Elections 2010 Mgombea Ubunge wa Chadema Arusha mjini afunguliwa Mashtaka kwa kutishia kuua

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Source: Habari TBC1
Mgombea ubungwe kwa tiketi ya Chadema amefikishwa kwa tuhuma za kutishia kuua. Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ndio amefungua kesi hiyo akimtuhumu Lema kumtishia kumuua endapo atashindwa((Lema) kwenye uchaguzi.

Hivi kweli haki itatendeka jimbo hili?
Jamani haya mambo yanatoka wapi tena, Batilda ameanza hujuma, badala ya yeye kukamatwa kwa rushwa, amzushia zengwe Lema.
 
Hivi kweli haki itatendeka jimbo hili?
Jamani haya mambo yanatoka wapi tena, Batilda ameanza hujuma, badala ya yeye kukamatwa kwa rushwa, amzushia zengwe Lema.

Usijali sana kwani sasa hivi CCM kubaki madarakani kunategemea nguvu ya dola lakini kama tulivyojifunza duniani kote nguvu ya dola haifui dafu kwa nguvu ya wananchi.

Baada ya kumwondoa Mbuya hapo Arusha na kuweka kibaraka wao ambaye wanaweza kumtumia watakavyo sasa wanalazimisha ushindi kwa Dr. Batilda ambaye hakubaliki hata kidogo.
 
ndo mazingira ya uchakachuaji yanaandaliwa hivyo chichi m walishasema kuwa watatumia mbinu za kijeshi ths election.go lema go.
 
Source: Habari TBC1
Mgombea ubungwe kwa tiketi ya Chadema amefikishwa kwa tuhuma za kutishia kuua. Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ndio amefungua kesi hiyo akimtuhumu Lema kumtishia kumuua endapo atashindwa((Lema) kwenye uchaguzi.

Hivi kweli haki itatendeka jimbo hili?
Jamani haya mambo yanatoka wapi tena, Batilda ameanza hujuma, badala ya yeye kukamatwa kwa rushwa, amzushia zengwe Lema.

Ndoto ya Lowasa kutaka kuwa rais bado anayo.

Lowasa tulia. Endelea kula laana ya Baba wa Taifa. Umeshiriki kuhujumu nchi. Hautapona
 
Kuna historia ya watu waliowahi kuchaguliwa in their absence na wakashinda. Lema atachaguliwa na wana Arusha hata akiwa kifungoni. Atarudi na kuwa mbunge wa Arusha baada ya kifungo maana haki inawezekana isitendeke ili tu wafanikiwe malengo yao.
 
wameanza . Akitunyima Mbunge kwa hila ajiandae kwa matokeo yake soon. Hatuogopi vibaraka asilani.
 
jamani ccm tuachieni mbunge wetu. Batilda hatukutaki jamani mbona unakuwa mgumu kuelewa? Go lema. Go chadema. 2010 hatudanganyiki!!!!!
nguvu ya umma itaamua.
 
Source: Habari TBC1
Mgombea ubungwe kwa tiketi ya Chadema amefikishwa kwa tuhuma za kutishia kuua. Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ndio amefungua kesi hiyo akimtuhumu Lema kumtishia kumuua endapo atashindwa((Lema) kwenye uchaguzi.

Hivi kweli haki itatendeka jimbo hili?
Jamani haya mambo yanatoka wapi tena, Batilda ameanza hujuma, badala ya yeye kukamatwa kwa rushwa, amzushia zengwe Lema.

Hivi unamjua Lema kweli hadi ukafikia conclusion kuwa hakufanya hilo na ni njama za mpizani wake??? Yaleyale ya wanaCCM waliokuwa wakikamatwa na takukuru halafu utetezi wao pekee ni kuwa ni njama za wapinzani wao???
 
We know the prime mover behind all this si mwingine ni yule mjamaa mwenye uchu mkubwa wa madaraka na fisadi No 2 in the country -- EL.

Ni kesi ya pili inside two years inayohusu kutishia kuua katika mkoa wa Arusha. Ya kwanza ilikuwa ile ya Mallya against Ole Sendeka na haki ikaptikana, Mallya na huyo EL wake wakaaibika ile mbaya.
 
Ndiyo mkakati wa CCM huo! wakiona wanashindwa wanaanza kubambikia watu kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu. Kwanza walimbambikia Dr Slaa kesi ya kuchukua mke wa mtu sasa hii ya kutishia kuua sijui itakayofuata itahusu nini. Wanatapatapa hawa maji yamewafika kushingo na Watanzania hawatarudia makosa ya miaka ya nyuma bali kuwaondoa madarakani kwa kishindo.
 
Nilijua tu kwa hali niloiona pale Arusha ningeshangaa kama wasingembambikizia kesi!
 
MODS; Mimi nadhani hii habari siyo kweli. Nimesoma leo magazeti ya T Daima, Mwananchi na Nipashe ambayo nina hakika habari hiyo isingeachwa lkuchapishwa akini hamna. Sijui magazeti mengine.
 
Hahaha
Hahaha
Ingawa inaonekana wanatumia mbinu dhaifu lakini ina sudi mbaya sana.
Dawa ni kuweka wakili makini na sisi tukapige kura kuwaondoa mabaniani hapo 31 oktoba
 
MODS; Mimi nadhani hii habari siyo kweli. Nimesoma leo magazeti ya T Daima, Mwananchi na Nipashe ambayo nina hakika habari hiyo isingeachwa lkuchapishwa akini hamna. Sijui magazeti mengine.
Haa haa haa! Yaani wewe unafanya judgement ya ukweli wa habari ya humu kwa kuangalia baadhi ya magazeti? Mbona wakati mwingine magazeti yanachukua habari humu? Ingekuwa vizuri umkomalie mleta habari athibitishe, si kama unavyotaka kufanya reference kwenye media nyingine.
 
Back
Top Bottom