Mgombea Ubunge: Polisi wasijichunguze kifo cha Mwanafunzi wa NIT

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
tlp%2Bpic.jpg


Aliyekuwa mgombea ubunge Kinondoni kupitia Chama cha Tanzania Labour (TLP) katika uchaguzi uliofanyika Februari 17, 2018, Dk Godfrey Malisa amesema polisi hawapaswi kuhusika katika uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwiline.

Akizungumza leo Februari 19, 2018 na MCL Digital, Malisa amesema polisi ni sehemu ya watuhumiwa, hivyo hawawezi kujichunguza wenyewe.

Akwilina aliuawa Februari 16, 2018 kwa kupigwa risasi na polisi eneo la Mkwajuni wakati askari wakiwatawanya wafuasi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliokuwa wakielekea katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai hati ya viapo vya mawakala wao.

Tayari Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia askari wake sita kwa uchunguzi pamoja na silaha zao huku Kamanda wa kKanda hiyo, Lazaro Mambosasa akisema hawajathibitisha kama risasi iliyompata Akwilina ilipigwa na askari na kwamba, watuhumiwa 40 wanachunguzwa ili kubaini kama miongoni mwao walikuwa na silaha za moto.

“Namuomba sana Rais (John Magufuli) kuingilia kati uchunguzi huru wa tukio la kifo cha mwanafunzi. Polisi hawatakiwi kujichunguza wenyewe kwa sababu ni sehemu ya watuhumiwa, inawezekaje mtuhumiwa kujichunguza?” amehoji Malisa.

“Tena wanasema tutachunguza kama risasi ilikuwa ya polisi au waandamaji. Namuomba Rais aingilie kati ili iundwe tume huru ya uchunguzi.”
 
Back
Top Bottom