Mgombea ubunge wa UPDP Igunga

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Pamoja na TBC1 kushindwa kutoa muda wa kutosha kwa habari za Msajili wa Vyama vya siasa na Tume ya Uchaguzi, wametoa muda wa kutosha kwa Mgombea ubunge wa jimbo la Igunga kupitia UPDP! Huyu jamaa alikuwa anaongea kama wasanii wa Zecomedy na mbaya zaidi anaonekana kama kalewa. Kama si hivyo basi huyu jamaa ni mteja wa Mirembe Hospital!!
 
Great thinkers mmemuona mgombea ubunge Igunga kwa tiketi ya UPDP...jamaa ni kituko..katoa vichekesho kibao..lkn ninachokikumbuka ni pale aliposema vijana wanaota jua kama solar power...akisema atatoa ajira kibao
 
mi mwenyewe kanivunja mbavu zangu! Hivi kuna watu wengine wakiwa serious wao wanafanya joke! Angekuwa tarime asingepona
 
Mgombea ubunge kwa tiketi ya UPDP akijinadi kuomba kura huko Igunga,nanukuu;Mkinipa ubunge,nitaanza na vijana>>>vijana mnakaa vijiweni bila kazi>>>Vijana mna very problem>>>Mnakaa juani kama solar panels>>>mkinipa kura zenu,watoto wenu hawataenda na majembe shuleni na badala yake nitauza VX langu na kununua powertillers kwa kila shule>>>Nitanunua matrekta na ninyi vijana msio na ajira ndo mtakuwa madereva,naombeni kura zenu.Yaani sera hazina ushirikiano,english mbovu,mtu anaongea kama kalewa,daah!MUNGU kibariki CHADEMA!
 
kwa faida ya ambao hawakuona:
.....amesema vijana wanaota jua tu siku nzima kama solor power kwasababu hawana kazi
....eti kilimo kwanza, education second
.....amesema marufuku wanafunzi kwenda shule na majembe, atanunua power tiller kwa kila shule
....amesema yeye ni mbele kwa mbele tu......samaki haina reverse
.
Kimsingi gage ya alcohol ilikuwa ipo chini ya Full kidooogo!!!

mimi nimempenda huyu jamaa..........kwenye swala la vijana kuota jua tuuu, kazi hakuna.
 
duh....mimi nilimuona nikashindwa kujua lengo lake hasa ni nini....tena mimi nilibahatika kumuona akicheza ndombolo huku yupo chicha.......tutaona mengi jamani....khaa
 
kwa faida ya ambao hawakuona:
.....amesema vijana wanaota jua tu siku nzima kama solor power kwasababu hawana kazi
....eti kilimo kwanza, education second
.....amesema marufuku wanafunzi kwenda shule na majembe, atanunua power tiller kwa kila shule
....amesema yeye ni mbele kwa mbele tu......samaki haina reverse
.
Kimsingi gage ya alcohol ilikuwa ipo chini ya Full kidooogo!!!

mimi nimempenda huyu jamaa..........kwenye swala la vijana kuota jua tuuu, kazi hakuna.

Hapo hukumsoma vizuri mkuu, kasema ardhi kwanza kilimo baada.
Atauza VX anunue power tila.
 
Mgombea ubunge kwa tiketi ya UPDP akijinadi kuomba kura huko Igunga,nanukuu;Mkinipa ubunge,nitaanza na vijana>>>vijana mnakaa vijiweni bila kazi>>>Vijana mna very problem>>>Mnakaa juani kama solar panels>>>mkinipa kura zenu,watoto wenu hawataenda na majembe shuleni na badala yake nitauza VX langu na kununua powertillers kwa kila shule>>>Nitanunua matrekta na ninyi vijana msio na ajira ndo mtakuwa madereva,naombeni kura zenu.Yaani sera hazina ushirikiano,english mbovu,mtu anaongea kama kalewa,daah!MUNGU kibariki CHADEMA!
Mwishoni mtangazaji alisema hawa jamaa wanafaa kuwa zecomedy, yaani mgombea anaingia na swaga la sebene la Werasoni zenith kisha kuwaambia vijana kuwa suala la ajira litakwisha na hivyo kuotea jua kama solar panel bye bye!!!
 
Mgombea ubunge kwa tiketi ya UPDP akijinadi kuomba kura huko Igunga,nanukuu;Mkinipa ubunge,nitaanza na vijana>>>vijana mnakaa vijiweni bila kazi>>>Vijana mna very problem>>>Mnakaa juani kama solar panels>>>mkinipa kura zenu,watoto wenu hawataenda na majembe shuleni na badala yake nitauza VX langu na kununua powertillers kwa kila shule>>>Nitanunua matrekta na ninyi vijana msio na ajira ndo mtakuwa madereva,naombeni kura zenu.Yaani sera hazina ushirikiano,english mbovu,mtu anaongea kama kalewa,daah!MUNGU kibariki CHADEMA!

Ametokea kilabuni kwetu kuomba kura, anapiga sana mizinga ya ulabu na vocha. Halafu anatuambia risiti ntawapeni kesho
 
Mi mwanzoni nilijua ni intro ya kumnadi mgombea but later on nikaona ni mwakilishi wa Magamba
 
Huyu mgombea ubunge nimemkubali maana amenichekesha sana kwakweli na he knew he was a joker!

Nadhani wasingelaunch wangekosa posho...

Ahadi kama za ndio mzee ya prof J...ametoa zile ahadi za kizamaniiiii
 
Chama kamini hufuatwa na wagombeaji makini.
Inaoneka yeye ndo aliwashinda wote aliongombea nao katika chama chake.
Hebu fikiria aliyekuwa wa mwisho katika kura za maoni za chama chao, anaweza hata kuzungumza kwali?
 
hahahahah! kwa kweli bado nacheka, it was funny, huyu mtu hayuko serious, anadai atawapa mashamba vijana, dah
 
Nimemwona jamaa. Inaonekana ni kweli kalewa. Ila kuna watu wanaopenda jinsi alivyokuwa anaongea na mwenyekiti wake anavyosakata sebene. Ndo maana hata TBC1 nao wakavutiwa wakawapa "air time" ya kutosha. Haikuwa siasa ilikuwa sanaa. yaani burudaaaaani.
 
Back
Top Bottom