Elections 2015 Mgombea Urais CCM 2015: Ni Bernard Membe au January Makamba

Wote wanaotajwa kuwania urais kupitia CCM hakuna hata mmoja mwenye vigezo vya kuwa rais wa nchi,Membe hana uwezo wa kuongoza,Pinda ameshathibitisha udhaifu wake kwa kushindwa kutoa maamuzi pale apostahili kufanya hivo,kitendo chake cha kulia bungeni kiliprove his failure. Lowassa ameonesha uchu wa madaraka uliopitiliza kwa kutumia a lot of money kuusaka huo urais.Janury Makamba huyo ndo kabisaaa mana kama ni waziri na hajui kuwa yeye ni sehemu ya serikali basi akili yake ni nyembamba haijajua methali.....
 
Nikadhani unauliza ili upate jibu, kumbe unauliza ili uendelee kusikitika juu ya ukweli kwamba Membe anapanda chati miongoni mwa wagombea. Swali lina maana gani kama jibu tayari unalo? Huyo mgonjwa wenu hata tano bora hakanyagi na mnajuwa hilo. Ccm haiwezi kuchagua mgonjwa wa parkson na dementia awe kiongozi hata kama and washabiki wengi.
 
Kwasababu anachekacheka na mlopokaji pia cos alishalopoka "tutawapiga walawi nk, pia anaweza kulinda mali za viongozi waliopita kwasababu hata yeye alishachuma kwa sana huku mtwara na hotel kama 3 moja hii kubwa kuliko
 
Ingawa hakuna kanuni inayohitaji mgombea Urais (CCM) kuwa mjumbe wa NEC, imekuwa ni utamaduni kwa kigezo hiki kutumika, na itaendelea kuwa hivyo for the next foreseeable future; Hii ndio sababu kubwa kwanini Chaguzi za NEC mara zote huwa na pilika pilika nyingi na ushindani wa hali ya juu; Hapo nyuma niliwahi kuja na mada iliyojadili kwanini bila ujumbe wa NEC, Urais Kupitia CCM haiwezekani, na kila siku zinavyozidi kwenda mbele, hoja hii inazidi kuwa na mashiko;

January na Membe walikuwa ‘Very Smart’ kuamua to take the risk na kugombea Ujumbe wa NEC kupitia zile nafasi kumi za kifo i.e. NEC Ngazi ya taifa; Ingawa uamuzi huu ulikuwa too risky, suala ambalo wengi waliikimbia na kuamua kwenda kujaribu bahati zao huko wilayani, inaonyesha Membe na January walifanya a Cost – benefit Analysis na hatimaye kuona kwamba, it is more of a political asset than a liability, either for 2015 or beyond, hasa iwapo Chadema itachukua nchi 2015; Faida kubwa ya kuchukua uamuzi huu ni kwamba - whether you lose or win, tayari jina lako litakuwa sio geni miongoni mwa waamuzi wa nani awe mgombea Urais kupitia CCM 2015, ambao ni Wajumbe Mkutano Mkuu wa Taifa (CCM);

Wajumbe wa sasa watamaliza muda wao mwaka 2017, kwahiyo, ni wajumbe hawa hawa waliowapitisha Membe, January, Lukuvi, Wassira, Shigela, Mathayo, Msome, Nchemba, Mukama na Mukangara, ndio watakaopigia kura jina la mgombea Urais (CCM) 2015; Nje na Member na January, wengine waliobakia ni aidha sio Presidential Material au umri hautawaruhusu; Suala hili la Presidential Material ni relative na tutalijadili baadae;

Je, ni vigezo gani hutumiwa na CCM kumpata mgombea Urais? Najua wengi katika mjadala huu wataleta hoja khanga, kofia, n.k, kwani ukweli ulio wazi ni kwamba Chama kimechafuka; Lakini tukiweka hili pembeni kwa sasa, Vigezo vinavyotumika kuteua jina la mtu kuwa mgombea Urais (CCM) vipo vingi, na vingine ni very arbitrary na pia mchakato wake sio democratic; Lakini huo ni mjadala mwingine, na kwa sasa ningependa kujadili vigezo vifuatavyo:

  1. Awe na Sifa za Kuwa Mbunge Kufikia Kipindi husika
  2. Awe Mjumbe wa NEC Kufikia Kipindi Husika
  3. Jina lake liwe familiar miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa
  4. Asiwe amethibitika kwamba ni mla rushwa (tetesi hazitoshi)/Awe na Sifa Za Kukemea Rushwa
  5. Na Awe na Umri utakaovutia Wapiga Kura Vijana
Kwa mtazamo wangu, mgombea Urais kupitia CCM (2015) atateuliwa kwa kigezo aidha namba nne au namba tano, kulingana na upepo wa siasa utakavyokuwa; Kwa upande mmoja, iwapo Chadema utamweka Kijana kwa mfano Zitto au Lissu, CCM itajibu mapigo kwa kumweka Kijana ambae atakuwa ni January Makamba; Kwa upande mwingine, iwapo agenda ya Vita dhidi ya Ufisadi itazidi kushika kasi chini ya Chadema, hasa iwapo CCM haitatoa kafara angalau watu wawili watatu kuonyeshe progress towards that end, na Chadema kumweka Dr. Slaa au Hata Lissu, CCM italazimika kumweka mgombea ambae atatumika kurudisha imani kwa wananchi kwamba Chama kipo tayari kumaliza rushwa nchini, hivyo kumsimamisha Bernard Membe;

Ifahamike tu kwamba wagombea wa NEC kupitia wilayani hawana prominence kichama kama wale Kumi waliopita ngazi ya Taifa kwani, tofauti na wa wilayani, wa taifa sasa tayari wanajulikana wapiga kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa 2012-2017, na ni wapiga kura hawa ndio waliompa Membe na January Kura nyingi za NDIO;

Kwahiyo iwapo Membe na January wataamua kugombea 2015, njia yao ni nyeupe, na sana sana wanachohitaji only ‘fine tuning’ za hapa na pale; Iwapo mungu atawajalia Afya na Uzima, kitendo cha hawa wawili kuchukau fomu ya kugombea Urais 2015, automatically kitapelekea majina yao kufikia hatua ya mwisho ya mchakato wa kupata mgombea wa CCM - yani majina yao yatakuwa ni miongoni mwa majina matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa May 2015 kupigiwa kura; Kilichobakia kwa sasa ni kujua jina la tatu litakuwa ni la nani, ingawa huyu wa tatu hatokuwa na nguvu kama Membe au January; Nitafafanua hili lidogo hapo chini;

Uchaguzi wa NEC mwaka huu ulikuwa ni tukio pekee lililobakia kutupatia picha halisi jinsi gani mbio za Urais zitakavyo unfold kuelekea 2015, na unless litokee tukio kubwa sana na lisilotarajiwa kama vile CCM kumeguka na kuwa vyama viwili tofauti, hayata kuja majina mengine mapya na yenye kuvuma kuliko ya Membe, January, Lowassa, Mwandosya, Kigoda, Mwakyembe, Sumaye, Sitta, Migiro, Nape na Magufuli; Kutokana na sababu mbalimbali ambazo tutazijadili baadae, iwapo hawa wengine pia watajaribu bahati yao, mwisho wa siku, wote hawa katika hatua mbalimbali, watahamia kwenye kambi kuu mbili: (1) Kambi ya Membe au (2) Kambi ya January;

Utabiri wangu kama mlivyoona haupo biased, bali ni objective na unaotumia hoja, na sio uganga; Kwahiyo nategemea kwamba hoja yangu itakuwa challenged objectively na bila matusi. Pia ningependa kwenda mbali zaidi kidogo na utabiri wangu kwamba, kutokana na Chadema kuendelea kushindwa kupanua agenda yake ya kuingia ikulu nje ya UFISADI, na pia kutokana na Chadema kuendelea ku-ignore kushinikiza mabadiliko ya Kanuni ya ushindi wa chaguzi kuu i.e. kanuni ya mshindi ni mshindi iliyopitishwa na Bunge, Uchaguzi wa 2015, CCM kupata 50.01% ya popular vote dhidi ya Chadema ni kazi ndogo sana, bila hata ya uchakachuaji; Na kupata 50.01% ni rahisi kwa CCM hata ikiweka mgombea yoyote yule; Vinginevyo, iwapo things remain constant until 2015, na Membe na January wakagombea, Basi Ifikapo November 2015, Rais wa TANO wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania atakuwa ni aidha Bernard Membe, au January Makamba;

Na yoyote kati ya hawa wawili ataweza tu kumudu nafasi hii as long as he fulfills conditions such as: Upeo wa masuala ya kiuchumi na kisiasa - kitaifa na kimataifa katika nyakazi za leo, Uzalendo, anajali maslahi ya taifa mbele, Mkali, Ana uelewa wa matatizo ya wananchi, na ana ubunifu na pia moyo wa dhati wa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya wananchi, hasa wa vijijini; Lakini Rais ajaye ataweza kumudu nafasi hii vizuri zaidi iwapo katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho ili kuondokana na migogoro inayoendana na nafasi ya Urais; Suala lingine ambalo ni muhimu sana ni kwamba kutakuwa na ulazima wa Rais mteule (CCM) kupewa ushirikiano na kambi zote zilizopo sasa ndani ya CCM, vinginevyo Rais na nchi itayumba/haitatawalika;

Mwisho kabisa niseme tu kwamba nia yangu hapa sio kupigia debe viongozi hawa wawili kwani mbali ya siasa za NEC nilizojadili na pia conditions nilizojadili hapo juu, bado wana kazi kubwa ya kuaminisha watanzania kwamba atakayepita atakuwa Rais Bora na sio Bora Rais; Na mpaka tufikie hatua hiyo, Chadema wakifanyia kazi mapungufu yao, Rais Bora kwa Tanzania 2015 ni Tundu Lissu, na hii ni changamoto kwa Wagombea wa CCM kwamba muda ukifika, waanze kujieleza kwa wananchi kwamba wanasimamia ISSUES gani, kwani suala la PERSONALITY halitakuwa kigezo tosha cha kumpelekea mgombea Urais ikulu 2015; Inawezekana huko mbeleni wagombea wa CCM wataanza kunadi issues wanazosimamia, lakini mpaka tufike huko, mimi binafsi nadhani iwapo kutakuwa na uchaguzi wa Rais leo, Rais bora wa Tanzania ni TUNDU LISSU;

Ushindwe na kiswaengilish chako. Unatia kichefuchefu
 
Mkuu, ni kweli chama chetu kina maajabu na vihoja, lakini ikifikia hatua hiyo ndio kitakuwa kimepotea kabisa; Sina sifa hata za kuwa katibu wa tawi kwani moja ya sifa hizo ni kuwa na uwezo wa kuhonga, mimi sina uwezo, na hata ningekuwa nao, sina msukumo wa kununua uongozi au kulamba mtu miguu kupata uongozi;

kwa akili na maono haya,kwanini usijitoe kwenye hilo kundi?
 
Asante kwa mchango wako kiongozi; Nia yangu katika hatua ya mwanzo ilikuwa sio kuelezea sifa za hawa wawili bali sababu kwanini nadhani matukio ya sasa yatapelekea kuwa top three kwenye kinyang'anyiro hicho; Lissu nimemtaja kwa makusudi kama njia ya kuchokoza mada, hasa kuonyesha kwamba jina lako kupita CCM haitakuwa automatic kushinda Urais, hasa iwapo Chadema watafanyia kazi mambo kadhaa niliyojadili hapa na kwingineko; Vinginevyo nchi yetu inahitaji rais ambae:

1. Ana msimamo unaoeleweka juu ya muungano, hasa wenye kuweka maslahi ya Tanganyika na Tanzania kwa pamoja, na hafichi msimamo wake kwa kuogopa kuangamia kisiasa kwa kudai Tanganyika ndani ya Tanzania;
2. Ambae atakuwa ana heshimu utawala wa sheria;
3. Ambae atakuwa mkali juu ya ufisadi/rushwa;
4. Ambae ataendana na demographics zilizipo sasa katika population i.e. taifa kuwa ni la vijana;
5. Ambae anaonyesha uwezo wa kujenga hoja kuhusiana na maslahi ya taifa nje na ndani ya bunge;
6. Mwenye elimu, uelewa na pia upeo juu ya masuala la kisiasa, kijamii, kiuchumi, na kisheria, ndani na nje ya nchi;
7. ETC

Lissu anatosha katika mengi kama sio yote juu ya haya, na ni vizuri wagombea wa CCM muda ukifika nao wao tuwapime kwa haya na mengineo;

Duh!
Hivi kuna uwezekano CDM wakamsimamisha jamaa?
maana naona anazidi kuwa Popular kila siku!
 
Mchambuzi umejitahidi sana kuwachambua mabosi wako kwa undani na sifa zao,ila mimi sikungi mkono bse inaoneka we kama vile umetumwa wala si akili yako hasa ulivyoanza kuzungumzia kambi ya membe na january.kaka kweli nikuambie tu sasahivi wananchi hawangalii chama wanangalia uwezo wa mtu na je kama alishawahi kushika madaraka je aliwatendea nini ambacho kimekuwa na benefit at individual level up to family level,sikutegemea wewe na akili zako uanze kuangalia umri na kuwa mjumbe wa nec hivi hata wewe unaweza kuwa nazo lakini je unamudu kuongoza watanzania 45m na kuhakikisha wote wanapata huduma muhimu zote in terms of quality and quantity.
 
hahahahahahaha Dhaifu again ikulu? haiwezi tokea na haitatokea kamwe......................watanzania hawawezi kuchaguliwa rais na Mama Salma mambo yamebadilika saizi sio miaka ya 47...... Membe akawe rais wa WAMA...... by the way anataka urais gani sii tayari ni rais wa WAMA.......
 
Ingawa hakuna kanuni inayohitaji mgombea Urais (CCM) kuwa mjumbe wa NEC, imekuwa ni utamaduni kwa kigezo hiki kutumika, na itaendelea kuwa hivyo for the next foreseeable future; Hii ndio sababu kubwa kwanini Chaguzi za NEC mara zote huwa na pilika pilika nyingi na ushindani wa hali ya juu; Hapo nyuma niliwahi kuja na mada iliyojadili kwanini bila ujumbe wa NEC, Urais Kupitia CCM haiwezekani, na kila siku zinavyozidi kwenda mbele, hoja hii inazidi kuwa na mashiko;

January na Membe walikuwa ‘Very Smart' kuamua to take the risk na kugombea Ujumbe wa NEC kupitia zile nafasi kumi za kifo i.e. NEC Ngazi ya taifa; Ingawa uamuzi huu ulikuwa too risky, suala ambalo wengi waliikimbia na kuamua kwenda kujaribu bahati zao huko wilayani, inaonyesha Membe na January walifanya a Cost – benefit Analysis na hatimaye kuona kwamba, it is more of a political asset than a liability, either for 2015 or beyond, hasa iwapo Chadema itachukua nchi 2015; Faida kubwa ya kuchukua uamuzi huu ni kwamba - whether you lose or win, tayari jina lako litakuwa sio geni miongoni mwa waamuzi wa nani awe mgombea Urais kupitia CCM 2015, ambao ni Wajumbe Mkutano Mkuu wa Taifa (CCM);

Wajumbe wa sasa watamaliza muda wao mwaka 2017, kwahiyo, ni wajumbe hawa hawa waliowapitisha Membe, January, Lukuvi, Wassira, Shigela, Mathayo, Msome, Nchemba, Mukama na Mukangara, ndio watakaopigia kura jina la mgombea Urais (CCM) 2015; Nje na Member na January, wengine waliobakia ni aidha sio Presidential Material au umri hautawaruhusu; Suala hili la Presidential Material ni relative na tutalijadili baadae;

Je, ni vigezo gani hutumiwa na CCM kumpata mgombea Urais? Najua wengi katika mjadala huu wataleta hoja khanga, kofia, n.k, kwani ukweli ulio wazi ni kwamba Chama kimechafuka; Lakini tukiweka hili pembeni kwa sasa, Vigezo vinavyotumika kuteua jina la mtu kuwa mgombea Urais (CCM) vipo vingi, na vingine ni very arbitrary na pia mchakato wake sio democratic; Lakini huo ni mjadala mwingine, na kwa sasa ningependa kujadili vigezo vifuatavyo:

  1. Awe na Sifa za Kuwa Mbunge Kufikia Kipindi husika
  2. Awe Mjumbe wa NEC Kufikia Kipindi Husika
  3. Jina lake liwe familiar miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa
  4. Asiwe amethibitika kwamba ni mla rushwa (tetesi hazitoshi)/Awe na Sifa Za Kukemea Rushwa
  5. Na Awe na Umri utakaovutia Wapiga Kura Vijana
Kwa mtazamo wangu, mgombea Urais kupitia CCM (2015) atateuliwa kwa kigezo aidha namba nne au namba tano, kulingana na upepo wa siasa utakavyokuwa; Kwa upande mmoja, iwapo Chadema utamweka Kijana kwa mfano Zitto au Lissu, CCM itajibu mapigo kwa kumweka Kijana ambae atakuwa ni January Makamba; Kwa upande mwingine, iwapo agenda ya Vita dhidi ya Ufisadi itazidi kushika kasi chini ya Chadema, hasa iwapo CCM haitatoa kafara angalau watu wawili watatu kuonyeshe progress towards that end, na Chadema kumweka Dr. Slaa au Hata Lissu, CCM italazimika kumweka mgombea ambae atatumika kurudisha imani kwa wananchi kwamba Chama kipo tayari kumaliza rushwa nchini, hivyo kumsimamisha Bernard Membe;

Ifahamike tu kwamba wagombea wa NEC kupitia wilayani hawana prominence kichama kama wale Kumi waliopita ngazi ya Taifa kwani, tofauti na wa wilayani, wa taifa sasa tayari wanajulikana wapiga kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa 2012-2017, na ni wapiga kura hawa ndio waliompa Membe na January Kura nyingi za NDIO;

Kwahiyo iwapo Membe na January wataamua kugombea 2015, njia yao ni nyeupe, na sana sana wanachohitaji only ‘fine tuning' za hapa na pale; Iwapo mungu atawajalia Afya na Uzima, kitendo cha hawa wawili kuchukau fomu ya kugombea Urais 2015, automatically kitapelekea majina yao kufikia hatua ya mwisho ya mchakato wa kupata mgombea wa CCM - yani majina yao yatakuwa ni miongoni mwa majina matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa May 2015 kupigiwa kura; Kilichobakia kwa sasa ni kujua jina la tatu litakuwa ni la nani, ingawa huyu wa tatu hatokuwa na nguvu kama Membe au January; Nitafafanua hili lidogo hapo chini;

Uchaguzi wa NEC mwaka huu ulikuwa ni tukio pekee lililobakia kutupatia picha halisi jinsi gani mbio za Urais zitakavyo unfold kuelekea 2015, na unless litokee tukio kubwa sana na lisilotarajiwa kama vile CCM kumeguka na kuwa vyama viwili tofauti, hayata kuja majina mengine mapya na yenye kuvuma kuliko ya Membe, January, Lowassa, Mwandosya, Kigoda, Mwakyembe, Sumaye, Sitta, Migiro, Nape na Magufuli; Kutokana na sababu mbalimbali ambazo tutazijadili baadae, iwapo hawa wengine pia watajaribu bahati yao, mwisho wa siku, wote hawa katika hatua mbalimbali, watahamia kwenye kambi kuu mbili: (1) Kambi ya Membe au (2) Kambi ya January;

Utabiri wangu kama mlivyoona haupo biased, bali ni objective na unaotumia hoja, na sio uganga; Kwahiyo nategemea kwamba hoja yangu itakuwa challenged objectively na bila matusi. Pia ningependa kwenda mbali zaidi kidogo na utabiri wangu kwamba, kutokana na Chadema kuendelea kushindwa kupanua agenda yake ya kuingia ikulu nje ya UFISADI, na pia kutokana na Chadema kuendelea ku-ignore kushinikiza mabadiliko ya Kanuni ya ushindi wa chaguzi kuu i.e. kanuni ya mshindi ni mshindi iliyopitishwa na Bunge, Uchaguzi wa 2015, CCM kupata 50.01% ya popular vote dhidi ya Chadema ni kazi ndogo sana, bila hata ya uchakachuaji; Na kupata 50.01% ni rahisi kwa CCM hata ikiweka mgombea yoyote yule; Vinginevyo, iwapo things remain constant until 2015, na Membe na January wakagombea, Basi Ifikapo November 2015, Rais wa TANO wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania atakuwa ni aidha Bernard Membe, au January Makamba;

Na yoyote kati ya hawa wawili ataweza tu kumudu nafasi hii as long as he fulfills conditions such as: Upeo wa masuala ya kiuchumi na kisiasa - kitaifa na kimataifa katika nyakazi za leo, Uzalendo, anajali maslahi ya taifa mbele, Mkali, Ana uelewa wa matatizo ya wananchi, na ana ubunifu na pia moyo wa dhati wa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya wananchi, hasa wa vijijini; Lakini Rais ajaye ataweza kumudu nafasi hii vizuri zaidi iwapo katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho ili kuondokana na migogoro inayoendana na nafasi ya Urais; Suala lingine ambalo ni muhimu sana ni kwamba kutakuwa na ulazima wa Rais mteule (CCM) kupewa ushirikiano na kambi zote zilizopo sasa ndani ya CCM, vinginevyo Rais na nchi itayumba/haitatawalika;

Mwisho kabisa niseme tu kwamba nia yangu hapa sio kupigia debe viongozi hawa wawili kwani mbali ya siasa za NEC nilizojadili na pia conditions nilizojadili hapo juu, bado wana kazi kubwa ya kuaminisha watanzania kwamba atakayepita atakuwa Rais Bora na sio Bora Rais; Na mpaka tufikie hatua hiyo, Chadema wakifanyia kazi mapungufu yao, Rais Bora kwa Tanzania 2015 ni Tundu Lissu, na hii ni changamoto kwa Wagombea wa CCM kwamba muda ukifika, waanze kujieleza kwa wananchi kwamba wanasimamia ISSUES gani, kwani suala la PERSONALITY halitakuwa kigezo tosha cha kumpelekea mgombea Urais ikulu 2015; Inawezekana huko mbeleni wagombea wa CCM wataanza kunadi issues wanazosimamia, lakini mpaka tufike huko, mimi binafsi nadhani iwapo kutakuwa na uchaguzi wa Rais leo, Rais bora wa Tanzania ni TUNDU LISSU;

Nami ninakubaliana nawe 90%. Most likely Mhe. January anaweza kuwa Rais wa 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siasa ni Hesabu tu!
 
Pamoja na mahaba yenu kwa ccm tambueni watanzania hatuko tayari kutawaliwa tena na ccm 2015.Labda kama hao mnaowasema kuwa marais wawe ni kwa chama kingine na si ccm.
 
Naamini Mkuu amezingatia pia kuwa wakti huu ni zamu ya Wakristo, ila pia kumbuka na wenyewe sikuzote ni Wakatoliki tu, je safari hii tutapata nje ya katoliki?

Ila pia kumbuka kuna uwezekano ikawa ni Zamu ya ZNZ na hapo ndipo Mwinyi atakapo chomoza na kuacha watu kwenye mataa tukiduwaa.
 
Membe hafai,ana makuzi ya kipwani.ukilelewa Pwani huwi mtendaji mzuri na mwoga kutoa maamuzi magumu.Tumeona JK anavyofanya mambo kama anacheza ngoma.marehemu Kighoma Malima alipokuwa waziri,Kawambwa na viongozi wengine Wa sasa na waliowahi kuwa mawaziri na viongozi Wa ngazi mbalimbali Wa kutokea ukanda wa pwani,kutoka Tanga hadi Mtwara, wengi wao hawakuwa viongozi bora.
 
Back
Top Bottom