Mgombea udiwani wa chadema iringa afanyiwa hujuma

Jun 9, 2011
16
0
[h=3][/h]

Edwin Sambala mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga (Chadema) akiwa ameduwaa ndani ya ofisi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata hiyo ambaye alitelekeza ofisi yake na kwenda kata ya KItanzini
Viongozi wa Chadema mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa kwanza kulia,mbunge wa viti malum mkoa wa Iringa Chiku Abwao mgombea udiwani kata ya Kitanzini Gervas Kalolo na katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonokulima wakimtazama msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kitanzini wakati akikagua fomu ya Kalolo

VITUKO vyaibuka zoezi la urejeshaji fomu za udiwani kata ya Gangilonga katika jimbo la Iringa mjini linaloongozwa na mbunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) mchungaji Peter Msigwa baada ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Gangilonga Lucas Wikes kuitelekeza ofisi yake kwa mgombea udiwani wa Chadema Edwin Sambala aliyekuwa diwani wa CCM kata hiyo mwaka 2005 hadi 2010 kabla ya kujiengua CCM na kujiunga na Chadema.

Msafara huo wa wafuasi wa Chadema na viongozi wake wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwalo (chadema ) pamoja na viongozi wa wilaya na mkoa walikutana na kituo hicho majira ya saa 8 .15 hivi mchana baada ya kufika katika ofisi ya afisa mtendaji kata ya Gangilonga na kukutana na kitabu cha wageni mezani huku mhusika ambaye ni msimamizi wa uchaguzi msaidizi akiwa ameikimbia ofisi hiyo.Kituo hicho ambacho kilionyesha kuwatibua nyongo wafuasi wa Chadema na kutaka kuifunga ofisi hiyo kimekuja huku kata hiyo ikionekana kuwa ni tete kwa ushindi wa CCM baada ya mshindi wa kura za maoni ndani ya CCM Michael Mlowe kukiumbua chama chake kwa kujitoa dakika za mwisho kugombea kabla ya CCM haijafanya uteuzi wa majina ya wagombea na nafasi yake kumpa mshindi wa pili Nicolina Lulandala ambaye alikataliwa na wana CCM katika kura za maoni.Mmoja kati ya watumkishi wa ofisi hiyo ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Gangilonga ambaye hakupenda kutaja jina lake aliwaeleza viongozi hao wa Chadema kuwa mtendaji huyo alikuwepo ofisini kwake dakika 10 zilizopita na baada ya kusikia shamla shamla za Chadema zikikaribia ofisi hiyo alilazimika kutoweka ofisini kwake na kuacha kitabu cha wageni na kusahau koti lake katika kiti na kutoweka kusiko julikana.Wakizungumzia tukio hilo wabunge wa Chadema Mchungaji Msigwa na Abwao walisema kuwa tukio hilo linafanana kabisa la lile la mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ambao ulipelekea CCM kushindwa vibaya katika uchaguzi huo.
Abwao alisema kuwa CCM imekuwa na kawaida ya kuandaa mazingira ya uchakachuaji wa matokeo toka mwanzo na kuwa hata kutokuwepo kwa msimamizi huyo ofisini na njama za CCM kutaka kuvuruga zoezi hilo kama ilivyotaka kufanya mwaka jana kwa kumzuia aliyekuwa mgombea urais wa Chadema Dkr Slaa kuhutubia katika viwanja wa Mwembetogwa kwa kuwatoa wanafunzi wa sekondari ya wazazi wa CCM Mwembetogwa kuigiza kufanya bonanza la kusaka vipaji katika uwanja huo hali iliyoamusha jazba kwa wananchi na kutoa hukumu dhidi ya CCM.
Hata hivyo alisema kuwa Chadema imejipanga kukabiliana na vituko vyote vya CCM katika uchaguzi huo ambao ushindi kwa Chadema upo wazi kwa kata zote.
Huku Mbunge Msigwa akidai kuwa tayari amewasiliana na msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini kumjulisha juu ya tukio hilo na kuwataka wana Chadema na wananchi kukumbuka kutoka hukumu kwa CCM siku ya uchaguzi.
Hata hivyo katika hali ya kujiami na njama hizo za kuachiwa ofisi viongozi hao wa Chadema walilazimkika kumwacha mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga Samba na wafuasi wawili pekee ndani ya ofisi hiyo na msafara mkubwa uliokuwa umewasindikiza wagombea hao wa udiwani kata ya Gangilonga na Kitanzini Miyombini kuondoka eneo hilo na kwenda kata ya Kitanzini kwa ajili ya kumsindikiza mgombea wao Gervas Kalolo kurudisha fomu ambako nje ya ofisi ya msimamizi msaidizi wa kata ya Kitanzini Miyomboni walishangazwa kumkutana Lucas Wikes ambaye ni msimamizi msaidizi wa kata ya Gangilonga aliyetelekeza afisi yake kitendo kilichowatibua zaidi wafuasi wa Chadema na kutaka kumpa kichapo kiongozi huyo.
Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonokulima alieleza kusikitishwa kwake na hatua ya kukosekana kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata ya Gangilonga na kuwa chama chake kinajipanga kufikisha malalamiko kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi.
Huku Wikes akijitetea juu ya kutokuwepo ofisini kuwa alilazimika kuondoka ofisini baada ya yeye kuwekewa pingamizi la kuwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata hiyo na hivyo kuondoka kwake ni sahihi kwani hata angekuwepo asingeweza kupokea fomu hiyo.

Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini Teresia Mahongo alisema kuwa kukosekana kwa msimamizi huyo msaidizi kwa leo si kosa kwani siku ya mwisho kurejesha fomu ni kesho ambapo wasimamizi wasaidizi wa vkituo vyote viwili hawatatakiwa kuondoka hata sekunde moja katika vituo hadi muda wa mwisho wa kurejesha fomu uliopangwa na tume ya uchaguzi ya Taifa.BOFYA HAPA
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,995
1,500
Hii ni mpya wameanza kukimbia nguvu ya umma na bado huu ni mwanzo tu kuna siku wataacha viatu ofisini wakikwepa peoples power.
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
5,190
2,000
Everyday we say this, CCM are delaying the inevitable. Watang'oka tu, kuanzia Igunga, kuna kata 3 Tarime na huko Iringa.
 
bi mkora

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
262
0
Edwin Sambala mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga (Chadema) akiwa ameduwaa ndani ya ofisi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata hiyo ambaye alitelekeza ofisi yake na kwenda kata ya KItanzini
Viongozi wa Chadema mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa kwanza kulia,mbunge wa viti malum mkoa wa Iringa Chiku Abwao mgombea udiwani kata ya Kitanzini Gervas Kalolo na katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonokulima wakimtazama msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kitanzini wakati akikagua fomu ya KaloloVITUKO vyaibuka zoezi la urejeshaji fomu za udiwani kata ya Gangilonga katika jimbo la Iringa mjini linaloongozwa na mbunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) mchungaji Peter Msigwa baada ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Gangilonga Lucas Wikes kuitelekeza ofisi yake kwa mgombea udiwani wa Chadema Edwin Sambala aliyekuwa diwani wa CCM kata hiyo mwaka 2005 hadi 2010 kabla ya kujiengua CCM na kujiunga na Chadema.

Msafara huo wa wafuasi wa Chadema na viongozi wake wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwalo (chadema ) pamoja na viongozi wa wilaya na mkoa walikutana na kituo hicho majira ya saa 8 .15 hivi mchana baada ya kufika katika ofisi ya afisa mtendaji kata ya Gangilonga na kukutana na kitabu cha wageni mezani huku mhusika ambaye ni msimamizi wa uchaguzi msaidizi akiwa ameikimbia ofisi hiyo.Kituo hicho ambacho kilionyesha kuwatibua nyongo wafuasi wa Chadema na kutaka kuifunga ofisi hiyo kimekuja huku kata hiyo ikionekana kuwa ni tete kwa ushindi wa CCM baada ya mshindi wa kura za maoni ndani ya CCM Michael Mlowe kukiumbua chama chake kwa kujitoa dakika za mwisho kugombea kabla ya CCM haijafanya uteuzi wa majina ya wagombea na nafasi yake kumpa mshindi wa pili Nicolina Lulandala ambaye alikataliwa na wana CCM katika kura za maoni.Mmoja kati ya watumkishi wa ofisi hiyo ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Gangilonga ambaye hakupenda kutaja jina lake aliwaeleza viongozi hao wa Chadema kuwa mtendaji huyo alikuwepo ofisini kwake dakika 10 zilizopita na baada ya kusikia shamla shamla za Chadema zikikaribia ofisi hiyo alilazimika kutoweka ofisini kwake na kuacha kitabu cha wageni na kusahau koti lake katika kiti na kutoweka kusiko julikana.Wakizungumzia tukio hilo wabunge wa Chadema Mchungaji Msigwa na Abwao walisema kuwa tukio hilo linafanana kabisa la lile la mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ambao ulipelekea CCM kushindwa vibaya katika uchaguzi huo.
Abwao alisema kuwa CCM imekuwa na kawaida ya kuandaa mazingira ya uchakachuaji wa matokeo toka mwanzo na kuwa hata kutokuwepo kwa msimamizi huyo ofisini na njama za CCM kutaka kuvuruga zoezi hilo kama ilivyotaka kufanya mwaka jana kwa kumzuia aliyekuwa mgombea urais wa Chadema Dkr Slaa kuhutubia katika viwanja wa Mwembetogwa kwa kuwatoa wanafunzi wa sekondari ya wazazi wa CCM Mwembetogwa kuigiza kufanya bonanza la kusaka vipaji katika uwanja huo hali iliyoamusha jazba kwa wananchi na kutoa hukumu dhidi ya CCM.
Hata hivyo alisema kuwa Chadema imejipanga kukabiliana na vituko vyote vya CCM katika uchaguzi huo ambao ushindi kwa Chadema upo wazi kwa kata zote.
Huku Mbunge Msigwa akidai kuwa tayari amewasiliana na msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini kumjulisha juu ya tukio hilo na kuwataka wana Chadema na wananchi kukumbuka kutoka hukumu kwa CCM siku ya uchaguzi.
Hata hivyo katika hali ya kujiami na njama hizo za kuachiwa ofisi viongozi hao wa Chadema walilazimkika kumwacha mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga Samba na wafuasi wawili pekee ndani ya ofisi hiyo na msafara mkubwa uliokuwa umewasindikiza wagombea hao wa udiwani kata ya Gangilonga na Kitanzini Miyombini kuondoka eneo hilo na kwenda kata ya Kitanzini kwa ajili ya kumsindikiza mgombea wao Gervas Kalolo kurudisha fomu ambako nje ya ofisi ya msimamizi msaidizi wa kata ya Kitanzini Miyomboni walishangazwa kumkutana Lucas Wikes ambaye ni msimamizi msaidizi wa kata ya Gangilonga aliyetelekeza afisi yake kitendo kilichowatibua zaidi wafuasi wa Chadema na kutaka kumpa kichapo kiongozi huyo.
Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonokulima alieleza kusikitishwa kwake na hatua ya kukosekana kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata ya Gangilonga na kuwa chama chake kinajipanga kufikisha malalamiko kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi.
Huku Wikes akijitetea juu ya kutokuwepo ofisini kuwa alilazimika kuondoka ofisini baada ya yeye kuwekewa pingamizi la kuwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata hiyo na hivyo kuondoka kwake ni sahihi kwani hata angekuwepo asingeweza kupokea fomu hiyo.

Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini Teresia Mahongo alisema kuwa kukosekana kwa msimamizi huyo msaidizi kwa leo si kosa kwani siku ya mwisho kurejesha fomu ni kesho ambapo wasimamizi wasaidizi wa vkituo vyote viwili hawatatakiwa kuondoka hata sekunde moja katika vituo hadi muda wa mwisho wa kurejesha fomu uliopangwa na tume ya uchaguzi ya Taifa.BOFYA HAPA
CDM lazima ishende gangilonga kiurahisi kama kupapasa maiti vile.Wapi manyama mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu iringa a.k.a mzee wa kujidanganya??
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
cdm lazima ishende gangilonga kiurahisi kama kupapasa maiti vile.wapi manyama mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu iringa a.k.a mzee wa kujidanganya??
somo kubwa la chadema.

Inaelekea ile amri ya kuwatimua watumishi wote ambao majimbo au kata zao zinakwenda kwa upinzani bado ipo.
Jiulize kama ingekuwa ni ccm wanarudisha fomu ofcourse asingekimbia. Somo kubwa hapa kwa chadema ni kwamba
never ever ever and ever rudisha fomu siku ya mwisho.
 
mfanyaji

Member
Feb 1, 2011
76
0
lakini yul mama anakubalika maana hata huyo mpinzani wake walipishana kura 4 tu katika maoni.tena hatumii hongo wala nini kama mwenzake.chadema sometimes tunajisahahu sana.mbwembwe nyingi matendo kidogo.
 
Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,339
2,000
Lakini yul mama anakubalika maana hata huyo mpinzani wake walipishana kura 4 tu katika maoni. Tena hatumii hongo wala nini kama mwenzake.

Chadema sometimes tunajisahahu sana.mbwembwe nyingi matendo kidogo.
<br />
<br />

Huyo mama angekuwa anakubalika angeshinda. Alikataliwa na wapigakura ndio maana akasindwa. Kura hata 1 kwenye kura za maoni ya kata inamaana kubwa sana!

Sijakuelewa unaposema cdm wanambwembwe nyingi, matendo kidogo. Wamemsindikiza mgombea wao kurudisha form, tena siku 1 kabla, msimamizi wa uchaguzi akaingia mitini. Hapo mwenye mbwembwe au mwenye matendo kidogo ni nani!? Na aliyejisahau hapo ni nani!?

Tafakari kabla hujatuma post yako! This is the place for GT!
 
Aggrey86

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
855
195
Huyo mama pia anakubalika kata ya Gangilonga hasa wakina Mama wenzake wanampigia sana kampeni so Cdm wasijisahau wafanye kazi sana km kweli wana nia ya kushinda!
 
ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
5,991
2,000
Francise godwine ulikuwa miongoni mwa waandishi wa vyombo vya habari (iringa kupitia radio moja maarufu)mliokuwa mna wahoji mh. Msigwa na mgombea wa udiwani ndg kalolo mwaka jana (2010) novemba. Kalolo alimlaumu mh. Msigwa kwamba kamtelekeza baada ya kupata ubunge.
Mh. Msigwa akajibu" msimsikilize kichaa huyo. Nani asiye fahamu ukichaa wake?
Swali: Mgombea ndg kalolo ukichaa wake umekwisha? Kauli zetu zinakanganya.
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,581
0
Hii hatari sana, sasa itakuwaje! Tume inabidi iangalie upya hii system ya kutumia watendaji wa kata na Wakurugenzi wa Halmashauri ni wana CCM hao.
 
deecharity

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
890
500
Francise godwine ulikuwa miongoni mwa waandishi wa vyombo vya habari (iringa kupitia radio moja maarufu)mliokuwa mna wahoji mh. Msigwa na mgombea wa udiwani ndg kalolo mwaka jana (2010) novemba. Kalolo alimlaumu mh. Msigwa kwamba kamtelekeza baada ya kupata ubunge.
Mh. Msigwa akajibu" msimsikilize kichaa huyo. Nani asiye fahamu ukichaa wake?
Swali: Mgombea ndg kalolo ukichaa wake umekwisha? Kauli zetu zinakanganya.
kama hujui kitu kaa kimya we nae yule anaitwa abuu majeki ndie alijibiwa hivyo na sio kalolo kaka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom