Huu wimbo 2a kutrka wqjumbe usha expireDiwani wa kata ya Daraja Mbili kupitia CCM, Prosper Msofe ambaye aligombea Umeya wa jiji la Arusha na kupata kura 9 amelalamikia yaliyotendeka katika uchaguzi huo.
Msofe amelalamikia wapiga kura kutekwa na kuwekwa kwenye ‘bar’ ambao pia walikatiwa mawasiliano naye. Amesema viongozi kuingilia uchaguzi unanyima haki za msingi za wananchi.
Ametoa rai kwa CCM na Serikali kuwa Uchaguzi uachwe kuwa huru, na wagombea wasibebwe.
Katika uchaguzi huo Maximilian Ilangye, diwani wa kata ya Kaloleni alichaguliwa kwa kura 24 na kuibuka kuwa Meya wa jiji hilo. Aidha Isaya Doita diwani wa Kata ya Ngarenaro kupitia CHADEMA alipata kura mbili.