Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM: Msisumbuke kuangalia majina mengine kwenye karatasi ya kura, majina na wagombea wengine siyo halali, usipoteze muda kuwaangalia

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,688
2,000
Akiwa Wilayani Chemba-Dodoma, akielekea makao makuu ya nchi Dodoma, mgombea Urais wa CCM amesimama na kuhutubia hadhira ya wana-Chemba. Lakini katika jambo la kushangaza ambalo pengine NEC wanapaswa kuliona kama sehemu ya kinyume na utaratibu, Mgombea Urais wa CCM anasema wagombea wengine wanaoonekana kwenye karatasi ya kupigia kura siyo halali na hawapaswi kupigiwa kura. Jina halali na linalopaswa kupigiwa kura ni jina namba moja ndio maana hata NEC wameliweka juu.

Mgombea huyo amenukuliwa akisema

"Unapopiga kura Jumatano, angalia jina la kwanza kabisa, ndio Chama Cha Mapinduzi na jina langu lipo, weka tiki hapo. Usiangalie majina mengine ya chini, hayo yote siyo majina halali ya wagombea. Usipoteze muda kuyaangalia, angalia jina la kwanza na ukimaliza kupiga nenda ukalale. Mkawape fundisho wale wanaohubiri kuwa muandamane baada ya kupiga kura"--

Je kutangazia umma kuwa majina na wagombea wengine siyo halali ni sehemu ya kampeni? Mgombea ambaye ana nafasi ya Urais anaposema wagombea wengine siyo halali na majina yao si halali, Je haiathiri uchaguzi katika uvunjaji wa kanuni? Nini nafasi ya NEC katika kauli kama hizi?
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,700
2,000
Ni dhambi kupigia kura chama kingine nje ya CCM

His Excellency President Magufuli is the man of century in Tanzania and Africa

All votes for you Mr President
 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,138
2,000
Ni dhambi kupigia kura chama kingine nje ya Ccm

His Excellency President Magufuli is the man of century in Tanzania and Africa

All votes for you Mr President
Please qualify further that noun phrase - the man of a century.
 

Kwetuntwara

Senior Member
Jun 13, 2020
135
225
Nadhani NEC wala hawatapoteza muda wao tena maana siku zenyewe zimeisha. Wananchi ni kazi kwao sasa kutumia akili zao na kuamua kama yale majina mengine ni halali ama la
Aah wapi...hata ingekuwa ndio siku ya kuanza campaign, yeye haguswi.
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,952
2,000
Tume yetu imetugeuza sisi watanzia na kutuona mafala. JPM na Checheme yake wanaweza wakafanya lolote hutasikia tume ikisema kitu. Toka tume hii ilipotuambia kuwa kule Korogwe kwa masaa matano vyama vya upinzani takribani 5 vilishindwa kujua wapi warudishe fomu isipokuwa yule wa CCM niliwafuta kabisa. Neno Haki halipo kwenye kamusi zao. Hatuna tume bali washikaji wa JPM pale. Walisema passport size foto maana yake ni ukubwa wa foto na si kingine. Nenda wewe upeleke passport size ya upande upande ndio utawajua uhamiaji ni wakina nani. JPM anatisha wapiga kura, anabagua wapiga kura, juzi akiwa kilimanjaro anaagiza katibu mkuu alete hela za mradi etc kwa tume yote poa tu. Tume inazijua sheri na kanuni zinapowahusu wapinzani tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom