgombea urais Jakaya Kikwete kujenga wodi tatu katika hospitali hiyo.

  Aidha mgombea huyo alionyesha kumbeza mgombea wa ubunge kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu.

  Alisema kuwa atawashangaa wakazi wa Jimbo la Mbeya kama watamchagua mtoto ambaye ni mwanafunzi wake na anavaa ‘kata kei na heleni’ wakati yeye ameweza kuwafanyia mambo mengi na kielimu amemzidi kwani mpaka sasa ana shahada mbili.

  source: Mwananchi

  Mpesya, uwe unaangalia maneno ya kuwaambia wapiga kura wako, unakili kuwa joseph mbilinyi ni mwanafunzi wako na anavaa kata kei na heleni!! nani alimfundisha? Wewe si ndiyo mwalimu wake? Kama mwanafunzi anavaa heleni na kata kei si mwalimu wake itakuwa zaidi maana mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu.

   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ameishiwa sera huyo
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hana jipya kabisa huyo choka Mbaya wanambeya fanyeni mabadiliko.
   
 4. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hilo ndo kubwa..? sasa hayo madogo sijui ni kitu gani..
  Tuna muda mrefu wa kufikia maendeleo tukiendelea na wabunge kama huyu..!
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ukisikia mbunge anazungumzia upuuzi huu ujue yuko ICU
   
 6. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  :llama:mpesya kazidiwa akili hata na huyu anayerukaruka hapa:llama:
   
 7. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ha ha ha, ati ukumbi umejengwa na Halmashauri, kisha anasema yy ndo kajenga, so kila diwani wa manispaa husika naye anaweza akajipa shavu kuwa arudishwe kisa amekuwapo kwny hatamu wakati ukumbi ukijengwa. Jipange vyema SUGU umng'oe MFA MAJI huyo maana naona anatapa tapa tu, hoja kwishnei, teh teh!
   
 8. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama maneno haya ya kuwaletea wananchi TBC na STAR TV imetoka kinywani mwake, basi nimeanza kutilia shaka hizo shahada zake mbili. Maana sioni tofauti ya mvaa kata kei na msomi hapo!
   
Loading...