Mgombea urais CCM na uadilifu

Ngamanya Kitangalala

Verified Member
Sep 24, 2012
482
1,000
Tangu tupate uhuru toka kwa wakoloni Desemba 1961, taifa letu limepatwa kuongozwa na marais watano mpaka sasa, na wote ni kutoka katika chama cha mapinduzi

Tukianzia mwaka 1961 mpaka 1985 tuliongozwa na muaaisi wa taifa hili, hayati Julius Kambarage Nyerere, toka 1985 mpaka 1995 tuliongozwa na mzee Ally Hassan Mwinyi, toka 1995 mpaka 2005, tuliongozwa na mzee Benjamini William Mkapa, toka 2005 mpaka 2015, timeongozwa na mzee Jakaya Mrisho Kikwete, na sasa toka 2015 tunaongozwa na mh John Pombe Magufuli

Binafsi nimejaribu kufuatilia kwa karibu historia za viongozi hawa , KABLA YA KUTEULIWA KUPATA NAFASI YA KUWA WAGOMBEA WA CCM NA KISHA KUWA RAIS, ni kweli usiopingika viongozi hawa wote walikuwa ni waadilifu sana, kuanzia mzee Mwinyi katika nafasi zote alizowahi shika huko nyuma tangu uwaziri npaka urais wa Zanzibar, inaonyesha alikuwa ni muadilifu sana, nakumbuka hata huko nyuma alipokuwa waziri wa mambo ya ndani aliwahi kujiuzuru kwa sababu tu ya vifo vya mahabusu Shinyanga

Ukija kwa mzee Mkapa, najaribu kumtizama tangu alipokuwa mwandishi wa habari wa Rais, waziri wa habari, waziri wa mambo ya nje na baadae waziri wa elimu sayansi nab tekinolojia, hakika suala la uadilifu lilikuwa si jambo la kutilia shaka kwake

Kwa upande wa mzee Kikwete, ukifuatilia tangu alipikuwa naibu waziri wizara ya maji, nishati na madini, baadaye waziri kamila katika wizara hiyo hiyo, kisha waziri wa fedha na baadaye waziri wa mambo ya nje kwa miaka kumi nfululizo, kwa kweli suala la uadilifu naye lilikuwa si jambo la kutilia shaka miongoni mwetu sote watanzania

John Pombe Joseph Magufuli, naye kwa upande wake toka alipokuwa naibu waziri wa ujenzi na kisha waziri kamili wizara hiyo hiyo, na kuja kuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, kisha waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi, na kurudishwa tena wizara ya ujenzi, hakika naye suala la uadilifu kwake si jambo la kutilia shaka, hasa ukizingatia kwa mtu aliyekaa wizara ya ujenzi kwa niaka 15, moja ya wizara yenye bajeti kubwa kabisa na nikataba ya mabilioni ya pesa, kama asingekuwa muadilifu leo hii angekuwa ni mmoja ya wanasiasa wenye ukwasi mkubwa kabisa, hasa nikikumbuka mh Nalaila Kiula alikuwa waziri wa ujenzi kwa kipindi kifupi tu, ila alikuja kupata kashfa kubwa kabisa ya rushwa

Kwa kweli ni ukweli usiopingika, linapokuja suala la kupata ngombea wa kusimama katika nafasi ya Rais wa jamhuri ya nuungano, uadilifu umekuwa likitazamwa kwa unakini sana na chama cha mapinduzi, kwa hilo binafsi natoa pongezi sana kwao

Hapa nieleweke tu, kuwa nimezungumzia uadilifu wao kabla ya kupata nafasi ya Urais wa JMT, kuhusu nini walifanya walipokuwa madarakani hilo tutazungumzia siku nyingine

Mwisho tu, nitoe rai kwa wanasiasa wa sasa wenye mawazo ya kuja kuwa wagonbea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM, wajitahidi sana kuwa waadilifu na wazalendo kwa taifa letu Tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom