Mgombea Ubunge NCCR (Mawazo Metusela) ajivua Uanachama NCCR

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,200
4,991
Hoja hii ilianzishwa wakati JF ikiwa katika marekebisho makubwa, haikuweza kupatikana hivyo tunairejesha:

Emil Lusambo said:
Mawazo Metusela (0717 238011) ambaye alikuwa Mgombea Ubunge kupitia NCCR ameamua kujivua uanachama na NCCR kwa sababu ya Kuhofia Kutumika na CCM.

Bw Mawazo anasema Kitendo cha Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kuwa na Imani na Mwenyekiti wa Upinzani (NCCR) na kumuteua kwa nafasi ya ubunge , kimeonyesha Dhahiri kuwa , James Mbatia amekuwa akitumika kuua Upinzani kwa muda Mrefu kiasi cha kuaminiwa na waliomupa kazi hiyo.

Kufuatia uteuzi huo Mawazo amesema NCCR itashindwa Kukosoa Utendaji wa Rais Kikwete na hivyo Chama chao kitashindwa kuwakilishwa na mwenyekiti aliyehuru kimawazo!!

"Ningeweza kumushauri Mbatia aachie Ngazi ya uenyekiti Taifa , lakini kwa habari nilizozipata, Mbatia hataki kufanya hivyo, na sasa naamua kujivua unachama ili kutafuta chama kisichotumika na CCM kama ilivyo sasa , Mbatia anaonekana wazi kuwa ni Pandikizi la CCM!!
 
Back
Top Bottom