Mgombea udiwani kata ya kimara-baruti ni rushwa kwa kwenda mbele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea udiwani kata ya kimara-baruti ni rushwa kwa kwenda mbele

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyange, Jul 27, 2010.

 1. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ama kweli watanzania sijui itakuwaje! Napiga picha wajukuu zetu watatuelewaje jinsi tulivyo changia kuharibu nchi tuliyo jaliwa yenye maziwa na asali.

  Juma pili nikiwa nyumbani, baada ya kutoka kazini, nilikuta ujumbe kuwa natafutwa sana kuna kikao cha wanachama wa thithiem, japo mi ni mwanachama lakini sijawahi kumpigia kura mwanachama wangu kwa sababu mi nachagua uwezo wa mtu na si chama. Ukweli ni kwamba nimeshiriki kupiga kura mara nne tangu kuzaliwa, japo huwa nachagua uwezo wa mtu na si chama hivo sijawahi kumchagua mgombea wa thithiem kwakuwa wanaoteuliwa kugombea binafsi naona hawafai.

  Nikiwa naangalia taarifa ya Aljazira jioni, nikapigiwa simu na mzee maarufu kuwa nasubiliwa. Ikabidi niende mbio kuona kulikoni. Kufika kwenye kusanyiko hilo, mara VX ikawasili ikiwa na mgombea mtarajiwa wa udiwani akiongozana na mamaa. Mara akaanza kuelezea kwa nini ametuita, pia kuelezea jinsi alivyo tenda kipindi kinacho malizika cha miaka mitano iliyopita. (alikuwa diwani wa Kimara Baruti). Na baada ya hapo akaomba watu watoe maoni na ushauri.

  Nilikuwa wa kwanza kushauri, nikasema ' nakushukuru sana mtarajiwa make we si wa design ninazo ziona za wagombea, kwani kugombea ni kwenda kutatua matatizo ya watu hivyo kutoa pesa, haiingii akilini kwa kuwa uongozi ni shida tupu kwa nini ununue shida? Sana sana tunatarajia wanachama wa ku-support ili uweze kuweka mafuta kwenye gari ili uwazungukie wapiga kura wako na kuwaelezea malengo yako. Nikasisitiza kuwa, ukiona mgombea anatoa fedha, ujue kuwa hajui anafanya nini na akiwa kiongozi atafanya nini'

  Wakati akijibu ushauri huo, alijibu kuwa ' mgonjwa mwenye kansa ya damu, akienda Hospitali dakitari hawezi kumwacha hivihivi, atampa panado ili impunguzie maumivu tu japo kuwa ina tazamiwa atakufa tu'
  Kauri hii imethibitisha kuwa kweli chama kilichopo madarakani hakijui kina fanya nini, na viongozi wa thithiem wamezoea rushwa na hivyo hawawezi kusaidia nchi.

  Mara baada ya yeye kuondoka kumbe kaacha mtu agawe sh. 5,000 kwa waliofika! Mi nilikimbia nikaona ni uchuro!
  WADAU KWELI NCHI HII THITHIEM INAIPELEKA WAPI?
   
 2. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  thats is politics man not ccm
   
 3. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  You are not clear, please explain clearly. what do you mean
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Waacheni bana
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, huyo anaitwa Mahmoud M.

  Anyway, ni vyema kuwa hukupendelea na ulisema wazi kuwa matumizi ya pesa ili kupata ushindi yalikuwa ni kuonyesha kutotambua majukumu ambayo alikuwa akiombea kura. Hasa kwakuwa alikuwa kiongozi kwa nafasi hiyo kwa miaka kumi iliyotangulia, ni dhahiri kuwa anajua kuwa kura zenu hazimmanishi kuleta maendeleo na badala yake ni kumuwezesha kuwa katika Kamati mbalimbali za maamuzi ambazo kwa kiasi kikubwa humsaidia yeye kufanikisha malengo yake kiuchumi.

  Kazi ipo, ila kama wananchi wengi zaidi wataelewa nia mbaya hizi za wagombea, mabadiliko ya maana yanaweza kufikiwa. Kuna wagombea wengi wazuri ambao hawana pesa za kugawa holela hivyo lakini wana nia njema sana na wananchi wao. Msiwapoteze hao. Wasaidieni ili washirikiane nanyi kuleta maendeleo mnayoyahitaji. Siasa za pesa zinachafua hata wagombea wasionazo. Si lazima kutumia pesa kutafuta kuchaguliwa. Imani ya wapiga kura haiko kwenye kiwango cha pesa mtu anachoweza kugawa bali kwenye nia ya mgombea kushirikiana na wananchi katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.
   
 6. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  HIYO NAFUU SOMA francisgodwin.blogspot.com uone kasheshe ya MTIKILA NA PROF. MWALYOSI. UCHAFU MTUPU. Hatari zaidi ni kuwa hata huyo Dr. Mwakyembe ni mdau wa ufisadi. tunazo taarifa za ndani za washirika wake, Daniel Yona na aliyekuwa Mkurugenzi wa NBC Bw. Kitomari na harakati zao za kuinunua Wilaya ya Ludewa. Wanachokizungumza hadharani sicho wanachofanya mafichoni.
  MBUNGE WA CCM ADAIWA KUUZA MALI ZA WILAYA ILI APATE FEDHA ZA KUGOMBEA UBUNGE TENA


   

  Attached Files:

 7. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umeshamripoti huyu mtoa rushwa kwa PCCB kwani viongozi watoa rushwa hawatufai kabisa, toa ripoti sehemu husika ili jina lake lifutwe kwenye majina ya wagombea. Ndio maana Kimara hakuna barabara, maji ni shida kumbe jamaa alikalia ifisadi ili apate hele za kununua uongozi
   
 8. R

  Renegade JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Ala kumbe kutoa rushwa ni Politiks !!! Hii nilikuwa siijui.!
   
 9. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mwenzenu sijui hata Takukuru wanapokeaje taarifa make hata namba za simu hawatoi ila nimewahi kupokea msg ya Takukuru ikiwa imeficha namba. Sasa sijui hapa tutashirikiana nao vipi kama wana ficha namba zao!
   
 10. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Tuambie basi kama ulilamba hiyo 5000 au uliishia kuona "uchuro"?
   
 11. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ilibidi nitimue
   
 12. K

  Kinte Member

  #12
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Unamzungumzia Mringo mkuu? Huyo ni msanii, anaishi kwa kuupepeta mdomo, ni ajabu anaendelea kuomba udiwani kwa miaka yote hiyo aliyokuwa diwani, hakuna mwelekeo wa kuisha kwa matatizo sugu ya Baruti hasa maji ingawa bomba linapita hapo, sijui anatafuta nini tena!! Sishangai kama anawanunua kwa style hiyo. Wakati kama huu, wazee wa vijiweni Baruti ndio wa mavuno, kuna watu wanajiita wajumbe, my foot!!
   
 13. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mkuu umepatia ndo huyo. Just imagine, Rais alipotembelea Kimara, tunakumnuka gari lake lilimzimikia, alisema kuwa: kama kuna watu wanafanya biashara ya maji, watumie bei iliyo wekwa na EURA ya ndoo shs. 20. Leo asubuhi nimeona gari hilo likizunguka, nikalisimamisha na kuuliza wanauza bei gani,wakajibu ndoo ni shs. 200 mzee! Hivi mtu anayeheshimiwa kama Rais anaweza akasea jambo afu likawa halitekelezwi? mbona mambo TZ amri yake nikama ya akina Joti!
   
Loading...