Elections 2010 Mgombea ubunge wa CHADEMA Arusha mjini (Lema) akamatwa

Kibs... hivi anko wako akizidi kukutusi, kukuchokoa na kukudharau nyumbani kwako utamuangalia tu??.... eniwei sisemi sana lakini nijuavyo mimi ni kwamba Lema ni style ya Mbowe, they can not hold back once excited, he needs to get super back up otherwise kesi itaisha in 5 days na yeye atafungwa; Lowassa ana nguvu sana and Lema should have known better

I see!! lakini kila penye mwanzo lazima pana mwisho.... iko siku yake huyo EL na si mbali sana.
 
Ilivyokuwa: Lema alikuwa anatoka kwenye mkutano wa kampeni ambao ulifanyika Levorosi na kufungwa saa 12:4 jioni basi wakati Lema anaondoka wapenzi wa CHADEMA wakaungana msafara wakimsindikiza huku wakiwa na mzuka wa ajabu yaani ni honi na miluzi ndiyo ilikuwa imeshamili inakadiliwa magari zaidi ya 30 hivyo ikawa kama kwamba anafanya maandamano na kusababisha jam kama unavyo ujua mji wa arusha walipo fika idara ya maji karibu na Posta Meru polisi walianza kuwa sihi wasitishe hayo maandamano kama walivyo yatafasili, hawakutii amri hiyo wakidai hayo siyo maandamano bali ni msafara wa kumsindikiza mbunge wao nyumbani na walioji kwani msafara mwisho gari gapi? walipo fika mnara wa mwenge ndiyo polisi walipoongezeka nakublock nakuanza kuamrisha baadhi ya magari yaelekee Kaloleni magine centre imradi wawasambaratishe kuna baadhi walikadi amri ya polisi ndipo polisi wakaanza kuwa telemsha kwenye magari yao nakuwapiga kuna jamaa aliumia sana hivyo lema aliamua kwenda polisi kuchukua PF3 ili jamaa akatibiwe alipofika pale reception (Polisi) alimkuta kamanda Basilio alimwambia anamtafuta ndipo alipomwambia “ningilia kwa wapi nipite juu ya meza au nizunguke” akamwambia zunguka Lema akazunguka, alipofika aliopo kamanda Basilio alimwambia nimekuja kwajaziba, Basilio akamwambia "nitakupiga" Lema akamwambia unataka unipige makofi au risasi kama ni risasi piga hapa akimwonyesha sehemu ya kupiga huku akivua shirt na kushika kwenye moyo akiimanisha ndiyo sehemu sahihi ya kupigwa kwa risasi ndipo Basilio nadhani kwa kuona anadhalilishwa maana hayo yote yalitokea mbele ya polisi na wananchi akaamrisha Lema awekwe ndani walimtaka aandike maelezo kabla hajaingia ndani Lema aligoma akitaka wakili wake (Amani) awepo ilibidi awekwe ndani huku wakimsubilia wakili, watu walijazana Polisi wakitaka kujua nini kimetokea kwa mbunge wao wakafukuzwa walitawaywa kwa virungu lakini ilipotimu saa 4:30 watuwalikuwa wamejaa tena wakitaka kujua kama Mbuge wao atatoka au laah, polisi walikuja na kuwaambia wakae mita 200 kutoka kituo cha polisi watu wakagoma kukatokea purukushani safari hii polisi walishinda tena kwani watu walipanda kwenye magari yao na kuondoka mahali hapo na kuja kusiama maeneo ya Arusha City park….
Bw Godbless Lema alitolewa usiku huo huo

Heshima kwako Crashwise,

Maelezo yako ni sahihi kabisa kwa mara ya kwanza umeeleza issue ya Lema bila ushabiki.
Mkuu Lema hana haja ya kubishana na askari ambaye alimshauri vizuri lakini hakutaka kutii tena alimtukana askari kwa kumwambia wewe ni kibaraka wa Kikwete.nadhani unaijua Arusha vizuri kitu kidogo jam.Inaonyesha huko karibu na Lema tafadhali mshauri awe mstaharabu.
 
Polisi baada ya kulinda usalama wa raia ndo wanakuwa mstari wa mbele kuvuruga usalama wa raia. Nawashauri wasiendeshwe na wanasiasa maana 31 Oct 2010 mambo yanaweza kubadilika kabisa wakajikuta waliowapinga ndo wanakuwa maboss wao. Muda huo wanasiasa wa CCM watawatosa
 
I see!! lakini kila penye mwanzo lazima pana mwisho.... iko siku yake huyo EL na si mbali sana.
I agree mkuu... But while that time inakuja, we should appreciate the real time scenario
 
Heshima kwako Crashwise,

Maelezo yako ni sahihi kabisa kwa mara ya kwanza umeeleza issue ya Lema bila ushabiki.
Mkuu Lema hana haja ya kubishana na askari ambaye alimshauri vizuri lakini hakutaka kutii tena alimtukana askari kwa kumwambia wewe ni kibaraka wa Kikwete.nadhani unaijua Arusha vizuri kitu kidogo jam.Inaonyesha huko karibu na Lema tafadhali mshauri awe mstaharabu.

:biggrin1:
 
mpaka sasa ni wagombea wangapi wa upinzani wanashikiliwa na polisi????
1. Arusha
2. Tanga
3. Moshi

Na nilisikia majuzi kuna mmoja wa udiwani sijui ni wapi kala miezi minane kwa kosa la ajabuajabu tu.

Je ni concidence?????? Au mchezo mchafu maana yule wa Tanga anashikiliwa kwa tuhuma za 2008.
 
wakati batrida anafungua kampeni zake alikuwa na msafara mrefu ulioleta jam karibu masaa mawili .hakuna askari aliyesimamisha, kuvuluga wala kupiga watu.Iweje leo kwa lema iwe issue! huyu basilo ni kibaraka na ni mchovu wa mawazo.hatuwezi kuongozwa na wajinga kama yeye
 
Polisi wanasema alikuwa anafanya maandamano yeye anasema sio kweli, ukweli ni kwamba alikuwa kwenye gari sasa suala la kuandamana bila kibali linakujaje?
Siasa za maji machafu.
 
Heshima kwako Crashwise,

Maelezo yako ni sahihi kabisa kwa mara ya kwanza umeeleza issue ya Lema bila ushabiki.
Mkuu Lema hana haja ya kubishana na askari ambaye alimshauri vizuri lakini hakutaka kutii tena alimtukana askari kwa kumwambia wewe ni kibaraka wa Kikwete.nadhani unaijua Arusha vizuri kitu kidogo jam.Inaonyesha huko karibu na Lema tafadhali mshauri awe mstaharabu.
Sikumbuki kuandika habari za kishabiki anyway tuendelea kubisha kwa hoja...ila kura yako kwa Lema nyingine kwa Dk Slaa
 
Lema ana cha kupoteza kuliko mgombea mwingine yeyote kwa kiti cha ubunge Arusha. Yeye ndiye mshindi tayari tena kwa kishindo.....asichofahamu ni kitu kinaitwa hujuma. Ndicho anachofanyiwa Mbowe.

Majasusi maalum wamekwisha wasoma tabia na wanachofanya ni kutumia mbinu za kuwachonganisha na jeshi la polisi. Lema ajitahidi kwa kiasi kikubwa kukwepa mtego huu.

Unapokuwa umeshinda hata kabla ya kura, adui mwerevu hutafuta njia nyingine nje ya uwanja wa vita kukumaliza, ikiwemo kukutafutia kesi.

Walifikiri Lema angeweza hata kupigana na polisi kwa jazba.....hapo ingekuwa kesi nyingine......watajaribu kuwategea hata 'murder case' ili tu walazimishe ushindi kwa girl friend wao.
 
Polisi wanasema alikuwa anafanya maandamano yeye anasema sio kweli, ukweli ni kwamba alikuwa kwenye gari sasa suala la kuandamana bila kibali linakujaje?
Siasa za maji machafu.
sijui sheria inasemaje maana ni kwamba alikuwa kwenye magari yasiyo puungua 30...lakini kwa maelezo ya Lema inaonekana maandamano nimpaka yanahusishe watembea kwa miguu
 
Sikumbuki kuandika habari za kishabiki anyway tuendelea kubisha kwa hoja...ila kura yako kwa Lema nyingine kwa Dk Slaa

Mkuu,

Ngongo anaweza kumpa Slaa kura yake. lakina kumpa Lema ... du! si rahisi. Sijui mwenzetu Ngongo walicross wapi njia zao na Lema
 
Mkuu,

Ngongo anaweza kumpa Slaa kura yake. lakina kumpa Lema ... du! si rahisi. Sijui mwenzetu Ngongo walicross wapi njia zao na Lema
Nasubiri uchanguzi ukiisha nitamuuliza vizuri kisa cha kuwa na chuki na Lema wakati huo Lema akielekea DODOMA
 
Mkuu,

Ngongo anaweza kumpa Slaa kura yake. lakina kumpa Lema ... du! si rahisi. Sijui mwenzetu Ngongo walicross wapi njia zao na Lema

Heshima kwako Misterdennis,

Mkuu unajua nilipangiwa kwenda Nairobi kikazi kuanzia tarehe 29/10/2010 mpaka 03/11/2010 nikaitolea nje wafanyakazi wenzangu wananishangaa kulikoni nikawaambia lazima nipige kura kwanza wakanicheka sana kwamba kura yako moja haiwezi kuathiri matokeo bwana[NB:unajua mambo ya posho za kusafiri zinavyochangamkiwa na wafanyakazi].
Mkuu sihitaji kuambiwa,kushawishiwa,kurubuniwa kumpigia kura Dr W Slaa,mke wangu,jirani zangu,beki tatu wangu bahati mbaya sina mtoto mwenye umri wa miaka 18 tutajihimu asubuhi na mapema kuwahi kituoni kutimiza wajibu wetu kwa taifa.Wakuu kura yako moja bila kuwashawishi wanaokuzunguka ni kulikosea taifa adabu tafadhali sana timizeni wajibu wenu kwa watoto wenu na Tanzania ya baadaye.

Mkuu Lema hapati kura yangu hilo liko wazi kabisa uhitaji kuwa mtabiri mbabaishaji kama Sheckh Yahaya kubaini hilo, sababu za kutompa kura zipo na nimeshazieleza kwa kina hakuna mwanajamvi hata mmoja aliyeweza kutoa utetezi wenye mashiko.Lema akishinda ubunge bila kura yangu sitajificha kwamba sikumpa kura yangu nitakuwa wazi nitaona fahari kubwa kwamba mimi si mmoja wa watu walioshindwa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi.Watanzania wanoshindwa kufikiri kidogo na kufanya maamuzi sahihi wako wengi sana bahati mbaya Arusha haitakuwa na tofauti na Monduli,Nzega,Bariadi na nk.
 
Nasubiri uchanguzi ukiisha nitamuuliza vizuri kisa cha kuwa na chuki na Lema wakati huo Lema akielekea DODOMA

Heshima kwako Crashwise,

Sababu za kumchukia Lema hazina tofauti na sababu za kumchukia Mramba,Chenge,Lowassa na Rostam Azizz.Tofauti inawekuwa ndogo sana kwamba Lema hajafanya ufisadi wa kulidhuru taifa moja kwa moja akipata nafasi hakika ataitumia vyema wengi wetu mtabaki kushangaa.
 
Back
Top Bottom