Mgombea Urais TFF Oscar Oscar: Yanga SC inaongozwa Kihuni na ikiri tu kwa Mashabiki kuwa inaogopa kufungwa nyingi tarehe 3 July, 2021

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,302
2,000
" Kinachoendelea Yanga SC na huu mkanganyiko kuhusu wao kucheza au kutocheza Mechi yao na Simba SC tarehe 3 July, 2021 ni Uthibitisho rasmi kuwa Yanga SC sasa imejaa Wahuni na inaongozwa Kihuni. Na katika hili Yanga SC wasitake Kuwaficha Mashabiki wao bali waseme tu kuwa wanaiogopa hii Mechi kwakuwa wanajua kwa Kikosi chao dhaifu huenda wakapigwa nyingi kwa Mkapa ".

Chanzo: EFM Sports Headquarters leo.

Alipochukua Fomu yake Kugombea Urais wa TFF wana Yanga SC wengi ambao ' mnamchukia ' Rais wa TFF sasa Wallace Karia mlimpenda na Kumfurahia Mchambuzi huyu wa EFM Oscar Oscar hivyo ni Matumaini yangu makubwa GENTAMYCINE kuwa hata hii ' Sindano Chungu ' aliyowachomeni Studioni leo mtaendelea Kumpenda na Kumuunga mkono mara kwa mara.
 
Science Priest

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
2,085
2,000
Yanga ni kikundi fulani ambacho kiko disorganised kuanzia kwenye management uongozini mpaka timu uwanjani, kuwaita watani ni sawa kabisa, ila Yanga hawajawa na uwezo wakuitwa washindani wa Simba SC.
Mpira wa afrika ni fitna na majungu na inaonekana umeanza kushabikia mpira wa afrika recently, huo ustaarabu unaotaka kutuaminisha uko ulaya na sio afrika point sio kuwatetea Yanga hapana Ila ndo mpira wa afrika ulivyo
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,018
2,000
Nafikiri umekosea kumhusisha ugombea wake wa TFF na hoja alizotoa, tulitakiwa kujadili hoja zake kama zina ukweli au la.
Ni kweli yanga inaendeshwa kihunihuni kwa sababu mifano ipo hai.

Kwanza msemaji wao alisema tarehe 3/07/2021 hamna mechi kwa sababu wao hawaitambui lakinbi kaimu katibu mkuu wa yanga akaja kumruka na kusema ile kauli aliitoa kama shabiki lakini TFF ikiwachukulia hatua wanalia kuwa wameonewa.

Pia nilitegemea yanga wangemchukulia hatua Bumbuli kwa kushindwa kutofautisha kauli zake kama msemaji wa Yanga au Shabiki wa yanga.

Juzi tumeona wazee wa yanga waliitisha mkutano na kusema kuwa hawaitambui mechi ya tarehe 3/07/2021 lakini mpaka sasa hatujasikia tamko lolote kutoka uongozi wa yanga.

Ukifatilia kauli zao inaonyesha ni kweli yanga wanaogopa kucheza na simba wakitambua kikosi chao ni dhaifu na hata siku ile walilala mbele sababu walijua watapigwa goli nyingi.

Hakuna asiyejua waziri wa michezo ni yanga lialia pia ndiye aliyewataarifu TFF wasogeze mechi mbele je kama waziri wa michezo angekuwa shabiki wa Simba unafikiri nini kingetokea, si ajabu wangehamasishana wafanye maandamano hadi ikulu ili waziri atolewe.

Oscar Oscar yupo sahihi yanga inandeshwa kihuni.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,302
2,000
Ukome na uache Kunipangia cha Kuandika hapa JamiiForums sawa? Kwanza ulishakiri hapa kuwa hunipendi na ukinihusisha na Yanga SC ( Kiushabiki ) sasa kwanini 24/7 huwa unanisoma na hata Kuchangia ' threads ' zangu? Ndiyo maana huwa nawadharau na Kuwaita ( Kuwaiteni ) Wapumbavu.

Cc: rodrick alexander
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
8,450
2,000
Yanga haiwezi kuiogooa simba. Kwa wachezaji wepi Wa Simba Wa kuogopwa!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku zote Simba ni wachumba zetu tu! Naungana na wewe, hakuna mchezaji wa kumuogopa pale! Karibia nusu ya hao wachezaji wenyewe, ni wazee!

Halafu ndiyo waogopwe na vijana barobaro walioko Yanga! Kuna watu wana utani sana.
 
petro matei

JF-Expert Member
May 11, 2014
670
1,000
Screenshot_20210616-130705_Instagram.jpg
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,018
2,000
Ukome na uache Kunipangia cha Kuandika hapa JamiiForums sawa? Kwanza ulishakiri hapa kuwa hunipendi na ukinihusisha na Yanga SC ( Kiushabiki ) sasa kwanini 24/7 huwa unanisoma na hata Kuchangia ' threads ' zangu? Ndiyo maana huwa nawadharau na Kuwaita ( Kuwaiteni ) Wapumbavu.

Cc: rodrick alexander
ukitaka watu wasichangie au kucomment nyuzi zako usiwe unazileta humu.
Naweza kufukua nyuzi zako ulizokuwa unashabikia utopolo kwa kifupi wewe ni bendera fata upepo.
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
5,814
2,000
Yanga ni kikundi fulani ambacho kiko disorganised kuanzia kwenye management uongozini mpaka timu uwanjani, kuwaita watani ni sawa kabisa, ila Yanga hawajawa na uwezo wakuitwa washindani wa Simba SC.
Simba anahitaji kumfunga Yanga zaidi ya mechi kumi ndio alingane na idadi ya mechi Yanga alizomkalisha. Hata mechi mbili za mwisho bado Simba kwa Yanga anapumulia mashine. Hata Yanga queens inatosha kuwanyamazisha.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
5,814
2,000
Nafikiri umekosea kumhusisha ugombea wake wa TFF na hoja alizotoa, tulitakiwa kujadili hoja zake kama zina ukweli au la.
Ni kweli yanga inaendeshwa kihunihuni kwa sababu mifano ipo hai.

Kwanza msemaji wao alisema tarehe 3/07/2021 hamna mechi kwa sababu wao hawaitambui lakinbi kaimu katibu mkuu wa yanga akaja kumruka na kusema ile kauli aliitoa kama shabiki lakini TFF ikiwachukulia hatua wanalia kuwa wameonewa.

Pia nilitegemea yanga wangemchukulia hatua Bumbuli kwa kushindwa kutofautisha kauli zake kama msemaji wa Yanga au Shabiki wa yanga.

Juzi tumeona wazee wa yanga waliitisha mkutano na kusema kuwa hawaitambui mechi ya tarehe 3/07/2021 lakini mpaka sasa hatujasikia tamko lolote kutoka uongozi wa yanga.

Ukifatilia kauli zao inaonyesha ni kweli yanga wanaogopa kucheza na simba wakitambua kikosi chao ni dhaifu na hata siku ile walilala mbele sababu walijua watapigwa goli nyingi.

Hakuna asiyejua waziri wa michezo ni yanga lialia pia ndiye aliyewataarifu TFF wasogeze mechi mbele je kama waziri wa michezo angekuwa shabiki wa Simba unafikiri nini kingetokea, si ajabu wangehamasishana wafanye maandamano hadi ikulu ili waziri atolewe.

Oscar Oscar yupo sahihi yanga inandeshwa kihuni.
Sikuelewi kusema kikosi cha Yanga ni dhaifu, Simba hii ikiwa full ilipigana kufa na kupona kupata draw kwa Yanga, mechi iliyofuata Simba wakapoteza, sasa sielewi kipimo kipi Yanga ni dhaifu kwa Simba hii.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
lunatoc

JF-Expert Member
Aug 16, 2017
1,293
2,000
Sikuelewi kusema kikosi cha Yanga ni dhaifu, Simba hii ikiwa full ilipigana kufa na kupona kupata draw kwa Yanga, mechi iliyofuata Simba wakapoteza, sasa sielewi kipimo kipi Yanga ni dhaifu kwa Simba hii.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Haya tuseme yanga ina kikosi kizuri na Bora kuliko simba ..

Niambie yanga iko nafasi ya ngapi na Simba yenye kikosi dhaifu nafasi ya ngapi ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom