Mgombea uraisi UPDP yu hoi kitandani anaumwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea uraisi UPDP yu hoi kitandani anaumwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ICHONDI, Oct 1, 2010.

 1. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Fredy Azzah

  AFYA ya mgombea urais wa Muungano kwa tiketi ya UPDP, Fahmi Dovutwa bado tete na yuko kitandani kwa siku tisa sasa kutokana na tumbo lake kujaa gesi, na hivyo kupata maumivu makali ya vichomi tumboni.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Dovutwa alisema tatizo hilo limekuwa likimsumbua tangu Septemba 22 mwaka huu na kwamba alienda Hospitali ya Tumaini na kupewa dawa ambazo anatakiwa kuzitumia mpaka Oktoba 2.
  "Bado nipo kitandani... tumbo linajaa gesi na kunisababishia vichomi ambavyo vinanipa maumivu makali kweli," alieleza Dovutwa jana.

  Dovutwa alisema kutokana na maumivu hayo, anashindwa hata kunyanyuka kutoka kitandani.
  Alisema tarudi tena katika hospitalini mwezi huu ili kupata matibabu zaidi,
  Akionekana kukata tamaa, Dovutwa alisema hajui lini ataanza lini kampeni kwa kuwa afya yake haionyeshi matumaini ya kuimarika mapema.

  "Bwana wee acha tuu; hali ni mbaya; sijui lini nitaanza kampeni. Kwa sasa wenzangu wanapambana huko mimi nimelala kitandani," alisema.
  "Sasa sijui itakuwaje kwa sababu siku zinakwisha na mimi nitakuja kuanza kampeni wakati wenzangu wanamalizia, sijui itakuwaje," elieleza.

  Akizindua Ilani ya uchaguzi ya chama chake Septemba 15 mwaka huu, Dovutwa aliahidi kuanzisha kiwanda cha silaha; kufukuza wageni; kujiondoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufukuza wawekezaji.

  Dovutwa, ambaye ofisi za makao makuu ya chama chake ziko Magomeni Kagera, aliwaambia waandishi wa habari kwenye hoteli ya nyota tatu ya Blue Pearl kuwa nia ya kuanzisha kiwanda cha silaha ni kuwezesha Tanzania kujilinda kwa ufanisi zaidi.
  "Ili nchi iweze kuwa na maendeleo zaidi, ni lazima iwe na ulinzi wa kutosha unaotokana na utengezaji wa silaha zake zenyewe bila ya kununua nje ya nchi," alisema mgombea huyo.

  Alisema, silaha zinazokamatwa nchini na Jeshi la Polisi, zinaletwa na walifu kutoa nje ya nchii baada ya kufanya uhalifu katika nchi zao.

  SOURCE: Mwananchi

  Si vizuri kuongea haya mambo lakini itakumbukwa mwaka 2005 wakati Mbowe akiwa kwenye momentum kali kabisa mgombea mwenza wake mara tiiii, akafa, na uchaguzi ukaahirishwa. Ni baada ya kufa, mambo yalibadilika sana. So yetu macho mwaka huu si ajabu mambo yale yakatokea, unajua mgombea mmoja anayelindwa na majini, anaweza kutuma jini lake moja kwenda kumdondsha mgombea mwingine na mchezo aumalizie kirahisi
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,603
  Likes Received: 4,708
  Trophy Points: 280
  Lakini huyu ni mtu wao usajili wa chama alifadhiliwa na TISS, hata milioni moja ya kuchukulia fomu ya kugombea urais alipewa na TISS, hivyo wana haki ya kumfanya wanalotaka kwani ndondocha lao
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tmesikia mengi na bado masikio yetu hayajakinai.
  Nilisema kwamba CCM initumia TISS kwa manufaa yao na si ya taifa. najua walichokifanya kule kwenye mafunzo yao ni kuwaaminisha kuwa uhai wa CCM ni uhai wa TAIFA, maslahi ya CCM ni maslahi ya TAIFA.
  poleni Watanzania
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  AFYA ya mgombea urais wa Muungano kwa tiketi ya UPDP, Fahmi Dovutwa bado tete na yuko kitandani kwa siku tisa sasa kutokana na tumbo lake kujaa gesi, na hivyo kupata maumivu makali ya vichomi tumboni.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Dovutwa alisema tatizo hilo limekuwa likimsumbua tangu Septemba 22 mwaka huu na kwamba alienda Hospitali ya Tumaini na kupewa dawa ambazo anatakiwa kuzitumia mpaka Oktoba 2.
  "Bado nipo kitandani... tumbo linajaa gesi na kunisababishia vichomi ambavyo vinanipa maumivu makali kweli," alieleza Dovutwa jana.

  Dovutwa alisema kutokana na maumivu hayo, anashindwa hata kunyanyuka kutoka kitandani.
  Alisema tarudi tena katika hospitalini mwezi huu ili kupata matibabu zaidi,
  Akionekana kukata tamaa, Dovutwa alisema hajui lini ataanza lini kampeni kwa kuwa afya yake haionyeshi matumaini ya kuimarika mapema.

  "Bwana wee acha tuu; hali ni mbaya; sijui lini nitaanza kampeni. Kwa sasa wenzangu wanapambana huko mimi nimelala kitandani," alisema.
  "Sasa sijui itakuwaje kwa sababu siku zinakwisha na mimi nitakuja kuanza kampeni wakati wenzangu wanamalizia, sijui itakuwaje," elieleza.

  Akizindua Ilani ya uchaguzi ya chama chake Septemba 15 mwaka huu, Dovutwa aliahidi kuanzisha kiwanda cha silaha; kufukuza wageni; kujiondoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufukuza wawekezaji.

  Dovutwa, ambaye ofisi za makao makuu ya chama chake ziko Magomeni Kagera, aliwaambia waandishi wa habari kwenye hoteli ya nyota tatu ya Blue Pearl kuwa nia ya kuanzisha kiwanda cha silaha ni kuwezesha Tanzania kujilinda kwa ufanisi zaidi.
  "Ili nchi iweze kuwa na maendeleo zaidi, ni lazima iwe na ulinzi wa kutosha unaotokana na utengezaji wa silaha zake zenyewe bila ya kununua nje ya nchi," alisema mgombea huyo.

  Alisema, silaha zinazokamatwa nchini na Jeshi la Polisi, zinaletwa na walifu kutoa nje ya nchii baada ya kufanya uhalifu katika nchi zao."Katika baadhi ya vipaumbele vilivyoviainishwa kwenye ilani yangu ni pamoja na kuanzisha viwanda vya kutengeneza silaha. Hii italeta heshima kwa nchi dhidi ya wahalifu wanaofanya vitendo hivyo katika nchi zao na kukimbilia hapa nchini," alisema Dovutwa.
  Aliongeza kipaumbele kingine ni pamoja na kuvunja jumuiya iliyofufuliwa ya Afrika Mashariki ambayo anaona haina faida kwa wananchi.

  Chanzo: Mgombea urais hoi kitandani
   
 5. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  Wana wa nchi.....Kuna kila dalili kuwa utabiri aliotoa sheikh yahya juzi ni mkakati wa TISS ..kuwaandaa watu kisaikologia ...iwapo itaonekana wazi kwa viashirio kuwa mgombea wa CCM Jakaya Kikwete atashindwa uchaguzi..........basi mgombea wa UPDP ambaye ni mgonjwa kwa sasa na amelazwa TUMAINI hospital ...watamalizana naye ....na kupelekea uchaguzi kusogezwa mbele kwa mwezi mmoja kama mwaka 2005..

  Itakumbukwa kuwa mwaka 2005 kusogezwa mbele kwa uchaguzi kulisababisha kura za wapinzani kupungua na hata viti vya ubunge kwani wabunge wengi wa upinzani na wagombea urais hawakuwa na pesa ya kuendelea kufanya kampeni ...na CCM ..wakitumia PESA za EPA waliwahawia wagombea wao ubunge pesa ....na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kukata makali ya wagombea wa upinzani na hata kufaniikiwa kuupunguza idadi ya wabunge wapinzani...

  Taahadhari hii nimeitoa ili kuwataka watu wapaaaze sauti kuhakikisha usalama wa mgombea wa UPDP Fahmi Devutwa na afya yake kwa ujumla inaangaliwa kwa makini ....na ikiwezekana apelekwa nje haraka kwa matibabu na uangalizi wake uwe chini ya chombo huru ........ili yale ya JUMBE yasije yakatokea.......

  ccm wanajiandaa kuchinjia mtu baharini hali ikizidi kuwa mbaya ...na ikitokea hivyo uchaguzi ukasogezwa ...wapinzani watashindwa vibaya sana...na hata bungeni kutapwaya...FUNGUENI MACHO NA MASIKIO ...PAZENI SAUTI..THIS ISSUE IS SERIOUS!!


  SAA YA UKOMBOZI NI SASA!
   
 6. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena mkuu, kabisa kabisa jamaa hawataki kuachia madaraka kirahisi. Hiyo ni possible tena probability yake karibu 90% kutokea. Ngoja tusubiri kujionea.
   
 7. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Dejavu'
   
 8. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well said
   
 9. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sheria imebadilishwa, hata afe nani..Uchaguzi Oct 31
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  oohh really?
   
 11. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ahsante mkuu nilishaogopa kwa sababu hawa mafisadi wako tayari hata watz wote wafe ili mradi wao wabaki madarakani.sijui watamtawala nani?
   
 12. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndio Maana walimtuma yahaya akaseme uchaguzi mwaka huu utaahirishwa kwa kifo cha mmoja wa wagombea.

  Alianza kwa kuumwa tumbo kama wiki 2 zilizopita na alikuwa akipata matibabu hospitali moja pale magomeni kabla ya kuzidiwa na kupelekwa Tumaini Hospital.

  Probably they have given him a slow killing poison like Balali
   
 13. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Can you give the reference?
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Ndiyo sababu afya za wagombea ni muhimu kujulikana mapema. Watatuongezea gharama tu tena kwa nchi maskini kama hii uchaguzi kusegezwa mbele ni tatizo kubwa.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wakikusikia oooh na ikitokea wa ........mmh
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu sasa hii si inaweza kutoa mwanya kwa watu wenye nia ovu wakaeliminate wapinzani wao, not necessarily now hata chaguzi zijazo huko mbeleni.
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa alikuwa buheri wa afya ....wakati anatangaza kugombea pale blue pearl......nadhani wametumia loop hole ya udogo wa chama chake ....na kukosa ulinzi wa kuaminika ....kumlisha polllonium.............pazeni sauti....ya Jumbe [mgombea mwenza wa CHADEMA ] wanataka kuyarudia...hasa saafari hii kutokana na upinzani anaopata JK na hali ngumu wanayokabiliwa nayo majomboni.......mlifikiri bilioni 50 za kampeni ni za nini ...ni pamoja na kutumia muda unaposogezwa...wagombea wa CUF NA chadema watakuwa hawana tena pesa za kampeni !!!.......na kule zanzibar kuna yule mgombea anapanda VESPA .....wakiamua wanaweza kumgonga tu...two options!!!

  Nashangaa....kwanini tume ya uchaguzi inashindwa kuelewa umuhimu wa kuwamiliki wagombea wote wa urais kwa kuhakikisha wakishateuliwa tu kugombea ..regardless what wanatakiwa kupewa facilities...usafiri ,malazi,matibabu na ulinzi....ni haki ya mtu kugombea lakini akishateuliwa analindwa na sheria ....ni muhimu TUME ifanye vettin kujua mgombea anaishi wapi...na kama mazingira yake yanaendana na viwango vya kiusalama na afya...kama haviendani ni muhimu ...alipiwe hoteli inayoeleweka ili kwa kipindi chote cha ugombea asipate taabu na kuliiingiza taifa gharama......kama wakiridhika na mazingira yake basi wanamuacha ......mwaka 1995 tume ilitoa gari mbili 110 landrover kwa kila mgombea .....na facilities nyingine.... hili ni muhimu!!
   
 18. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Utabiri wa Sheikh yahaya nini? na akifa
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hivi mtu akishakubaliwa kuwa ni mgombea urais, inabidi kodi zetu zitumike kuangalia afya na ulizni wake mpaka siku ya kutangazwa matokeo ya urais.
  Mnajua kikwete ingawa anagombea urais bado anatumia 100% ya fedha za umma kwa yeye binafsi kuanzia afya hadi ulinzi? Hatuwezi kuondoa ulinzi kwa rais bali tuongeze ulinzi kwa wengine kwani ni possible presidents.

  Wakulu kuanzia sasa mpaka miezi sita baada ya uchaguzi chunga sana mialiko na misosi mnayokula kwenye jumuiko maana mafioso wa sisiem waliomo kwenye system hawataki kusikia sauti zetu wala mawazo yetu
   
 20. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  haya nayo, makubwaaaaaaaaaaaaaa
   
Loading...