Mgombea ubunge: Nikipata ubunge nitaweka pazia kwenye Mlima Kilimanjaro

yahoo

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
3,527
1,405
Mgombea ubunge katika mkoa wa Kilimanjaro ameahidi kuweka bonge la pazia ili watu wa nchi jirani wanaopiga pesa kupitia mlima huo waambulie patupu.

====

Moja ya stori itakayokuacha hoi ni ya Mgombea Ubunge katika Jimbo la Moshi Mjini Omary Mwariko ameahidi kushawishi utengenezaji wa noti ya shilingi elfu hamsini ya Rais Magufuli kama zawadi kwa mambo makubwa aliyofanya.

Mbali na hilo Mwariko amesema atashauri kubadilishwa kwa jina la Mji wa Moshi na kuweka pazia Mlima Kilimanjaro, huku akipendekeza Wizara inayohusika na masuala ya sanaa kuruhusu kuruka na ungo.

 
Haha paka uchaguzi uishe tutaona mengi.Wa Serengeti nae atasema tutajenga Ukuta ili nyumbu wasihamie Kenya kipindi cha ile migration yao.
 
Mgombea ubunge katika mkoa wa kilimanjaro ameahidi kuweka bonge la pazia ili watu was nchi jirani wanaopiga pesa kupitia mlima huo waambuie patupu.
Itakua katumia lugha ya mafumbo kama Kiswahili umedandia sio lugha yako lazima hautomuelewa nn alimaanisha ila sio pazia kama la mlangoni kwako
 
Mgombea ubunge katika mkoa wa kilimanjaro ameahidi kuweka bonge la pazia ili watu was nchi jirani wanaopiga pesa kupitia mlima huo waambuie patupu.
Wanapiga pesa ipi? Kuna mtalii anapanda kilimanjaro kutokea Kenya?
 
namkubali sana mbunge huyu na nina uhakika atatupeleka mbali sana sisi kama Watanzania. 2025 ningependa awanie urais. #MATAGA

Sote tumepiga magoti na kukubaliana na hii kauli yako

2257396_IMG_20191230_125043.jpeg


 
Na hapo wananchi wakashangilia na kushabikia sana na kufurahi, yaani ningekua mkaazi wa hilo jimbo, kura yangu ingekua ya kwake mara moja.....CCM hoyeeee!!! CCM mbele kwa mbele!!!!
Mkuu neno makarao lina maana gani?
 
Huyu mzee ameongea pumba mwanzo mwisho
Anasema atabadili kabisa jina Moshi,
Atafanya maboresho ya usaifiri wa ungo angani
 
Uchaguzi mkuu wa mwaka huu umeanza kwa kishindo kuanzia kuvunja rekodi ya namba ya wagombea na vituko huko kwenye majukwaa.

Pia kuna matukio ya kushitukiza kama kumwagwa kwa Makonda na kadhalika. Ah! Kidogo nimsahau "baba askofu" alivyoponda vyeo vya kisiasa na kisha kuchukua fomu ya kugombea ubunge.

Katika hali isiyo ya kawaida mgombea ubunge huko Kawe aliomba kura kwa Kichina.

 
Back
Top Bottom