Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ADC, Queen Curthbert Sendiga achukua fomu ya kuteuliwa kugombea

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,352
Mgombea wa Chama cha ADC, Queen Curthbert Sendiga amefika katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 7,2020 kuchukua fomu ya kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania.

Chama hicho kinakuwa cha sita kuchukua fomu na Queen amekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage.

Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi Agosti 25,2020.

photo_2020-08-07_13-13-07.jpg
 
Back
Top Bottom