Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kujibu maswali ya wananchi watumiao mitandao

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kumuuliza maswali Mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Ndg. Tundu Lissu; imebidi apate muda kuyapitia maswali yote (takriban 200) ili kila mmoja ajibiwe. Maswali hapa JF yaliulizwa kupitia > Uchaguzi 2020 - EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Aidha, takribani maoni 600 yamekusanywa toka Facebook na mengine takribani 165 toka Instagram; mengine 66 ya Twitter pamoja na wale waliotuma SMS, DM na barua pepe(Email).

Tunatarajia kufikia kesho atakuwa ameyapitia maswali hayo na yote yatajibiwa.

Shukran kwa wote walioshiriki; tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza
 
Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kumuuliza maswali Mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Ndg. Tundu Lissu; imebidi apate muda kuyapitia maswali yote (takriban 200) ili kila mmoja ajibiwe.

Aidha, takribani maoni 600 yamekusanywa toka Facebook na mengine takribani 165 toka Instagram; mengine 66 ya Twitter pamoja na wale waliotuma SMS, DM na barua pepe(Email).

Tunatarajia kufikia kesho atakuwa ameyapitia maswali hayo na yote yatajibiwa.

Shukran kwa wote walioshiriki; tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza
IMG-20201015-WA0040.jpg
 
Raisi wa tanzania mheshimiwa Tundu lissu umefika hapa? Kwanza sikuwahi kuamini kama utakuwa unasepa na kijiji kama unavyofanya maana miaka 5 mlifungiwa kufanya siasa wakawa wanatamba ccm tu kwa hii miez mitatu mliyopewa imetosha kuizika CCM wanapata tabu sana polisi na tume ya uchaguzi wamegeuka watetezi wa ccm kuwajibia hoja badala ya chama mheshimiwa uko hapa nikuulize? Kura yangu unapata tena ya
 
Ulinzi wa kura yangu ananihakikishia ulinzi ukoje ikiwa kuna njama za kununu mawakala kwa kuanzia laki 3 mpaka laki 5 na anazungumzia vip swala la watumishi na mawakala wa nec kuambiwa kuandika no za kadi zao za mpiga kura n kuzituma ikiwa zoez la kura bado akinijibu vzuri atapata kura yangu na familia yangu maana siwez piga kura hali ya kuwa najua kura zinaenda kuibiwa
 
Hamucha munyampaa.

Vp uendeshaji wa serikal ya kimajimbo utakavyokuwa?maana unasema tuu utaunda serikal ya majimbo bila kutuambia itakuaje na n zip faida serikal hiyo kwa mie mwananchi wa ilongero ambaye ni mkulima wa mtama?

Kwenye bunge la katiba uliwah kumkashifu mwl.nyerere vp uliwah kufuta maneno yako au bado msimamo wako ni uleule?
 
Back
Top Bottom