Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia UPDP, Twalib Kadege aahidi kutoa Ruzuku kwa Vyama vyote vitakavyoshiriki Uchaguzi hata kama havina Wabunge

Faith Luvanga

Member
Aug 21, 2018
14
15
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha UPDP, Twalib Kadege, amesema kuwa ikiwa Watanzania watampa ridhaa ya kuongoza nchi watahakikisha vyama vyote vinapata ruzuku kipindi cha Kampeni ili waweze kuendesha shughuli za Kampeni, pasipo kujali kama Vyama hivyo vitakuwa na wabunge au havina wabunge.

Katika mahojiano maalumu na Jamii Forums Kadege amesema, kutokana na Chama chake kutokuwa na Mbunge hata mmoja katika Bunge lililopita, hawajapata ruzuku ya kuwawezesha kuendesha Kampeni zao na hivyo kushindwa kufika maeneo mengi zaidi kuomba kura.

"Hatupewi ruzuku kwasababu hatuna mbunge,lakini hata hivyo naviomba Vyama vya upinzani vinichague mimi kwani katika Uongozi wangu Serikali itatoa ruzuku kwa Vyama vyote vitakavyoshiriki uchaguzi, haijalishi vina wabunge au havina" amesema Kadege.

Ameongeza kuwa ruzuku ya Uchaguzi ni keki ya taifa hivyo kila Chama lazima kipate kidogo, wenye wabunge watapata kadri ya wabunge walionao na wale wasio na wabunge watapata ili angalau waweze kupata mahitaji ya stationery na kuweza kuzunguka maeneo mbalimbali kuomba kura.
 
Kwa tafsiri nyingine ni kuwa "atawagawia pesa za walipa kodi vyama ili wafaidi pesa za bure hata kama hawana wabunge wa kutumia pesa hizo kwa ajili ya maendeleo"
 
Back
Top Bottom