Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge Sumbawanga kuomba kura za Ubunge kwa kutaja miradi ya Ubungo Interchange, flyover za Dar na ukuta wa Mererani

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,395
512
Ukijiuliza Ubungo Interchange na Sumbawanga wapi na wapi. Yaani wakupe kura kwa sababu ya flyover za Dar. Hivi wabunge wa CCM wanajielewa kweli?

Mgombea anajikakamua kweli kweli kuhusu ndege Rais alizonunua na jimbo lake wapi na wapi? Wagombea ubunge wameshindwa wengi wao kujipambanua wao kama wao kwanini achaguliwe tena?

Mgombea anaomba kura kwa kuaambia nipeni kura nikaungane na Magufuli tukanunue ndege zingine. Wakati huo Wananchi hawana maji, halo zao ni mbaya kweli.

Sio mantiki ya kuwachagua wambuge wa CCM.

Naona CCM imechoka hoi ipo taabani kweli, mgombea wa juu, kachoka, wabunge wamechoka, madiwani ndo usiseme. Kazi kwenu wananchi.
 
Ukijiuliza Ubungo Interchange na Sumbawanga wapi na wapi. Yaani wakupe kura kwa sababu ya flyover za Dar. Hivi wabunge wa CCM wanajielewa kweli?

Mgombea anajikakamua kweli kweli kuhusu ndege Rais alizonunua na jimbo lake wapi na wapi?
Kuna uwanja wa kimataifa unajengwa sumbawanga mwaka huu wa fedha yuko sahihi kuongelea ndege pia kuna soko la kimataifa linajengwa sumbawanga la mazao na madini ndege muhimu

Mazao mengi kutoka sumbawanga soko lake kuu liko dar es salaam kaulize madereva wa malori foleni waliyokuwa wakikutana nayo kabla ya flyover wakitumia mafuta mengi mno wakiingia dar au kutoka dar kwenda sumbawanga
 
Matatizo ya nchi sio wananchi wenyewe kwa kujitakia. Tena naona nikama chama tawala kilikua kinaufanya mtaji, umbumbu wa watanzania. Watanzania wameendeshwa kweli na kudharauliwa sana.
Kazi kwenu watanzania
 
Huyo hafai kupewa kura hata moja!

Ndio maana mkoa huo unakuwa nyuma kimaendeleo sababu viongozi wake wanashabikia maendeleo ya mikoa mingine badala ya kuyapeleka maendeleo hayo mkoani hapo!

Hata hivyo, taarifa kutoka huko zinasema wanaRukwa walishaikataa CCM toka mwaka 2010, lakini huko ndiko udanganyifu mkubwa wa kuchakachua matokeo hufanyika na sababu kubwa ni kutokana na mwamko mdogo wa wananchi wa mkoa huo kutumia vyombo vya habari kupaza sauti zao.

Hawana utamaduni huo wa kudai haki kupitia vyombo vya habari ndo sababu hata haki zinapominywa mambo yanaishia chini kwa chini lakini kiukweli mkoa huo kwa sasa ni sehemu ya mikoa ambayo inaunga mkono sana upinzani!
 
Wanasumbawanga huwaambii kitu kwa Magufuli
Ukitaka wakukimbize mseme vibaya Magufuli
Usidanaye wananchi mimi nina jamaa zangu wanaishi huko, Wale wananchi kwasasa hawaipendi kabisa CCM ukitataka kujua hili tazama hata mapokezi waliyompa Lissu alipokwenda huko kuna clip zilitupiwa humu!

Wana Sumbawanga wamechukizwa na ubaguzi wa kimaendeleo unaoendelea kufanywa na serikali dhidi ya mkoa huo! CCM ilifanya hila ikatwaa majimbo yote ya mkoa huo, lakini hakuna mbunge yeyote toka huko aliyepewa uwaziri wala naibu waziri! Uwaja wa ndege wa mkoa huo ambao ulitumiwa na Baba wa taifa mwalimu Nyerere mpaka upo vilevile ni kinjia flani chenye vichaka vya nyasi, huku Chato iliyokuwa kijiji majuzi tu ikijengewa uwanja wa kimataifa!

Miaka yote 5 hakuna mradi wowote mkubwa uliojengwa mkoani huko ambao serikali ya awamu ya tano inaweza leo kujivunia na ninafkiri ndio sababu Mgombea wa CCM hajakanyaga kabisa huko!

Hata hii miradi ya bandari za Kasanga na Kalema ni miradi ya Kikwete! Alafu leo jitu linaibuka na kusema Sumbawanga huwezi waambia kitu kuhusu CCM! Ni uwongo wa mchana kweupe, CCM ilishachokwa kote!
 
Sasa kama anataka Sumbawanga iwe na hayo pia.. ulitaka ataje ya nchi zingine!!!!

2020 kesho kutwa ni kama tunajaza tiki za upendo 💚💛💚💛💚
 
Usidanaye wananchi mimi nina jamaa zangu wanaishi huko, Wale wananchi kwasasa hawaipendi kabisa CCM ukitataka kujua hili tazama hata mapokezi waliyompa Lissu alipokwenda huko kuna clip zilitupiwa humu!
Wana Sumbawanga wamechukizwa na ubaguzi wa kimaendeleo unaoendelea kufanywa na serikali dhidi ya mkoa huo! CCM ilifanya hila ikatwaa majimbo yote ya mkoa huo, lakini hakuna mbunge yeyote toka huko aliyepewa uwaziri wala naibu waziri! Uwaja wa ndege wa mkoa huo ambao ulitumiwa na Baba wa taifa mwalimu Nyerere mpaka upo vilevile ni kinjia flani chenye vichaka vya nyasi, huku Chato iliyokuwa kijiji majuzi tu ikijengewa uwanja wa kimataifa!
Miaka yote 5 hakuna mradi wowote mkubwa uliojengwa mkoani huko ambao serikali ya awamu ya tano inaweza leo kujivunia na ninafkiri ndio sababu Mgombea wa CCM hajakanyaga kabisa huko! Hata hii miradi ya bandari za Kasanga na Kalema ni miradi ya Kikwete! Alafu leo jitu linaibuka na kusema Sumbawanga huwezi waambia kitu kuhusu CCM! Ni uwongo wa mchana kweupe, CCM ilishachokwa kote!

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Jamaa zako unaandika kama vile eti wamejaza Sumbawanga nzima... hasira zenu za kutopenda kujiongeza na kutaka vya dezo... umeandika upupwu wa karne.. eti kutaka kupinga eeeeh.. jicheke sana.. ena tiki yako moja.. lala nayo.. tulia uone ya 2020.. ulete uongo mwinginevhata mkoa huo hujawahi kanyaga mguu..
 
Unacheka na point badala ya kuleta point! Dalili ya mjinga ni kuchekacheka hovyo! Ungejua kujiongeza ungeacha kufagilia uwongo! Anyway siku hizi hata ukahaba ni kujiongeza!
 
Haya maneno umeandika.. imeonyesha nimeandika ya kweli 💯... ujanja achia akina sisi.. kumbe ulisha ninoti.. haya pokea hizi 💉💉💉 tatu tosha dozi kwa leo..🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kijana miezi mitatu ya kempeni nimefika sumbawanga
Mimi sio mtu wa porojo
Usidanaye wananchi mimi nina jamaa zangu wanaishi huko, Wale wananchi kwasasa hawaipendi kabisa CCM ukitataka kujua hili tazama hata mapokezi waliyompa Lissu alipokwenda huko kuna clip zilitupiwa humu!
Wana Sumbawanga wamechukizwa na ubaguzi wa kimaendeleo unaoendelea kufanywa na serikali dhidi ya mkoa huo! CCM ilifanya hila ikatwaa majimbo yote ya mkoa huo, lakini hakuna mbunge yeyote toka huko aliyepewa uwaziri wala naibu waziri! Uwaja wa ndege wa mkoa huo ambao ulitumiwa na Baba wa taifa mwalimu Nyerere mpaka upo vilevile ni kinjia flani chenye vichaka vya nyasi, huku Chato iliyokuwa kijiji majuzi tu ikijengewa uwanja wa kimataifa!
Miaka yote 5 hakuna mradi wowote mkubwa uliojengwa mkoani huko ambao serikali ya awamu ya tano inaweza leo kujivunia na ninafkiri ndio sababu Mgombea wa CCM hajakanyaga kabisa huko! Hata hii miradi ya bandari za Kasanga na Kalema ni miradi ya Kikwete! Alafu leo jitu linaibuka na kusema Sumbawanga huwezi waambia kitu kuhusu CCM! Ni uwongo wa mchana kweupe, CCM ilishachokwa kote!
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom