Mgombea UDIWANI kata ya mwawaza ni mwizi - BABA YAKE mzazi

Huyu baba anawazimu ni mnafiki na mzandiki....katumika vibaya...nadhani wananchi wanamjua...kwani wizi anaufanyia mbali?
 
ameuza ng'ombe kumgomboa mwanae, atueleze vizuri nani alimpa izo pesa na kwampango upi? na je alipewa risiti?kwanini takukuru wasiojiane naye?
 
Mahakama ya Tanzania ndiyo iliyosema the guy is innocent,kama baba ana uhakika aende mahkamani akakate rufaa na kusema mahakama ilisahau.Lakini wakati mzee huyu PETER MHOLA ana zungumza alikuwa katika hali gani?

CCM kwa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi wameona ni bora wamchafue mgombea wa CDM.Mzee wammenyesha Gongo kwa siku mbili mfululizo,wamempandisha kwenye jukwaa wakiwa wamemlisha maneno,lakini mwisho wa siku kitendo hicho kiliwakera sana wazee wenzake ambao wanajua sifa za Anthony Mhola na kuamua kujivua gamba kutokana siasa za maji taka ambazo hazitatui matatizo yao.

Wamepiga risasi wakijua ni mgombea aliyemsumbua sana marehemu diwani Magina,kiasi inaaminika walichakachua kwenye uchaguzi uliopita.Anthony Peter Mhola ni mtu makini, mwanaharakati na mhanga wa mazingira duni ndani ya miaka ambayo CCM na baba yake TANU wametawala.Waja wakikuchukia mengi watakuzushia




Baba amwumbua mtoto wake anayegombea udiwani

Jumatatu, Octoba 15, 2012 06:27 Na Sam Bahari, Shinyanga

*Amtangaza hadharani kuwa ni mwizi, hana sifa
MGOMBEA udiwani wa Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga, Anthony Peter (CHADEMA), juzi aliumbuka baada ya baba yake mzazi kumtangaza katika mkutano wa hadhara, kuwa hana sifa za kuwania nafasi hiyo kwa madai kuwa ni mwizi.

Hali hiyo ilijitokeza katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni katika uchaguzi mdogo, ambao umeitishwa baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo Charles Magina, kufariki dunia kwa ajali ya pikipiki.

Katika mkutano huo, mzazi wa mgombea huyo mzee Peter Molla (62), aliwaacha hoi wananchi waliohudhuria mkutano huo pale alipomshambulia kijana wake akisema kuwa, hafai kuwa kiongozi.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Molla alisema pamoja na kuwa mwanaye huyo hapendi kufanyakazi, licha ya kuwa na umri mkubwa na kwamba muda mwingi amekuwa akizurura kwa ndugu zake kijijini bila ya mafanikio.

Molla alisema, hivi karibuni aliuza ng’ombe zake kwa ajili ya kwenda kumuokoa mgombea huyo, baada ya kukamatwa na polisi usiku kwa kosa la kukutwa na bunduki kinyume cha sheria.

“Mimi sikujua nilidhani nimezaa mtoto wa kiume ambaye atakuja kunilea na kunitunza uzeeni, kumbe hakuna kitu, amenitelekeza hapa mnaniona na umri huu nimebaki napata shida.

“Siyo siri mwanangu amekuwa mwizi, hawezi kukaa sehemu moja anatangatanga ovyo na makundi ya vijana wenzake anaozunguka nao huku wakimshauri mambo machafu, hao jamaa zake nao ni wezi,” alisema.

source wavuti na magazeti ya jana (mtanzania).

MY TAKE; IMEKUWAJE CHAMA KINASIMAMISHA MGOMBEA WA NAMNA HII BILA KUMCHUNGUZA KWANZA???
 
Wazee wananisikitisha sana. Wanatumiwa kwenye kampeni afu wanatelekezwa jumla. Kama mwanae mwizi si ndo angenyamaza mwanae apate a decent work ya kufanya? Very fishy!
 
Mkuu hapo kigezo kilikuwa ni kutafuta mwizi kidogo, kwani hujui ukisha kuwa mwana ccm tu unatakiwa kufunguliwa mashitaka ya kuunga mkono wizi

my take; imekuwaje chama kinasimamisha mgombea wa namna hii bila kumchunguza kwanza???
 
Mtoa mada naomba utwambie ushahidi alio utoa kuhusu mwanae kuwa mwizi.
 
Heh, hoja ndo inaondoka hivyo we bado unasubiri tuanze!
Afu huyo baba ni mwehu, mtoto kamlea mwenyewe anakuja kutupiga kelele Great thinkers!.
Tunapojadili vitu tuwe na hakika na kile tunachojadili kama ndiyo haswa kinatakiwa kujadiliwa tusije tukawa tunajadili kisicho mjadala. Hivi ni baba yake huyo kijana ndiye kaleta humu hiyo hoja kwamba mtoto wake ni mwizi, au bandiko hili limeletwa na mtu anayejiita rais wa migomo?

Sasa kama hata hilo hulioni unajadili nini sasa?
 
Taarifa za kupikwa hizo! Magamba yanatapatapa hayana pa kushika! Aliyasemea kwenye mkutano wa chama gani hayo?
 
Jamani nawaomba msikurupuke. huyo baba amesema mwanae alishawahi kufungwa kwa kosa lolote? Kumbukeni ni mahakama pekee ndicho chombo chenye uwezo kisheria wa kusema huyo mtoto wa huyo mzee ni mwizi au la!! Kitendo tuu cha kukutwa na hiyo silaha(kama ni kweli) haimaanishi ni mwizi! Na kama alibambikwa hiyo silaha je? Na baba yake alikuwa wapi siku zote kusema huyu kijana wake ni mwizi mpaka aje kusema mbele ya halaiki ya watu? Think before u judge smone
 
Diwani jitoe, kisha hamishia ajira yako kwenye kihenge cha baba yako! Mlize kwa kwenda mbele!.
 
kumbe ni mgombea wa cdm?? ngoja nikae pembeni mapigo ya moyo yameongezeka gafla. nilidhani ni wa m.a.g.amba!!
 
kama ni kweli basi baba huyu anapaswa kulaumiwa kwa makosa mawili au matatu, mosi malezi mabaya kwa mwanae yaliyopelekea kuwa mwizi, yeye mwenyewe ni mwizi mwanae karithi na tatu ameshindwa kumchukulia mtoto wake hatua za kisheria huku akijua wazi kabisa ni mwizi!!! hizi tumbo jamani hadi mtu unafikia kumsaliti mwanao wa kuzaa kisa vijisenti vya magamba nahisi mkewe angegombea angetangaza asipewe kura ni malaya!! tumbo?????
 
Ukweli ukidhihiri ubaya hujitenga..hongera baba yake mana umesema ukweli haya wana CDM munasemajeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Huyu mzee kaandaliwa na ccm kuja kumchafua mgombea wa cdm kama angekuwa mwizi angelikuwa gerezani cku nyingi lakn mwanga na giza havikai pa1
 
Huyo mzee amechunguzwa akili yake? Na CCM kama imemtumia huyo mzee kwa hila ili atangaze hayo na watu wakagundua basi mbinu hiyo itaimaliza kabisa CCM

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom