Mgombea ubunge ubungo wa CCM apandisha katika mdahalo urafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea ubunge ubungo wa CCM apandisha katika mdahalo urafiki

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jatropha, Aug 28, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Bibi Hawa Ng'ambi, usiku huu alishindwa kujizuia na kupandisha hasira kiasi cha mara kwa mara kumzonga mwendeshaji wa kipindi cha mchakato majimboni kilichokuwa kikiendeshwa na kurushwa na TBC baada ya kuulizwa swali aelezee ushiriki wake katika uuzwaji wa nyumba ya Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) Kinondoni ambapo yeye alikuwa kiongozi wa ngazi ya wilaya.

  Alimzonga mwendeshaji wa kipindi akitaka kupatiwa upendeleo wa kujieleza na zaidi. Ilibidi wahudhuriaji waanze kumzomea kwa jinsi alivyokuwa akionyesha kutaka kumruhusu Mama huayo kugeuka ndiye mwendeshaji wa kipindi; ndipo mwendeshaji akapata ujasiri wa kuendelea kusimamia kipindi kama alivyokuwa akifanya kutoka mwanzo.

  Yaani CCM imetapakaa mafisadi wakubwa na wadogo. Kwa jinsi alivyoonyesha kupandisha na kutishia kwenda mahakamani ni wzi kuwa alihusika na kashafa hiyo.

  Jibu la aliyeuliza swali hilo nalo lilikuwa bomba "Mahakama zimetengenezewa watu na sio wanyama".

  Mwenye habari kamili atahabarishe
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi ni afadhali nikalewe taska kuliko kumsikiliza huyu mama
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  Aug 29, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kama wagombea wengi wa CCM, hana tofauti na wenzake.

  Usitarajie kunywa mvinyo kwa mtu anayeandaa mkojo. Mkojo ni mkojo, mvinyo ni mvinyo. Hata ukiuchanganya na mvinyo, mkojo ni mkojo tu!
   
 4. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  aisee ni hatari yaani mwanzoni na mbwembwe nyingi kedekede nilidhani bonge la kiongozi na digrii kibao kedekede....nikashangaa anashindwa kaswali kakijinga mno yaani angejibu tu "si kweli" ilikuwa tosha matokeo yake amekuwa kituko mpaka kuzomewa .........pole mama <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mhh..hebu mwageni mbigiri zaidi wadau..
   
 6. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Ile attitude aliyoonyesha ndio ya mtu mwenye shshada 2 za uchumi na 2 sijui za kitu gani. Shahda za ngono hizo!!!!!!!!!!!!!!. Mara mia mgombea mwenza wetu angeweza kuonyesha hekima, busara na ueledi wa uongozi.

  Namkumbuka siku moja nilikuwa pale Wizara ya Kilimo ya zamani Pamba House basi mama huyu na mwenzake walijisimamisha karibu na gari la Mhe Sumaye wakati huo akiwa naibu au Waziri wa Waziri wa Kilimo kwa masaa na alipotoka kuingia kwenye gari wakajigonga kisawa sawa KiOHIO OHIO
  . Kila mtu aliyekuwa pale aliwashangaa sana na ukware wao.

  Kibamba ndio wameshapata hasara mgombea ubunge ndio kama hivyo. Nasikia hata mgombea udiwani wa CCM aliyepita ni aina ya kiOhio Ohio kwa kwenda mbele!!!!!!! Kazi kwenu mkiwapitisha hao machangu:mad2::mad2::mad2:
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Duh,hizi mbigiri sasa zina sumu..
   
 8. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #8
  Aug 29, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Wenye data mwageni upupu na mbigiri, hata kama zikiwawasha SHAURI YAO!
   
 9. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  anatuharibia kauli mbiu yetu ya "wanawake tukiwezeshwa tunaweza" jazba zimezidi sana bana! agrrrrrrh!
   
 10. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  umeona eh! kazi ipo
   
 11. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  ni hivi, yule mama lazima kuna mkubwa 'anakaa', haikua rahisi kumshinda Nape/Mwangunga katika mchakato....jana kachemshwa ipasavyo,na penye uongo ukweli hujulikana, first round tayari tumeshajua kwamba ni bogus...utaratibu huu wa CCM wa "women empowerement" ni mbaya sana,wanawake wengi wanadhalilishwa sana pamoja naelimu zao.....
   
 12. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Lady N ni kweli kwamba alihusika katika uuzwaji wa nyumba hiyo na kufilisi miradi kibao ya UWT Kinondoni. Sasa atawezaje kuwakomboa akina mama wakati ndiye alihusika na wao kuwa maskini kwa kutafuna miradi ya UWT? Baada ya kashafa hiyo ndio Lowassa akamtoa na kumpa UDC.
   
 13. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Juzi, Jumamosi usiku TBC walikuwa na kipindi walichokianzisha cha kuwakutanisha wagombea ubunge na wapiga kura wao ili waweze kuelezea sera zao na wapiga kura waweze kuwauliza maswali.

  Moja ya jambo lililonifurahisha ni la mgombea wa CCM kuhamaki na kuanza kuropoka hovyo akitishia kumpeleka mahakamani muuliza swali kama asingetoa vielelezo vya tuhuma alizotoa kuwa yeye (Ng'umbi) alishawahi kuhusishwa na tuhuma ya kuuza mali nyumba za umoja wa wanawake alipokuwa mwenyeketi wa umoja huo. Nadhani hii haikuwa mara ya kwanza kusikia tuhuma hizi.

  Mgombea yule alilipuka na kuanza kulopoka hovyo na kumtishia yule muuliza swali, bahati nzuri yule muuliza swali alimjibu kuwa haogopi kwenda mahakamani na akamtaka mgombea ajibu hoja na si kurusha vitisho... yule mama hakujibu na alipopewa nafasi ya kufanya majumuisho yake alirejerea swali lile huku akionyesha kuyumbishwa kiakili na swali lile.

  Swali je ukweli ni upi? Je huyu mama ni kweli aliuza nyumba zile kwa manufaa yake? Kama ni kweli, je huyu mtu atafaa kutuwakilisha sisi wanyonge kudai haki zetu na kuhakikisha kuwa haki yetu inasimamiwa ipasavyo???
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,471
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Huyu mama huyu.....haya jamani...ana bahati sana....JK aliwahi muwakia akiwa DC Mvomero.....ajabu ni kuwa watu wasio wanasiasa wanang'ang'ania siasa tuu...si arudi MECCO alikokuwa fundi barabara?
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mhu!
  Mtangazaji amemtukana mgombea wa CCM (kwa kumuambia ukweli)
   
 16. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  Ubunge Ubungo ni wa kijana wetu na mwenzetu kamanda John Mnyika ...FULL STOP... huyo mama kama ni mwizi au jambazi la mali za umma akawaibie hao ccm wake...ile ubunge ata akija bila nguo "hatumpiiiii"
   
 17. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Siku zote hayo ndo majibu ya mtu anayeambiwa ukweli pale anapokuwa anaulazimisha ulimi wake upingane na roho/moyo wake!
  Kaaaaziiiiiiiii kweli kweli
   
 18. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hata mi nilishangaa sana... watu kama hawa wakikabiliana na sofia simba lazima patachimbika! manake sofi nae huwa halazi damu!
   
 19. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Tunatafuta 50/50 kwa hiyo kuweni wapole tu tuwapeni maendeleo sisi ccm............kidumu chama cha mafisadi
   
 20. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ukiingalia hata picha ya huyo mama inaonyesha tools of analysis kichwani ni sifuri. na sielewi inaonekana hata wana-ccm walioko ubungo wameichoka ccm, ingekuwa wanaitaka ccm wangemteua Nape.
   
Loading...