Mgombea udiwani kata ya Daraja Mbili, Arusha (CHADEMA) akamatwa na polisi

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Mgombea udiwani kata ya daraja mbili CHADEMA Kamanda Prosper Msofe amekamatwa na polisi jioni hii.Amekamatwa baada ya Kada mmoja wa CCM kudai kuwa mgombea amemzuia kufanya kazi.

Ilikuwa hivi:
Mgombea wa CHADEMA alikuwa anaongea na wapiga kura wake, mara akatokea jamaa wa CCM na kuanza kuporomosha matusi, kisha akawapigia simu polisi kuwa anafanyiwa fujo, baada ya polisi kufika wakamchukua na kumpeleka kituoni, na sasa yupo ndani Lock up hadi kesho,
 
IGP Mwema aongee na watu (police) wake. Watasababisha balaa.
 
Polisi sasa wameacha kabisa ku deal na mambo ya msingi badala yake wameamua ama kujikuta wakilazimishwa kuwa anti chadema software,huwa wanakaa kusubiria tu waambiwe chadema wapo sehemu fulani ndipo wanaona kuwa wapo kazini!

Habari ya uhalifu wameachana nayo kabisa,si ajabu sasa ukienda kuripoti uhalifu mkubwa kama ujambazi nk ukaambiwa hakuna askari,wote wapo kwenye harakati za kukimbizana na chadema!!any how,tutafika tu hata kwa mikongojo.
 
Lakini kampeni si hata jela hiyo ndio fursa pekee kwa wapiga kura kukutana na mgombea wao.
 
Wala asijali, mtoto kabla hajaota meno lazima aharishe. Ndo mchakato wa ushindi. Mambo madogo tu hayo kamanda.

ndo serikali ya tanzania ilivyo by now, muda wa mabadiliko ukifika huwezi kuepuka, please serikali better mkawa wapole tu
 
Wana kazi hawa poliCCM .....wakiitwa kwenye mambo ya msingi huwa hawaendi kabisa ila kwenye ishu za CCM wako mstari wa mbele....
 
Mungu ampiganie atoke kwenye lock up naendelee na kampeni hadi ushindi upatikane
 
Lakini kampeni si hata jela hiyo ndio fursa pekee kwa wapiga kura kukutana na mgombea wao.
Hapana!ni wakati pekee sasa wa polisi kukaa chini na kujiuliza wao ni nani ndani ya jamii,wauvae umuhimu wao kwa jamii na kukataa kutumika kama robot,sijui huwa hao polisi wanawaza nini wanapotumwa kwenda kuvunja sheria wanazostahili kuzilinda na kuzisimamia polisi wasasa wamekuwa si tofauti na mashine zisizo na utashi kabisa.
 
kamanda asikate tamaa hayo ni majaribu ya kawaida tu, hata mandela alikuwa mfungwa, leo hao hao waliomfunga wanamwabudu.... polisi ni ccm na ccm ni adui wa watanzania, kwa hiyo hta polisi ni maadui wa watanzania, lakini Mungu wetu si kiziwi.. atayajibu yote hayo mwisho wa ubaya nia aibu cdm itashinda kwa nguvu zoote
 
Hao policcm hawajui watumika kama c.....om; kwanza wameshakamata mahabusu waliowatoroka, Igp anatakiwa afunguliwe mashtaka the Hague. Simply ameshindwa kazi: Hii nduo hasara ya watu kuteuliwa bila kuwa vetted they are capable:

wafanye watakalofanya tutampigia kura huko huko mahabusu:
 
Hao policcm hawajui watumika kama c.....om; kwanza wameshakamata mahabusu waliowatoroka, Igp anatakiwa afunguliwe mashtaka the Hague. Simply ameshindwa kazi: Hii nduo hasara ya watu kuteuliwa bila kuwa vetted they are capable:

Wanaume wa ukweli.........hutumia dume!
 
Back
Top Bottom