Mgombea udiwani CHADEMA kata ya Kati apata kipondo Korokoroni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea udiwani CHADEMA kata ya Kati apata kipondo Korokoroni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngongo, Sep 23, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kata ya Kati mjini Arusha Bwana Simba aumizwa vibaya kituo cha polisi wilaya ya Arusha.Bwana Simba alikamatwa na polisi kwa sababu ambazo bado sijazithibitisha.

  Bwana Simba alishambuliwa vibaya na watuhumiwa wenzake aliowakuta wamewekwa rumande katika kituo cha polisi hadi kuzimia na baadae kukimbizwa hospital ya mkoa wa Arusha [Mt meru Hospital] kwa matibabu.
   
 2. m

  mnazareti Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :mad2:hizo ni hila za CHAMA CHA MABWANYENYE...... mwaka huu wao watasoma namba.
   
 3. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Wameshaanza hujuma zao na mungu yupo tu

  kijana atapona na kura atapata za kutosha
   
 4. h

  hagonga Senior Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Please tunataka kujua sababu ya kupigwa vibaya hivyo na ilikuwaje kuwa rumande
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  jamaa huyo ambaye ni mgombea wa udiwani Chadema alisema akipata udiwani atafuta kodi zote ikiweko ya masoko pale Arusha (Source, slaa kwenye kampeni za moshi). Binafsi naona serikali na polisi ilichofanya ni sawa tu kumsweka ndani. sasa kama wewe unaahidi utafuta kodi utaendeshaje kata yako? jimbo lako? Nchi yako? yaani hawa ni wababaishaji tu hamna lolote.
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe mwenyewe unayeripoti hii habari unajua ukweli sana tu na ndo maana umekwepa kueleza ukweli kuwa jamaa alitangaza kufuta kodi zote, sasa hata kama wewe ndo ungekuwa unasimamia serikali ungefanyeje? ungeacha mtu wa aina hii aendelee kukampeni? usalama wa taifa unafanya nini
   
Loading...