Mgombea ubunge wa chadema afukuzwa kazi serikalini

Lkn si waliambiwa kabla ya uchaguzi kua sheria ya utumishi haiwaruhusu kugombea na wakigombea watafukuzwa kazi? Sijaona kosa mie hapo.

Meya wa Kinondoni-Dar ambaye ni diwani kupitia chama cha CCM bado ni mtumishi tena afisa wa ngazi za kati wa TRA
 
Sina hakika na sheria za bara, ila kule visiwani Diwani anatakiwa awe na shughuli binafsi (Sio ajira katika serikali/kampuni) kwa wakati wote wa Udiwani wake. Aidha kama alikuwa ameajiriwa anapaswa kuacha kazi yake. Iwapo hakuweza kuupata udiwani ana uwezo wa kurudishwa tena kazini kwake.

Kama unazungumzia Kisiwa cha ZNZ ningependa kuuliza swali hili kwa kibunango;

ZNZ wana wanachagua madiwani au Masheha au wote wawili?
 
Ofisini kwangu kuna watu 4 walienda kugombea kwa hicho chama chao na walishindwa woote kabisa wamerudi kazini wanakula per diem kama hawana akili nzuri! usikate tamaa mura ryoba baada ya MSRI ni zamu yetu kulianzisha baadae serikali mpya itakuajiri kwa ths laki 9 kwa mwezi.
 
sheria ya utumishi iko wazi wala haijafishwa, mtumishi wa umma anaweza kuwa mwanachama cha chama cha siasa lakini hatakiwi kugombea uongozi au kufanya kampeni za kisiasa lakini kwa upande wa vyombo vya dola hawatakiwi kabisa kuwa wanachama wa chama cha siasa isipokuwa kupiga kura tu.

kama kuna wanaCCM walikiuka sheria hii na bado wanafanya kazi, tupeane taarifa ili tutoe ushauri ili waondolewe kazini mara moja.

Acha uongo hamna sheria kama hiyo; wanachukua likizo kwa ajili ya uchaguzi akishindwa anarudi kazini, akishinda anaamua moja kuendelea na siasa au la! akiamua kiendelea na siasa utumishi unaishia hapo hapo na lazima ku-diclare, kuhusu vyombo vya dola sheria hinakataka kushabikia vyama vyama vya siasa sio kuwa mwanachama wa chama cha siasa kama huna chama utapiga vipi kura!!! kumbuka viongozi kibao wa hivyo vyombo ni makada wa CCM hapa hoja ya msingi ni kwanini wakiwa upinzani hawapewi hazi zao lakini wakiwa ccm wanapewa zaidi ya haki??! kama huyo Peter kwavile alikuwa pandikizi la ccm hakudhulika!!! huko ni kufinya maendeleo ya upinzani.
 
Ukifikiria mengi kuhusu hii serikali ya kikwete unaweza kufariki siku si zako.me namshauri awasiliane na Tundu Lisu kwa ushauri ama msaada wa kisheria
 
Aende ktk chama cha wafanyakazi (waalimu) kitamsaidia.
Au atafute mwanasheria amfungulie kesi ya madai mwajiri wake.
 
Sina hakika na sheria za bara, ila kule visiwani Diwani anatakiwa awe na shughuli binafsi (Sio ajira katika serikali/kampuni) kwa wakati wote wa Udiwani wake. Aidha kama alikuwa ameajiriwa anapaswa kuacha kazi yake. Iwapo hakuweza kuupata udiwani ana uwezo wa kurudishwa tena kazini kwake.

Nadhani siasa za bara zinafikia pabaya. Kwa bara hali ni ngumu. Zenj wako mbele yetu maana siyo ajabu kwa mtu kuwa CUF au CCM.

Bara wafanyabiashara woote lazima waonyeshe utiifu kwa CCM, bila hivyo wanakuwa kwenye mapambano na TRA. Kwa watumishi wa serikali pia ni tatizo kubwa. wakionyesha u-CUF wao au u-CDM, basi nafasi imepotea.
 
sheria ya utumishi iko wazi wala haijafishwa, mtumishi wa umma anaweza kuwa mwanachama cha chama cha siasa lakini hatakiwi kugombea uongozi au kufanya kampeni za kisiasa lakini kwa upande wa vyombo vya dola hawatakiwi kabisa kuwa wanachama wa chama cha siasa isipokuwa kupiga kura tu.

kama kuna wanaCCM walikiuka sheria hii na bado wanafanya kazi, tupeane taarifa ili tutoe ushauri ili waondolewe kazini mara moja.

Hapana siyo kweli kwamba sheria ya utumishi wa umma haimruhusu mtumishi kugombea Ubunge, hebu tafuteni kitu kinaitwa "Civil servants code of conduct" Kwa mlioko Dar nafikiri itakuwa rahisi kwenu kukipata kuna maktaba moja kubwa pale karibu na IFM kama sijakosea, sipakumbuki vizuri ila ni kama .....................Development Learning Centre. Kuna kipengele kinachoruhusu kwa mtumishi wa daraja fulani kuomba likizo isiyokuwa na malipo kwa kipindi chote cha tangu kuingia kwenye mchakato wa kujaza fomu hadi siku ya uchaguzi. Isipokuwa kwa nafasi ya daraja la kuanzia Mkurugenzi wa Wilaya na kuendelea hao hawaruhusiwi kabisa labda waombe kuacha kazi!

Kwa hiyo kwa huyo mwalimu kama kweli alifuata taratibu zote za kuomba likizo isiyokuwa na malipo kwa mwajiri wake na akaruhusiwa atafute msaada wa kisheria naamini kesi yake atashinda na fedha yake atalipwa, hivyo hao jamaa wanamtunzia fedha yake. Lakini kama aliondoka kinyemela, imekula kwake labda akajiunge na shule za binafsi maana yuko kwenye nafasi za watu wanaotafutwa sana!!
 
Aende ktk chama cha wafanyakazi (waalimu) kitamsaidia.
Au atafute mwanasheria amfungulie kesi ya madai mwajiri wake.

Hawezi kufanikiwa. Nchi hii si unawaona majaji wanavyokwenda kinyume kila wakati. Tuna majaji wa kuokota mtaani kwa faida zetu kisiasa.

Wote wana bei zao. kuna wale ambao ukiwapa madaraka wanaamua watakavyo. wengine ukiwa na kesi wape milioni 5, 10 na hata 50 kama mambo ni magumu sana.

Walimu walipotangaza mgomo si ulisikia kesi ikiamuliwa j'pili!
 
hawa ccm wanajulikana kwa visasi na ubabe hasa kwa wanyonge ila wakiwaachia huru hao mafisadi papa wakipeta tu barabarani
 
Wadau,
Kama mnavyofahamu kuna baadhi ya watumishi wa serikali walioamua kutumia haki yao ya kidemokrasia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi yetu kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.Wapo waliogombea kupitia ccm na wengine vyama vya upinzani.

Miongoni mwa wengi waliogombea kupitia vyama vya upinzani ni mwalimu Marwa Ryoba(Mwalimu wa shule ya sekondari Tarime) anayefundisha masomo ya sayansi (fizikia na kemia). Huyu bwana 'inasemekana" amefukuzwa kazi mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kwakuwa aligombea kupitia chama cha upinzani.

Binafsi nimeongea naye, ameniambia serikali imesitisha mshahara wake tangu mwezi novemba mwaka jana, pamoja na kwamba alirejea kazini kwake mara tu baada ya uchaguzi.Pamoja na juhudi alizofanya kutaka kujua sababu ya kusitishwa mshahara wake, hajapewa majibu ya kueleweka na wala hajapewa barua rasmi kumjulisha kama amefukuzwa kazi, ama kasimamishwa kazi ama kuna tatizo gani lililosababisha kufikiwa kwa uamuzi huo.

Kwakuwa hili jambo linaweza kuwa limewatokea watumishi wa umma wengi, kama ilivyomtokea Pro.Baregu mwaka juzi, nadhani kuna sababu za msingi hili jambo likawekwa wazi, kama ni muongozo wa utumishi wa umma uwekwe wazi ili kila mtu ajue.Ni jambo la ajabu kwamba mtumishi wa umma akiwania nafasi ya kisiasa kupitia ccm inakuwa halali lakini akifanya hivyo kupitia vyama vya upinzani inakuwa haramu.

Hii tabia ya serikali kuleta ubaguzi miongoni mwa watanzania inabidi tuipinge kwa nguvu zote. Ili kila mwananchi awe na uhuru wa kweli wa kushiriki zoezi la demokrasia pasipo na kificho wala wasiwasi.

Nawasilisha.

Hawa watumishi wa serikali wenye akili za kiCCM wajinga sana na wapumbavu hao hao kesho utasikia tunauhaba wa walimu wa masomo ya sayansi alafu mwalimu mzuri kama huyo wanamnyima nafasi, bora atafute private akale mshahara wa nguvu
 
Back
Top Bottom