Mgombea Udiwani wa CCM mbaroni kwa kugawa pombe usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea Udiwani wa CCM mbaroni kwa kugawa pombe usiku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bams, Mar 14, 2012.

 1. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,617
  Likes Received: 2,998
  Trophy Points: 280
  Taarifa nilizopokea usiku huu (majira saa 5: 23) na kuthibitishwa na
  Mbunge wa Chadema Jimbo la Ilemela Haines Kiwia, zinadai Mgombea
  Udiwani kwa tiketi ya CCM Jacksoni Masamaki ametiwa mbaroni akiwa
  katika zoezi la kugawa Pombo ili kuwashawishi wapiga kura. Imeelezwa
  kwa sasa mgombea huyo amepelekwa kituo cha polisi Kirumba. Nitaendelea
  kufuatilia kwa kina.

  Source: Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Kanda ya Ziwa
   
 2. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kula CCM
  Kura CHADEMA
   
 3. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo rushwa kuisha CCM, ni mpaka waliopo wafe wote, wazaliwe wapya!!
   
 4. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  je waweza kutenganisha kobe na gamba lake asife?
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Bado ni tuhuma tuwe makini kuhukumu kama ilivyowahi kusikika kwamba Godbless Lema aliwahi kuwa jambazi. Propaganda za kisiasa ni nyingi kama kapelekwa polisi tuwe na subira kujua kwamba ni kweli au hapana
   
 6. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii ni habari njema kwa wapenda haki na mabadiliko lakin binafsi naona kama ni Danganya toto! Tatizo kubwa litakalotokea ni kuthibitisha kuwa Pombe hiyo ilitolewa ili kurubuni wapiga kura (kama Rushwa). labda tujiulize, kwani kuwa kwenye kampeni kunamzuia mgombea kuendelea kunywa pombe kama ni mnywaji, (na kawaida ya wanywaji si mnazijua)

  Na kama ni kweli hawa watu waliomkamata walikuwa serious na kazi yao, ni kwa nini wasingewakamata na wale walionunuliwa Pombe? Sheria inasema aliyetoa na aliyepokea wote wametenda makosa
   
 7. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nimefanya kisayansi nimemkamkata kobe na kuondoa Gamba lake , Naona damu na tayari aliyekuwa kobe ni Mzoga
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  mwingine huyu hapa:

  428179_407844965908383_100000486493679_1614236_843641567_n.jpg
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,669
  Trophy Points: 280
  Ndio hivyo mama mwenzenu amekamatwa na kupewa mkong'oto juu,hutaki unaacha.
   
 10. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi imeanza, tutasikia mengi toka kwa Magamba.
   
 11. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hizi zitakuwa ni porojo mbona mpaka sasa hazijathibitishwa!
   
 12. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Thubutu,,,,,ukitenganisha kobe lazima awe marehemu. CCM na rushwa ni kama ulimi na mate
   
 13. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,609
  Trophy Points: 280
  Watanzania nao wamezidi,hata pombe nayo ni hongo?!
   
 14. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  inategemea ameitoa kwenye mazingira yapi. Si angetoa kabla hajaanza mchakato wa kugombania?
   
 15. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kaazi kweli kweli, hivi ukiwahonga wapiga kura kwa pombe halafu wakalewa unaanzaje kuwaomba kura?? Mtaelewana kweli??

  Kweli magamba.com wamebanwa kote kote... Kuanzia Meru, Kiwira hadi Kirumba!
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Muacheni Mungu aitwe Mungu
   
 17. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mods. unganisha hii post na ile inayosema alipata kichapo baada ya kukutwa akigawa pombe maana ni huyu huyu inawezekana amekuja na nguvu ya pesa...
  amedanganywa
   
 18. M

  Matapishi Member

  #18
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  jamani ee tuspotoshwe na watu wasiotaka maendeleo hizi tuhuma si za kweli hata kidogo,ndo maana hata alie positi hii habari hakuweza kuikamilisha kwa undani,hii inatokana na siasa majitaka ambazo ni za kumchafua mtu, mgombea udiwani wa ccm kata ya kirumba bw.jackson masamaki hayuko mbaroni na hajafanya kitendo hicho.Kwaiyo ndugu zanguni tuweni waungwana katika kipindi hiki cha kampeni tusiposti kitu kwa mapenzi ya mioyo yetu bali tupositi ukweli.
   
 19. M

  Matapishi Member

  #19
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Si kweli maana kuna watu wanataka kuudanganya umma wa Watanzani
   
 20. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Matapishi yako yananuka sana aisee.
   
Loading...