Elections 2010 Mgombea ubunge wa CHADEMA Arusha mjini (Lema) akamatwa

Jethro hata akiamia huko hao wameru watamkubali kweli au ndo atakosa bara na pwani:nono:

Jamaaa EL/RA mie hawa jamaaa siwapi shavu kwani ni pesa ndio inawaweka juu wajuwa kama wewe ni mwana mapinduzi siku zote utasimama utasema ile kweli kwa jamii.

Kwani EL ni mtu wakulazimisha kuhusudiwa ni ile hali ya yeye kutaka kujitakasa kwa watanzania kumwonyesha Mwl.Nyerere kuwa alimtabilia vibaya lakini kama ulisha chafua na wananchi hawajataka kukusafisha basi hutosafishika bali wachache ndio watako kuunga mkono

Ishu nzima iko hivi; jana Lema akiwa kwenye kampeni za ubunge kuna landcruiser ilienda ikapaki kwenye eneo la kampeni..

Baada ya muda kuna mama akashuka akaanza kugawa kanga na tshirt, pale vurugu zikaanza na watu wawili kati ya wanne waliokuwa kwenye lile gari wakakimbia..

Wananchi walipomtaiti dereva, dereva akasema ni gari ya usalama wa taifa...na waandishi walisema it is possible sababu haikuwa na stika zozote kwenye kioo..kilichowachanganya ni kuwa namba za gari zilikuwa tofauti na namba za kwenye vioo...

Gari ilipekuliwa na kulikuwa na pesa na tshirt ndani..ishu ikafika polisi...baada ya muda ishu ikageuka na ikasemekana Lema na kundi lake ndio wameishambulia ile gari...leo Lema akiwa anatoka kwenye kampeni jioni hii ndio wakamtait...hivi ndivyo ishu ilivyo...
 
siasa ya sisiemi ndivyo ilivyo inaanzisha ugomvi , alafu inakimbilia polisi, ila godbless lema mungu atakulinda kwani VOX POPULI VOX DEI
 
Ahsante kwa ufafanuzi mkuu!
Ishu nzima iko hivi; jana Lema akiwa kwenye kampeni za ubunge kuna landcruiser ilienda ikapaki kwenye eneo la kampeni..

Baada ya muda kuna mama akashuka akaanza kugawa kanga na tshirt, pale vurugu zikaanza na watu wawili kati ya wanne waliokuwa kwenye lile gari wakakimbia..

Wananchi walipomtaiti dereva, dereva akasema ni gari ya usalama wa taifa...na waandishi walisema it is possible sababu haikuwa na stika zozote kwenye kioo..kilichowachanganya ni kuwa namba za gari zilikuwa tofauti na namba za kwenye vioo...

Gari ilipekuliwa na kulikuwa na pesa na tshirt ndani..ishu ikafika polisi...baada ya muda ishu ikageuka na ikasemekana Lema na kundi lake ndio wameishambulia ile gari...leo Lema akiwa anatoka kwenye kampeni jioni hii ndio wakamtait...hivi ndivyo ishu ilivyo...
 
E bwana ni hivi jamaa alienda kutetea wana-CHADEMA ambao walikuwa wamekamata gari la CCM lenye vitenge na nguo hivi nadhani kule Moshono. Ilikuwa hivi.. CHADEMA walikuwa wanafanya mkutano wao mara wakaja CCM na kuanza kuita watu wapewe kanga za kijani wakimaanisha mashabiki wa CHADEMA.. Kilichotokea Mungu tuu anajua, hayo mawe walioyorusha nusura ya kuua na gari la CCM chapachapa kama mawe yaua basi tena.... CCM wakaenda polisi kushitaki mara ghafla Lema na washabiki wake ndani ya polisi na kuomba lile gari la sisiem lifunguliwe ili watu waone hivyo vifaa vya rushwa visivyohusika lakini mkuu akawa anakataaa... Basi Lema akasema kama vipi akamatwe yeye baadae lakini walimuacha maana jamaa alikomalia gari mpaka likafunguliwa... MAWEEE Mambo yoote yakaharibika... Leo jioni nilikuwa pale stand wakapita magari ya CCM nakwambia wale makondakta wakazomea sana hadi jamaa wa gari la CCM wakawarushia mayai viza.. Alhamdilah nikakambia yaliyojiri sikujua kwa kweli.. Lakini Jimboni hapa Lema atashinda tuu kama 2005 alifika kura 47000 kwa 51000 za mrema basi mwaka huu ni wake watu wanampenda sana kwa kuwa sio muoga ni mjasiri sana.. Ili kukimbizana na CCM yahitajika nguvu ya ziada sio kipolepole ukiwa mkimya wanakudhulumu kabisa....
Sijui nisemaje CHADEMA hoyeee au LEMA hoyeeee????

Mchague DR.SLAA mtoto wa kiume mwenye ujasiri wa kweli haogopi mtu anamuogopa Mungu...
God Bless Tanzania...
 
Tatizo la Lema ni anakitu kama utoto flani hivi,anadhani anaweza kufanya chochote na hatishiki

Hicho unachoita chochote ni nini? mbona mwenzio anatoa rushwa huku akilindwa na Takukuru? au macho yako yanaomwona Lema tu? Unadhani umechangia kitu kwa kutuambia "chochote" bila kutaja kitu?
 
Huo ubabe unasabaibishwa na nini wakati vyombo vya dola vipo? Jiulize, kwa nini waliamua kkuvamia ofisi za TAKUKURU Arusha? Je, kwa nini aliamua kumkamata mgombea wa TLP aliyekuwa akitangaza kwa gari kuwa Wagombea wa vyama vya Upiznani wamejitoa na kumuunga mkono yeye wakati ni uongo? Polisi walikuwa wapi? Walichukua hatua gani wakati Polisi wenyewe wa Doria wapo mitaani, hata wale Trafiki wapo barabarani hata Mlalamikaji aamue kutoka alikokuwa na kuamua kumkamta?

Majibu yako yakupe clue kuwa Dola hapa ARUSHA ina-side na upande fulani au imeamua kumpuuza kitu ambacho ni hatari maana naye Lema ana watu wanoomuunga mkono.

Walivamia ofisi za takakuru kwa kuwa wamekuwa wakipigiwa simu kwenda kuona Chama Cha Mafisadi wakigawa rushwa na hawaendi au wanakwenda masaa mawili baada ya tukio.hapo kuna uwajibikaji gani kwa hao takukuru??? Wanafanya kazi kwa maekekezo ya CCM ndio maana watu wamechoka.
 
Siasa kweli ni siasa tupu.
kama mtu anaelekea kushindwa basi aoneshe upendo kwa watu wake kuwa yupo tayari akajipange upya na sio kuiharibu jamii ambayo anapaswa kurudi kwayo baadae. Batilda kweli binti wa KIHUNI

Mimi nilianza kuwa na mashaka naye tangu alipoteuliwa waziri wa mazingira, halafu kukaja ile ishu ya mgodi iliomwaga sumu kwenye maji yakaathiri wananchi. she dare to talk publicly kwamba yeye hakuwa na taarifa ya uharibufu wa mazingira wala maafa kwa wananchi wanaotumia maji ya mto tigite. Ina maana anatuambia idara za serikali hazifanyi wajibu wake wa kimawasiliano? Alisababisha nianze kumchukia since that day.
Kuna mtu anaweza kutuwekea cv yake humu?
 
Kuna mdau katutumia ujumbe kuwa Godfrey Lema ambaye ni mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Arusha mjini yupo mikononi mwa polisi. Kisa na mkasa tutawafahamisha punde kwani anaendelea kufuatilia chanzo cha kukamatwa kwa bwana Lema

Nimeongea na mgombea Udiwani kata ya Levolosi Chadema sasa hivi. Kilichotokea ni kwamba alikuwa na mkutano katika kata yake na Lema alikuwepo pia, baada ya mkutano waliondoka kwa kuongozana magari mengi walipofika mnara wa mwenge round about wakakutana na OCD wakasimamisha msafara na kuanza kuwapiga watu vibaya, Lema na bwana Nanyaro wakaenda Central police kutafuta PF 3 kwa ajili ya majeruhi ndipo alipoambiwa anatafutwa na kuswekwa rumande kwa muda na saa hizi ndio wanachukua maelezo yake nadhani atatoka muda sio mrefu. Huu utakuwa ni uonevu tu lakini nguvu ya Umma kuizuia itakuwa vigumu. Mungu ibariki nchi yetu.
 
Sishangai kusikia hayo, kwani kama ni kuvunja sheria, CCM wamevunja sheria zote za uchaguzi pamoja na zile za matumizi. Pia kupitia Green Guards wananchi wasio na hatia wamepigwa na kutishwa. Huko vijijini - ambako kuna wapigakura wengi zaidi walio maskini - watu wameamka, sasa baada ya kuona hawaambiliki, vimebakia vitisho. Sishangai Lema kukamatwa, kwani hiyo ni hulka ya MFA MAJI.

Nchi inaendeshwa kidikteta. Nyie mlikuwa mnadhani kuna demokrasia. Mmeotea! Sio goli hilo!

CCM haitakubali kuiachia nchi hii KWA HIARI. Natarajia machafuko makubwa baada ya uchaguzi, kwani kuna WAPUMBAVU wengi ambao wanadhani kwamba nchi hii ni mali yao. Ni mali ya Watanzania.

JK alipohutubia nchi Okt. 14, kule Kigoma, alizungumzia wanasiasa kuwashawishi Watanzania kufanya vurugu. Hakuwataja wanasiasa hao, lakini wanaowashawishi Watanzania kufanya vurugu, kupiga watu wasio na hatia, kuwaumiza kwa mapanga, kuwakamata kwa makosa bandia, NI NANI ZAIDI kama sio CCM?

Mtakuja kuhukumiwa na historia. Mmesahau yaliyotokea Kenya? Kwa hiyo mko radhi damu imwagike ili mrudi Ikulu?

MIE SIMO!
 
Nimeongea na mgombea Udiwani kata ya Levolosi Chadema sasa hivi. Kilichotokea ni kwamba alikuwa na mkutano katika kata yake na Lema alikuwepo pia, baada ya mkutano waliondoka kwa kuongozana magari mengi walipofika mnara wa mwenge round about wakakutana na OCD wakasimamisha msafara na kuanza kuwapiga watu vibaya, Lema na bwana Nanyaro wakaenda Central police kutafuta PF 3 kwa ajili ya majeruhi ndipo alipoambiwa anatafutwa na kuswekwa rumande kwa muda na saa hizi ndio wanachukua maelezo yake nadhani atatoka muda sio mrefu. Huu utakuwa ni uonevu tu lakini nguvu ya Umma kuizuia itakuwa vigumu. Mungu ibariki nchi yetu.
That is the true version ya kilichotokea. Hata mimi nilikuwepo hapo Police Central usiku huu. Bado yupo ndani hawajamtoa. Vijana wa CHADEMA walianza kukusanyika hapo Central, Polisi (in riot gear) wakawafukuza around saa 4 usiku hivi.
 
Ishu nzima iko hivi; jana Lema akiwa kwenye kampeni za ubunge kuna landcruiser ilienda ikapaki kwenye eneo la kampeni..

Baada ya muda kuna mama akashuka akaanza kugawa kanga na tshirt, pale vurugu zikaanza na watu wawili kati ya wanne waliokuwa kwenye lile gari wakakimbia..

Wananchi walipomtaiti dereva, dereva akasema ni gari ya usalama wa taifa...na waandishi walisema it is possible sababu haikuwa na stika zozote kwenye kioo..kilichowachanganya ni kuwa namba za gari zilikuwa tofauti na namba za kwenye vioo...

Gari ilipekuliwa na kulikuwa na pesa na tshirt ndani..ishu ikafika polisi...baada ya muda ishu ikageuka na ikasemekana Lema na kundi lake ndio wameishambulia ile gari...leo Lema akiwa anatoka kwenye kampeni jioni hii ndio wakamtait...hivi ndivyo ishu ilivyo...

Asante kwa taarifa.
Siasa za Tanzania ni wizi mtupu maana kanga na T-shirt ndo zimekuwa ngao za kuwanasa wananchi wanaopenda vitu vya bure.
Sidhani kama usalama wa taifa wanajukumu la kusambaza hizo bidhaa.
 
Atakuwa amevikosea adabu tu kwa vyombo vya sheria...
Kibs... hivi anko wako akizidi kukutusi, kukuchokoa na kukudharau nyumbani kwako utamuangalia tu??.... eniwei sisemi sana lakini nijuavyo mimi ni kwamba Lema ni style ya Mbowe, they can not hold back once excited, he needs to get super back up otherwise kesi itaisha in 5 days na yeye atafungwa; Lowassa ana nguvu sana and Lema should have known better
 
Atakuwa amevikosea adabu tu kwa vyombo vya sheria...

hapana, ni kwa sababu amemkali koo demu yule kisiasa, sasa washikaji wa demu huyo wameamua kumjia Lema wazimwazima ili demu aingie mjengoni kwa namna yoyote ile.
 
Ilivyokuwa: Lema alikuwa anatoka kwenye mkutano wa kampeni ambao ulifanyika Levorosi na kufungwa saa 12:4 jioni basi wakati Lema anaondoka wapenzi wa CHADEMA wakaungana msafara wakimsindikiza huku wakiwa na mzuka wa ajabu yaani ni honi na miluzi ndiyo ilikuwa imeshamili inakadiliwa magari zaidi ya 30 hivyo ikawa kama kwamba anafanya maandamano na kusababisha jam kama unavyo ujua mji wa arusha walipo fika idara ya maji karibu na Posta Meru polisi walianza kuwa sihi wasitishe hayo maandamano kama walivyo yatafasili, hawakutii amri hiyo wakidai hayo siyo maandamano bali ni msafara wa kumsindikiza mbunge wao nyumbani na walioji kwani msafara mwisho gari gapi? walipo fika mnara wa mwenge ndiyo polisi walipoongezeka nakublock nakuanza kuamrisha baadhi ya magari yaelekee Kaloleni magine centre imradi wawasambaratishe kuna baadhi walikadi amri ya polisi ndipo polisi wakaanza kuwa telemsha kwenye magari yao nakuwapiga kuna jamaa aliumia sana hivyo lema aliamua kwenda polisi kuchukua PF3 ili jamaa akatibiwe alipofika pale reception (Polisi) alimkuta kamanda Basilio alimwambia anamtafuta ndipo alipomwambia "ningilia kwa wapi nipite juu ya meza au nizunguke" akamwambia zunguka Lema akazunguka, alipofika aliopo kamanda Basilio alimwambia nimekuja kwajaziba, Basilio akamwambia "nitakupiga" Lema akamwambia unataka unipige makofi au risasi kama ni risasi piga hapa akimwonyesha sehemu ya kupiga huku akivua shirt na kushika kwenye moyo akiimanisha ndiyo sehemu sahihi ya kupigwa kwa risasi ndipo Basilio nadhani kwa kuona anadhalilishwa maana hayo yote yalitokea mbele ya polisi na wananchi akaamrisha Lema awekwe ndani walimtaka aandike maelezo kabla hajaingia ndani Lema aligoma akitaka wakili wake (Amani) awepo ilibidi awekwe ndani huku wakimsubilia wakili, watu walijazana Polisi wakitaka kujua nini kimetokea kwa mbunge wao wakafukuzwa walitawaywa kwa virungu lakini ilipotimu saa 4:30 watuwalikuwa wamejaa tena wakitaka kujua kama Mbuge wao atatoka au laah, polisi walikuja na kuwaambia wakae mita 200 kutoka kituo cha polisi watu wakagoma kukatokea purukushani safari hii polisi walishinda tena kwani watu walipanda kwenye magari yao na kuondoka mahali hapo na kuja kusiama maeneo ya Arusha City park….
Bw Godbless Lema alitolewa usiku huo huo
 
Ilivyokuwa: Lema alikuwa anatoka kwenye mkutano wa kampeni ambao ulifanyika Levorosi na kufungwa saa 12:4 jioni basi wakati Lema anaondoka wapenzi wa CHADEMA wakaungana msafara wakimsindikiza huku wakiwa na mzuka wa ajabu yaani ni honi na miluzi ndiyo ilikuwa imeshamili inakadiliwa magari zaidi ya 30 hivyo ikawa kama kwamba anafanya maandamano na kusababisha jam kama unavyo ujua mji wa arusha walipo fika idara ya maji karibu na Posta Meru polisi walianza kuwa sihi wasitishe hayo maandamano kama walivyo yatafasili, hawakutii amri hiyo wakidai hayo siyo maandamano bali ni msafara wa kumsindikiza mbunge wao nyumbani na walioji kwani msafara mwisho gari gapi? walipo fika mnara wa mwenge ndiyo polisi walipoongezeka nakublock nakuanza kuamrisha baadhi ya magari yaelekee Kaloleni magine centre imradi wawasambaratishe kuna baadhi walikadi amri ya polisi ndipo polisi wakaanza kuwa telemsha kwenye magari yao nakuwapiga kuna jamaa aliumia sana hivyo lema aliamua kwenda polisi kuchukua PF3 ili jamaa akatibiwe alipofika pale reception (Polisi) alimkuta kamanda Basilio alimwambia anamtafuta ndipo alipomwambia “ningilia kwa wapi nipite juu ya meza au nizunguke” akamwambia zunguka Lema akazunguka, alipofika aliopo kamanda Basilio alimwambia nimekuja kwajaziba, Basilio akamwambia "nitakupiga" Lema akamwambia unataka unipige makofi au risasi kama ni risasi piga hapa akimwonyesha sehemu ya kupiga huku akivua shirt na kushika kwenye moyo akiimanisha ndiyo sehemu sahihi ya kupigwa kwa risasi ndipo Basilio nadhani kwa kuona anadhalilishwa maana hayo yote yalitokea mbele ya polisi na wananchi akaamrisha Lema awekwe ndani walimtaka aandike maelezo kabla hajaingia ndani Lema aligoma akitaka wakili wake (Amani) awepo ilibidi awekwe ndani huku wakimsubilia wakili, watu walijazana Polisi wakitaka kujua nini kimetokea kwa mbunge wao wakafukuzwa walitawaywa kwa virungu lakini ilipotimu saa 4:30 watuwalikuwa wamejaa tena wakitaka kujua kama Mbuge wao atatoka au laah, polisi walikuja na kuwaambia wakae mita 200 kutoka kituo cha polisi watu wakagoma kukatokea purukushani safari hii polisi walishinda tena kwani watu walipanda kwenye magari yao na kuondoka mahali hapo na kuja kusiama maeneo ya Arusha City park….
Bw Godbless Lema alitolewa usiku huo huo
 
Naam hivyo ndivyo ilivyo. Bado tunaona mtumizi mabaya ya dhamana waliyopewa watu. Kama asingeenda Basilio alikuwa ampate wapi? Mtu yupo kila saa anahutubia kila siku kiongozi mkubwa kama huyo unatoa kauli NILIKUWA NAKUTAFUTA! Hivi hawafundishwagi namna ya kuuliza! Aibu sana. Kama ni treni ya mkaa ndo imeshika kasi sasa mpaka kituo cha piliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Bye bye Batilda
 
afadhali nilikosa nafasi ya kwenda upolisi enzi zile...nisingeweza kuvumilia ujinga kama huu
 
Back
Top Bottom