Elections 2010 Mgombea udiwani wa chadema ahamia ccm

mtiwadawa

Member
Aug 27, 2010
24
0
Mgombea udiwani wa kata ya Endasaki,Wilayani Hanang,Mohamed Tandu amehama chama chake na kuhamia CCM. Jambo hilo linamfanya mgombea wa CCM kupita bila kupingwa.

Source: Mwananchi,16.09.2010,ukurasa wa 8.

Maoni: Chadema msikurupuke kupata wagombea,kama nina kumbukumbu sahihi huyu ni mtu wa 3 ambaye ana impact kwa chama tangu kampeni zianze.
 
Haitishi na wala haimlazi Dr Slaa macho. huyo ni wale wanaotumiwa na CCM kujifanya CHADEMA halafu wahamie tena CCM
Babu yangu kwa upande wa mama alikua kada wa CCM nampaka akapewa jina la chairman. alipokua mahututi hospitalini hakuna hata mtu mmoja wa CCM aliyekuja kumuona. alipofariki wakaleta libedendera lao liwe kwenye jeneza mbona ndugu zangu walilikataa nakulitupa.

Hata mimi nilikua CCM kama nini lakini sasa ninayemuamini ni Dr Slaa tuu. Slaa for a president
 
NILIWAAMBIA hapa
CCM isiwapokee viongozi wanaohamia kutoka ccm bila ya kuwapeleka jando kwanza.
Wasipewe uongozi hata kama ni kikwete kahamia leo tusimpe hata ujumbe wa shina mapaka akolee na kuhitimu jando letu kwanza
 
Mtu yeyote mwenyea akili unapaswa kufikiria kitu kimoja, inakuwaje kuhama kwa wagombea ni kutoka CHADEMA kwenda CCM tu? Mbona hatujasikia CUF, TLP, UPDP, DP, SAU kwenda huko CCM. Kwa jinsi hilo linchi lilivyofisadiwa kuna kila uwezekano kwamba wagombea hao wanaohama wananunuliwa! Hili ni tatizo la kitaifa..............uadilifu, and mark my words hata hao wagombea udiwani wa CCM kama una milioni kumi anahama kiulaini tu kuja CHADEMA.
 
Political prostitute in action.... si vibaya sana maana angeondoka baada ya kushinda uchaguzi ingekua mbaya zaidi!!! NJaa hizi bana zinaumiza kweli, mtu mzima anakua changudoa wa siasa
 
Political prostitute in action.... si vibaya sana maana angeondoka baada ya kushinda uchaguzi ingekua mbaya zaidi!!! NJaa hizi bana zinaumiza kweli, mtu mzima anakua changudoa wa siasa
Ofcourse!
 
Nahisi kila mtu ana haki ya kujiunga chama anachokitaka. Tusimlaumu sana. Hivi angekuwa wa CCM ndio kahamia CHADEMA tugekasirika? Muhimu ni kuwa na umakini zaidi katika kuwapata wagombea.
 
Nahisi kila mtu ana haki ya kujiunga chama anachokitaka. Tusimlaumu sana. Hivi angekuwa wa CCM ndio kahamia CHADEMA tugekasirika? Muhimu ni kuwa na umakini zaidi katika kuwapata wagombea.

Si sula la kukasirika ni suala zima la reality, I would be surprised kama wewe ni mtanzania na unaifahamu Tanzania kutoweza kupambanua some of these fishy moves!!!!!!!
 
Mgombea udiwani wa kata ya Endasaki,Wilayani Hanang,Mohamed Tandu amehama chama chake na kuhamia CCM. Jambo hilo linamfanya mgombea wa CCM kupita bila kupingwa.

Source: Mwananchi,16.09.2010,ukurasa wa 8.

Maoni: Chadema msikurupuke kupata wagombea,kama nina kumbukumbu sahihi huyu ni mtu wa 3 ambaye ana impact kwa chama tangu kampeni zianze.
Kwa mjibu wa Chadema JF, huyu jamaa ana akili sana, na ameona mbali.
 
CHADEMA wangejifunza kutoka kwa CUF. Mwaka 2000 wagombea wengi walinunuliwa na CCM hivyo kukidhoofisha Chama. CUF walichofanya uchaguzi wa 2005 nafikiri mpaka leo watakuwa wanaendelea na utaratibu huo ni kuwa wagombea wote wanaotaka kupitishwa na Chama wanasainishwa mkataba wa Kisheria kuwa pindi watakapojitoa kwa namna yoyote isiyokuja natural kama Kifo au Ugonjwa ambao ni terminal basi watatakiwa kuilipa CUF shilingi za kitanzania Milioni sitini. Hii iliondoa kabisa mchezo wa watu kununuliwa kwa laki moja moja ili alipe milioni sitini.

Chadema wanatakiwa kulifahamu hili na kuchukua utaratibu huu, kwani chama chochote kinachoonekana ni tishio kwa CCM ni dhahiri wagombea wake watafuatwa na TISS pamoja na wagombea wa CCM ili kuwashawishi ama kuwatisha wahamie CCM au kujitoa
 
Mgombea udiwani wa kata ya Endasaki,Wilayani Hanang,Mohamed Tandu amehama chama chake na kuhamia CCM. Jambo hilo linamfanya mgombea wa CCM kupita bila kupingwa.

Source: Mwananchi,16.09.2010,ukurasa wa 8.

Maoni: Chadema msikurupuke kupata wagombea,kama nina kumbukumbu sahihi huyu ni mtu wa 3 ambaye ana impact kwa chama tangu kampeni zianze.

Huu ni umalaya, ni sawa sawa na kutongoza mwanamke ukadhani umepata mchumba wa kuoa kumbe ni changu doa unamwalika aje alale kwako halafu asubuhi akitoka kwako anahamia kwa jirani naye anamtumia.
Waswahili husema jasiri haachi asili, kama ni changu ataendelea kuwa changu tu.

Hawa ni wale ambao wanauzwa na kununuliwa, ni wale ambao kwao laki moja ya kitanzania ina thamani kuliko utu wao, ni wale ambao hawaoni taabu kujidhalilisha kwa kusimama hadharani wakirudisha kadi ya chama fulani ili mradi akitoka hapo anaondoka na elfu kadhaa mfukoni.

Hawa ni watu wa kupuuzwa na kusonga mbele
 
Back
Top Bottom