Mgombea ubunge wa chadema afukuzwa kazi serikalini

naomba kueleweshwa kidogo hivi mkuu wa mkoa sio mfanyakazi wa serikali? maana nimeona mkuu wa mkoa hapo hapo mwanasiasa.
 
Namshauri huyo mwalimu apeleke suala lake katika vyombo vya sheria akianzia kwenye chama cha wafanyakazi. Nawahakikishieni kama tapitia chama cha waalimu au TUGHE kesi hiyo atashinda na akishinda na serikali ikakaidi kumlipa haki zake, kesi inaendelea hadi kufikia mahali pa kumshtaki kiongozi binafsi kwa kukataa kulipa - rejea kesi ya tazara ambapo ilifika mahali meneja akashtakiwa kibinafsi.
Mwalimu, kwa wakati huu utakapokuwa unapambana na serikali huwezi kufa njaa, zipo shule nyingi zinakuhitaji (tena fizikia na kemia!).
Pole sana, hiyo ndiyo gharama ya dOMOcrasia ya Tanzania, lakini TUTASHINDA.

Ahsante kiongozi kwa ushauri wako,
Nitaufikisha kwa mhusika.
 
Nasikitika sana ila mwambie anitafute nimpe kazi na mshahara mzuri. Achana na serikali inayofilisika ya Kikwete. Kama anafundisha vizuri na nyanga ni nzuri basi anione

Yego Masika, poti unasema kweli ama unaleta utani?
Kama uko serious nimwambie akutafute.
 
sheria ya utumishi iko wazi wala haijafishwa, mtumishi wa umma anaweza kuwa mwanachama cha chama cha siasa lakini hatakiwi kugombea uongozi au kufanya kampeni za kisiasa lakini kwa upande wa vyombo vya dola hawatakiwi kabisa kuwa wanachama wa chama cha siasa isipokuwa kupiga kura tu.

kama kuna wanaCCM walikiuka sheria hii na bado wanafanya kazi, tupeane taarifa ili tutoe ushauri ili waondolewe kazini mara moja.

Mkuu kama usemayo ni kweli, hebu nipe ufafanuzi kidogo;

Mara kadhaa iwe ni uchaguzi mkuu ama uchaguzi mdogo watumishi mbalimbali wa umma wamekuwa wakijitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi na baada ya uchaguzi wanaoshindwa hurudi kwenye majukumu yao. Sijawahi kushuhudia kada wa ccm ameshiriki kuwania nafasi ya uongozi na baada ya uchaguzi akarudi kwenye eneo lake la kazi akasimamishwa ama kufukuzwa, labda kama unawafahamu unaweza kunifahamisha.

Sasa kama hizo sheria zipo, zinawabana wanaoshiriki uchaguzi kupitia vyama vya upoinzani tu na wan ccm haziwabani?
 
Inawezekana haya yakawa ni maagizo ya wanasiasa. Mpaka hapo wanasiasa watakapotambua kwamba Mwalimu ni asset muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu tutakuwa tumetatua tatizo la wanafunzi kufanya vibaya.
Inashangaza kuona serikali badala ya kufurahi mwalimu tena wa Fizikia na Kemia (Gonjwa sugu linalohitaji tiba) anarudi kazini tena kwa hiari yake anaundiwa zengwe kwa kisingizio cha siasa na utashi wa wanasiasa uchwara.
Mimi namshauri Mwl. Ryoba adai haki yake kwa kufuata taratibu za ajira, na wakati huo huo atafute temp. kwenye private schools, am sure haitakuwa shida kwake kutokana na aina ya masomo anayofundisha.
 
Nadhani ku-uphold hiyo sheria tata ya utumishi wa umma vs siasa hakuwezekani kuwa kwa haki katika mazingira ya leo. Bila shaka ilitungwa kwa nia ya kuumiza watu fulani katika tafsiri na utekelezaji wake.

Katiba Mpya Tz ndio suluhisho wa matatizo ya aina hii.
 
DIWANI WA NJIRO ARUSHA KUPITIA CCM NI MWAJIRIWA WA TRA MIAKA MINGI! NA HUU NI MHULA WAKE WA PILI.
AU UKIWA MPINZANI SIO RAIA WA TANZANIA?:sad:
 
lkn si waliambiwa kabla ya uchaguzi kua sheria ya utumishi haiwaruhusu kugombea na wakigombea watafukuzwa kazi? Sijaona kosa mie hapo.

Ikiwa wana ccm wanagombea na hawafukuzwi kazi basi ni wajibu wetu kuilazimisha serikali ifate sheria na si kuendelea na sisi kuvunja sheria. Na hapa ndio napata shaka ya hoja ya chadema kweli inaweza kusimamia uadilifu.
kama unamfukuza kazi mtumishi zipo taratibu za kufuatwa sasa kuzuia mshahara maana yake nini kama sio udictator????
Hakuna chochote alichoambiwa unazuia mshahra wa mtu-huu ni udhalimu wa hali ya juu-unatakiwa kukemewa, kama sheria ifuatwe apewe barua kwa wakati sio mateso aliyonayo.
 
Ulimuuliza kama alitoa taarifa kwa mwajili wake kama hatokuwepo katika kituo cha kazi wakati wa uchaguzi? Ama aliomba likizo ili aingie kwenye siasa? Kisha kurudi baada ya uchaguzi? Na kama alichukua likizo ni aina gani ya likizo aliyochukua?

Bwana shem hata wewe?
 
kama unamfukuza kazi mtumishi zipo taratibu za kufuatwa sasa kuzuia mshahara maana yake nini kama sio udictator????
Hakuna chochote alichoambiwa unazuia mshahra wa mtu-huu ni udhalimu wa hali ya juu-unatakiwa kukemewa, kama sheria ifuatwe apewe barua kwa wakati sio mateso aliyonayo.

Hilo ndo jambo la kushangaza kwamba badala ya kumpa barua ya kumuachisha kazi wameamua kuzuia mshahara wake.
 
Unasema kugombea Uongozi! Ni ngazi ipi hiyo?

Pale Morogoro kuna mtu alilalamika kuhusu mtu mmoja aitwaye Profesa Ishengoma, aliyekuwa diwani na baadaye kuchaguliwa Meya. mtu huyu aliendelea kulamba mshahara wa u-meya na bado SUA aliendelea kula mshahara.

Wakati hayo yakiendelea, Profesa Balegu akapigwa stop! Nasikia tena kwamba hapo hapo SUA sasa hivi kuna madiwani wawili na bado ni watumishi waandamizi wako ofisini kama kawaida.

Hebu tuelelweshe ni ngazi ipi ya uongozi.
Sina hakika na sheria za bara, ila kule visiwani Diwani anatakiwa awe na shughuli binafsi (Sio ajira katika serikali/kampuni) kwa wakati wote wa Udiwani wake. Aidha kama alikuwa ameajiriwa anapaswa kuacha kazi yake. Iwapo hakuweza kuupata udiwani ana uwezo wa kurudishwa tena kazini kwake.
 
Mkuu kama usemayo ni kweli, hebu nipe ufafanuzi kidogo;

Mara kadhaa iwe ni uchaguzi mkuu ama uchaguzi mdogo watumishi mbalimbali wa umma wamekuwa wakijitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi na baada ya uchaguzi wanaoshindwa hurudi kwenye majukumu yao. Sijawahi kushuhudia kada wa ccm ameshiriki kuwania nafasi ya uongozi na baada ya uchaguzi akarudi kwenye eneo lake la kazi akasimamishwa ama kufukuzwa, labda kama unawafahamu unaweza kunifahamisha.

Sasa kama hizo sheria zipo, zinawabana wanaoshiriki uchaguzi kupitia vyama vya upoinzani tu na wan ccm haziwabani?

Ndg yangu ajira yako inakuwa valid wakati wa mchakato wa kuteuliwa ndania ya chama chako cha kisiasa kuwa mgombea wa nafasi kwenye uchaguzi mkuu. Ukifanikiwa kuteuliwa, ajira yako immediately inaota nyasi. Ndivyo nilivyoambiwa. Sasa sijui ni kweli? Wanasheria watujuze.
 
kwa usanii uu hatuitaji mnajimu. Mbona walimu wa ifm wamegombea na bado wanafundisha?
 
Jamani mbona mimi ni mwalimu na ni mwanachama wa CDM nina mpango wa kugombea ubunge miaka ijayo itakuwaje

USHAURI WADAU
 
kule chuo cha ualimu korogwe kuna mwl anaitwa muhidini msangi alikuwa diwani wa ccm huko hai lakini bado alikuwa kazini kama kawaida katika uchaguzi wa 2005-2010
 
Back
Top Bottom