Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu afanyiwa mahojiano kwenye kipindi cha ITV dakika 45

Lisu anapotosha hakuna uhusiano tuliokuwa nao na jumuia ya kimataifa ulioharibika.

Kama ni kweli kuna damage, Marekani asingeleta Balozi wake hapa baada ya kaimu kuondoka.

Hakuna Nchi iliyofunga ubalozi wake hapa Nchini.
 
119057614_197973511683765_7178176507246786920_n.jpg
 
Hii hoja ya ubeberu haitasaidia chochote CCM...kwanza anayewapokea mabeberu wote wanaokuja kujitambukisha nchini ni nani? Hiyo ndiyo aulizwe anawapokea kwa misingi ipi...
 
Lisu ni kibaraka !
Oktoba tutamrudisha kwa kibaraka wake Amsterdam
 
Hii hoja ya ubeberu haitasaidia chochote CCM...kwanza anayewapokea mabeberu wote wanaokuja kujitambukisha nchini ni nani? Hiyo ndiyo aulizwe anawapokea kwa misingi ipi...
Hii hoja imembomoa sana Lisu
 
✳TUNDU LISSU AJIBU HOJA YA YEYE KUTUMIKA NA MABEBERU KATIKA UCHAGUZI MKUU 2020

Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema,Tundu Lissu alijibu swali aliloulizwa na wandishi wa habari waliokusanyika nyumbani kwake Jumatano 9/9/2020 , "JE TUNDU LISSU INASEMEKANA UNATUMIKA NA MABEBERUU, NA UNAWEZA KUIUZA NCHI KWA MABEBERU IKIWA UTAKUWA RAIS?"


Mheshimiwa Tundu Lissu alianza kulijibu swali hilo kwa kuuliza swali " JE HAO MABEBERU NI AKINA NANI?

MAJIBU YAKE YALIKUWA HIVI!!

LISU : Hao mabeberu ni akina nani? Mkinipa jibu la hao ni akina nani, basi the rest is easy,

Je ni wamerakani?, Kama marekani ni mabeberu, basi kumbuka wanatufundishia Polisi wetu na wanajeshi wetu wanapofanya military exercise na majeshi mengine ya east africa, anayelipa ni Wamarekani, Africa command iliyocko based Germany ndio wanao cordinate na kufundisha hao wanajeshi wetu!! Je hao wamarekani ndio mabeberu? Kama hao ndio mabeberu basi tuambie nani anayetumiwa kati ya serikali yenu(CCM) Au mimi? wakati polisi wenu na usalama wenu mnafundishiwa na hao mnaowaita Mabeberu

Hao ambao wana fund, wanatoa misaada ya madawa tunazotumia, Are they mabeberu?Hawa ambao wamekuwa wanatupa misaada tangu uhuru ambao nyerere alienda kuomba chakula cha njaa mwaka 1962, hao ndio mabeberu? Hao ambao kipindi cha kikwete ndio walitoa uniform za wanajeshi wetu wote , je hao ndio mabeberu?

Hii hoja ya mabeberu ni hoja ya KIJINGA NA KIPUMBAVU kabisa!!.Hizi nchi ni nchi Rafiki za Tanzania , zilikuwa rafiki wakati Nyerere, wakati wa Mwinyi, Mkapa na hata Kikwete lakini Rais Magufuli ndio amevuruga marafiki zetu wote

Mimi(Lissu) nasema, tuta repair this damage to our international diplomacy, lazima tutawarudia marafiki zetu wote wamarekani, Waingereza, wachina,Warusi na kila mmoja ambaye amekuwa rafiki yetu miaka yote hii ambaye amevurugwa na kuitwa beberu na Rais magufuli wakati bado wanaenda kuwaomba misaada, ila sisi(Serikali ya Chadema) tutatengeneza upya huo uhusiano wetu wa kidiplomasia wa kimataifa ulioharibiwa na Rais Magufuli

Sasa kama sisi Chadema, tukifanya hivyo ni kuwa tunatumika na mabeberu, Sasa niambieni kwanini mnatumia madawa yao mbalimbali kama ya ukimwi,Malaria n.k Hata swala la kusomesha watoto, ule mradi wa kuboresha elimu, mmelipiwa na nani? mmeenda kukopa hao mabeberu! Hii ni nchi ambayo ni omba omba kwa miaka yote alafu tuna ujasiri wa kusimama na kuwaita watu mabeberu? Huku tunawaomba misaada? Huu ni ujinga kabisa!

Nani anayesaini mikataba ya madini na makampuni ya nje ya hao tunaowaita mabeberu?Nani anayemiliki madini yetu,by the way?.Miaka 5 ya magufuli , ni nani anayemiliki mgodi wa geita?ambao ndio mgodi mkubwa kuliko yote katika nchi hii Nani anayemiliki mgodi wa nyamwungu na Bulyanhulu na Buzwagi? utaona ni hao hao ambao mnawaita mabeberu ila miki nikizungumza mnasema Lissu anatumiwa na mabeberu ila akija mzungu wanazungumza nae wanasema Mwanaume amekuja yaani wakiwapa hela mnawaita wanaume ! Huu ni ujinga kabisa

Fikirieni, Nyinyi amshangai kwamba wale waliodai wametuibia kwamba hawajalipa kodi ya dola bilioni 495 hiyo kesi imeishia wapi?wakawakamata wakina deo mwanyika na kuwafungulia makosa makubwa lakini leo hiyo Deo mwanyika ndio mgombea wa ccm , Sasa hapo nani anatumia ufisadi, nani anatumika na mabeberu?Hivyo tuachane na haya maneno ya kupeana ujinga ujinga yasiyo na maana

Kwahiyo Mimi we will build our international diplomacy, maana bila kuwa na diplomasia huru basi nchi yetu tumekwisha.Magufuli anafikiri na sisi Tanzania ni Donar country? Are we donar country?Tanzania hii isiyoweza kulipa mishahara ya wafanyakazi wake, sisi ndio donar country?

Lazima tufahamu sisi(Tanzania) ndio tunaihitajo dunia kwani dinia inaweza kuendelea bila kununua pamba ya Tanzania au corosho ya Tanzania, au kahawa ya Tz au almas ya tanzania au dhahabu ya tanzania, dunia inaweza ikaendelea bila kununua chochote cha Tanzania, ila Je sisi Tanzania tunaweza kuka survive au kuendelea bila kununua vitu vya dunia? Can we survive?Kwahiyo hapa donar country ni nani?

Hayo ndio majibu ya Mhe tundu lissu aliyojibu alipoulizwa kuhusu kutumiwa na Mabeberu.....

Usikose kuendelea kujua maswali mengine mengi ya mtego aliyoulizwa Mhe Tundu lissu na kuyajibu kwa ufasaha wa hali ya juu..# Ni YEYE- 2020
Dhana nzima ya ubeberu huwa inakamilika pale taifa lenye nguvu linapotaka kulitawala taifa dogo kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.

Lissu anatumiwa na mabeberu ndio maana alikiwa hataki Accacia waondolewe hapa Tanzania ili waendelee kutunyonya. Na akawa anasema tukiwaondoa watatushitaki MIGA.
 
Back
Top Bottom