Mgombea udiwani CHADEMA Msalato akuta bundi chumbani kwake.

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Msalato, Mkoa wa Dodoma zimezidi kupamba moto, huku Chadema na CCM vikionyesha kuchuana vikali.Hali hiyo imesababisha kuwapo kwa vituko na vitimbwi kadhaa hasa imani zinazohusiana na masuala ya ushirikina.
Imani za ushirikina zilibainika juzi baada ya bundi kukutwa chumbani kwa mgombea udiwani wa Chadema, Nsubi Bukuku ilhali hakuna tundu lolote chumbani au nyumba linalowezesha ndege mkubwa kama bundi kuindia.
bukuku4.jpg
“Hatukatai kuwa huyu ni ndege kama walivyo ndege wengine, lakini kwa imani zetu Waafrika ndege huyu ni nadra kuingia chumbani kwa mtu na mara nyingi hutumiwa kwa masuala ya ushirikina,” amesema Alphonce Mawazo ambaye ni Meneja wa kampeni.
“Kwa hiyo tunaamini sasa wenzetu CCM Msalato, sera zimewashinda wameingia kwenye masuala ya ushirikina.”
Licha ya tukio hilo, kampeni hizo zimeshuhudia kuwapo kwa mbinu mpya ya kusambaratisha wafuasi wanaosikiliza mikutano ya kampeni, nyuki wamekuwa wakiwekwa katika mifuko ya plastiki na kufunguliwa katikati ya kundi la watu, hali ambayo husababisha watu kukimbia.
Tukio hilo lilitokea Kitongoji cha Chikowo, Chadema walipokuwa wakimnadi mgombea wao ghafla vijana ambao hawakufahamika aliyewatuma, walifungulia nyuki ambao waliwashambulia watu hao.
“Walianza vipigo wameona tunaendelea kuvumilia,watu wanazikubali sera zetu na kumkubali mgombea wetu,sasa wameanza kutumia mbinu chafu zaidi ushirikina na Nyuki,lakini nataka kusema mbinu zote hizo zimeshindwa maana tuna hakika tarehe Novemba 4, Kata ya Msalato itakuwa chini ya Chadema,”alisema Mawazo.
Kwa upande wake, Bukuku amesema vitibwi vinavyofanywa na wapinzani wake, haviwezi kurudisha harakati zake za kutaka kuikomboa kata hiyo ambayo haina zahanati tangu uhuru. Chanzo: Mwananchi.
 
Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Msalato, Mkoa wa Dodoma zimezidi kupamba moto, huku Chadema na CCM vikionyesha kuchuana vikali.Hali hiyo imesababisha kuwapo kwa vituko na vitimbwi kadhaa hasa imani zinazohusiana na masuala ya ushirikina.
Imani za ushirikina zilibainika juzi baada ya bundi kukutwa chumbani kwa mgombea udiwani wa Chadema, Nsubi Bukuku ilhali hakuna tundu lolote chumbani au nyumba linalowezesha ndege mkubwa kama bundi kuindia.
bukuku4.jpg
"Hatukatai kuwa huyu ni ndege kama walivyo ndege wengine, lakini kwa imani zetu Waafrika ndege huyu ni nadra kuingia chumbani kwa mtu na mara nyingi hutumiwa kwa masuala ya ushirikina," amesema Alphonce Mawazo ambaye ni Meneja wa kampeni.
"Kwa hiyo tunaamini sasa wenzetu CCM Msalato, sera zimewashinda wameingia kwenye masuala ya ushirikina."
Licha ya tukio hilo, kampeni hizo zimeshuhudia kuwapo kwa mbinu mpya ya kusambaratisha wafuasi wanaosikiliza mikutano ya kampeni, nyuki wamekuwa wakiwekwa katika mifuko ya plastiki na kufunguliwa katikati ya kundi la watu, hali ambayo husababisha watu kukimbia.
Tukio hilo lilitokea Kitongoji cha Chikowo, Chadema walipokuwa wakimnadi mgombea wao ghafla vijana ambao hawakufahamika aliyewatuma, walifungulia nyuki ambao waliwashambulia watu hao.
"Walianza vipigo wameona tunaendelea kuvumilia,watu wanazikubali sera zetu na kumkubali mgombea wetu,sasa wameanza kutumia mbinu chafu zaidi ushirikina na Nyuki,lakini nataka kusema mbinu zote hizo zimeshindwa maana tuna hakika tarehe Novemba 4, Kata ya Msalato itakuwa chini ya Chadema,"alisema Mawazo.
Kwa upande wake, Bukuku amesema vitibwi vinavyofanywa na wapinzani wake, haviwezi kurudisha harakati zake za kutaka kuikomboa kata hiyo ambayo haina zahanati tangu uhuru. Chanzo: Mwananchi.

SWALI. Je aliingiaje mwanawani? na je ni ishara ya nini?
 
SSM =Rushwa-tunguli inashika kasi sana!!! But 2015 kata mti panda mti!1
 
Duh!! Ndio maana tukawa hatuna maendeleo kwasababu ya kuendekeza uchawi kwa ubinafsi wetu.EE mungu tusaidie na uwaweke maalbino salama.
 
Hahahaha! kazi ipo, mbona kama mgombea wa CDM ana vituko. Pamoja na hayo, amani itawale na mshindi apatikane kwa halali.
 
Hakuna uchawi katika haki .mabadiliko hayazuiliki kwa uchawi.Mungu amlinde na mbinu zote wanazopanga wapinzani wake zishindwe
 
Duh, bundi tena ndani chumba! Siku ya kupiga kura itabidi Wachungaji na Mashekhe watangulize maombi icje ikawa sanduku la kura ndo Bundi mwenyewe anameza kura za CDM. Kazi kweli kweli!
 
CCM wanaamini kamati za ufundi! teh teh teh! marehemu sheikh yahaya alisema amemwekea JK ulinzi usioonekana!
 
bukuku4.jpg
Licha ya tukio hilo, kampeni hizo zimeshuhudia kuwapo kwa mbinu mpya ya kusambaratisha wafuasi wanaosikiliza mikutano ya kampeni, nyuki wamekuwa wakiwekwa katika mifuko ya plastiki na kufunguliwa katikati ya kundi la watu, hali ambayo husababisha watu kukimbia.

Hilo la NYUKI Msaada tutani! kwa huko MSALATO watu wanfuga nyuki, how come wawe ni CCM tu na si CDM au wengine! na nyie tumieni NYIGU!
 
Bundo ndo ushindi sawa kabisa!
Ishara njema peopleeeeeeeeezzzz!
 
Mitaji mikuu ya CCM katika siasa ni wizi, rushwa, ujinga wa wananchi na ushirikina. Hata hivyo hayo yote tumeshayapatia ufumbuzi mapema kabla ya 2015. CCM wajiandae kuangukia pua katika chaguzi hizi ndogo na uchaguzi mkuu wa 2015 utakuwa msiba mzito kwao. CCM HAIKUBALIKI, TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA. PLAY YOUR ROLE, WE CAN.
 
Back
Top Bottom