Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia SAU aomba wananchi kumchagua ili afanikishe Sera mbalimbali zenye lengo la kumpa raha Mtanzania

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuptia SAU, Muttamega Mgaywa, amesema kama atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, atakuwa mstari wa mbele kulinda amani iliyopo.

Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro baada ya kushindwa kufanya mkutano wa kampeni kutokana na kuchelewa kufika mkoani humo.

Alisema pamoja na kwamba suala la kulinda amani ya nchi ni jukumu la Watanzania wote, lakini baada ya kuapishwa kuongoza taifa, atahakikisha nchi haiingii katika vita ya aina yoyote.

Mgaywa kadhalika aliwaomba wananchi kumchagua ili aweze kufanikisha sera za chama chake ikiwamo kumwezesha kila Mtanzania shilingi milioni moja.

Aliongeza kuwa sera nyingine zenye lengo la kuwapa raha Watanzania ni elimu na afya bure kwa watu wote, na kutoa posho ya kuishi yatima, walemavu na wazee sambamba na kujenga mabweni ya wanafunzi kwa shule zote za sekondari za serikali.

Alisema sera za chama chake zinatekelezeka kutokana na utajiri wa Tanzania hasa kwenye sekta ya madini, utalii na viwanda ambavyo kwa kiasi kikubwa vimechangia nchi kuingia katika uchumi wa kati.

“Nataka niwahakikishie Watanzania kwamba sera za SAU zinatekelezeka kutokana na utajiri tulionao, tunaposema elimu bure kuanzia awali hadi chuo kikuu, pamoja na kuwezesha kila Mtanzania shilingi milioni moja, serikali yangu itajenga nyumba za kuishi milioni moja ambazo wananchi watapewa na kulipa kidogo kidogo,” alisema Mgaywa.
 
Back
Top Bottom