Mgombea Urais, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani-Awe mkazi eneo la jimbo husika, apimwe afya ya akili na asiwe mtoro wa kesi jinai

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,163
2,000
Wakuu,

Hili ni bandiko la Pendekezo,

1. Inapendekezwa kwamba mtu yeyote atakayejitathimini kuwa na nafasi ya kugombea uongozi wa kisiasa itamkwe kwenye katiba na sheria husika ni sharti apimwe afya ya akili na cheti cha uthibitisho kitolewe na kuambatanishwa kwenye fomu ya maombi ya nafasi ya uteuzi;

2. Inapendekezwa kwamba lia mgombea wa nafasi yoyote ya kisiasa katika linalotambulika na mamlaka ya usimamizi wa uchaguzi itamkwe bayana kwenye katiba kwamba ni sharti awe ni mkazi wa eneo hilo (jimbo, kijiji, kitongoji, mtaa au nchi kwa muda wote kabla ya uchaguzi kuwadia (hasa Urais ambapo jimbo lake ni ama Jamhuri ya muungano wa Tanzania au Tanzania Zanzibar;

3. Inapendekezwa kwamba mtu yeyote anayeomba kugombea nafasi ya uongozi wa kisiasa katika ngazi yoyote itamkwe kwenye katiba na sheria kwamba asiwe ni mtoro wa kesi ya jinai iliyokuwa inamkabili kabla ya uchaguzi (hati za kesi husika ziambatanishwe kupinga uteuzi wake endapo mhusika itabainika ametoa kiapo cha udanganyifu;

4. Vipindi vya uongozi wa kisiasa kupitia ubunge itamkwe kwenye katiba na sheria kwamba visizidi vitatu kwa mfululizo;

5. Chama chochote kinachohamasisha uvunjifu wa sheria, amani, kuvunjika muungano, uasi na tuhuma dhidi ya washindani wenzao pasipokuwa na ushahidi, uthibitisho wa mahakama itamkwe kwenye katiba na sheria kwamba ni sharti kifutwe mara moja wakishindwa kutoa ushahidi unaohalalisha matamko hasi yenye kuchochea chuki miongoni mwa jamii husika;

6. Mawaziri wote wateule kwenye wizara tofauti tofauti itamkwe kwenye katiba na sheria kwamba uteuzi wao sharti uzingatie kuwa na taaluma ya uongozi na utawala kwa ngazi ya shahada na katibu mkuu wa wizara sharti sharti awe na taaluma ya eneo husika ikwa pamoja na uongozi na utawala ili kupunguza misuguano isiyo na tija kazini baina yao na wafanyakazi wa idara.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061
2,000
Unawaambia CCM? sasahivi hatuna bunge, wala baraza la madiwani tuna mabaraza ya CCM.
 
Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,134

Kama Bwana Yule pale Chamwino
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom