Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge Mwenzetu alilipia ukumbi wa kura za Maoni akashinda

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Baadhi ya wagombea Ubunge wa Kura za Maoni CCM katika jimbo la Arusha mjini wamefichua mazito siri ya Ushindi wa mgombea mwenzao Mrisho Gambo aliyepata kura 333 na kufuatiwa na Philemon Mollel aliyepata kura 68 kuwa alilipia ukumbi wa uchaguzi na kulala katika hotel ya Mt.Meru karibu na ukumbi wa uchaguzi siku moja kabla ya uchaguzi ili kujijengea mazingira mazuri ya kukutana na wajumbe.

Makada hao wa CCM ambao waligombea nafasi hiyo, RAYSON NGOWI NA VICTOR NJAU wameamua kujilipua kwa kudai kwamba hawezi kuvumilia kuona demokrasia ikibakwa na wenye fedha kwa uroho wa madaraka jambo hilo ninapoteza heshima ya CCM na kuwapa nguvu wapinzani.

Siku chache baada ya kura za maoni kupitia hapa nchini za kupata waakilishi wa ubunge katika majimbo makada wa chama chamapinduzi CCM Mkoa wa Arusha wamelalamikia kitendo cha wajumbe kumpa kura za ndio aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kufanikiwa kuzoa kura za kishindo .

Makada hao wamesema wajumbe wa mkutano Mkuu maalum wamepingana na kauli ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi taifa John pombe Magufuli aliyemtoa kwenye nafasi ya Ukuu wa Mkoa Mrisho Gambo baada ya kupingana na watendaji wenzake akiwemo Mkuu wa wilaya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Arusha Maulid Madeni

"CCM ilipewa ukumbi bure na AICC kufanya mkutano wa kura za Maoni lakini ulibadilishwa ghafla na kupelekwa Mount Meru iweje CCM ikachukue ukumbi wa gharama kubwa za mamilioni ya fedha hii nia ajabu"

"Kilichonisukuma hapa ni uzalendo wa nchi yangu na chama changu ninapogundua haki imekiukwa siwezi kuvumilia nikiwa kama mtumishi wa mungu...

"Mgombea Mwenzetu alipata namba siku moja kabla ya uchaguzi, mgombea Mwenzetu kutoa usafiri kwa wajumbe, kulipia watu chai, kulipia ukumbi, kulala hoteli tuliofanyia ukumbi na kulala chumba namba 403 ushahidi tunao, mgombea Mwenzetu kupanga safu ya madiwani, Rais alisema uchaguzi lazima uwe huru matokeo yake hili jimbo litaenda upinzani" Alisema Ngowi.


IMG-20200802-WA0002.jpg
 
Ok wao walishindwa au walizuiliwa kukodi ukumbi na angalau kupata ka gheto ndani ya ukumbi
 
Baadhi ya wagombea Ubunge wa Kura za Maoni ccm katika jimbo la Arusha mjini wamefichua mazito siri ya Ushindi wa mgombea mwenzao Mrisho Gambo aliyepata kura 333 na kufuatiwa na Philemon Mollel aliyepata kura 68 kuwa alilipia ukumbi wa uchaguzi na kulala katika hotel ya Mt.Meru karibu na ukumbi wa uchaguzi siku moja kabla ya uchaguzi ili kujijengea mazingira mazuri ya kukutana na wajumbe.


Makada hao wa CCM ambao waligombea nafasi hiyo ,RAYSON NGOWI NA VICTOR NJAU wameamua kujilipua kwa kudai kwamba hawezi kuvumilia kuona demokrasia ikibakwa na wenye fedha kwa uroho wa madaraka jambo hilo ninapoteza heshima ya CCM na kuwapa nguvu wapinzani.Siku chache baada ya kura za maoni kupitia hapa nchini za kupata waakilishi wa ubunge katika majimbo makada wa chama chamapinduzi Ccm Mkoa wa Arusha wamelalamikia kitendo cha wajumbe kumpa kura za ndio aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kuganikiwa kuzoa kura za kishindo .


Makada hao wamesema wajumbe wa mkutano Mkuu maalum wamepingana na kauli ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi taifa John pombe Magufuli aliyemtoa kwenye nafasi ya Ukuu wa Mkoa Mrisho Gambo baada ya kupingana na watendaji wenzake akiwemo Mkuu wa wilaya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Arusha Maulid Madeni


"CCM ilipewa ukumbi bure na aicc kufanya mkutano wa kura za Maoni lakini ulibadirishwa ghafla na kupelekwa Mount meru iweje CCM ikachukue ukumbi wa gharama kubwa za mamilioni ya fedha hii nia ajabu"


"Kilichonisukuma hapa ni uzalendo wa nchi yangu na chama changu ninapogundua haki imekiukwa siwezi kuvumilia nikiwa kama mtumishi wa mungu...


"Mgombea Mwenzetu alipata namba siku moja kabla ya uchaguzi ,mgombea Mwenzetu kutoa usafiri kwa wajumbe,kulipia watu chai,kulipia ukumbi ,kulala hoteli tuliofanyia ukumbi na kulala chumba namba 403 ushaidi tunao,mgombea Mwenzetu kupanga safu ya madiwani ,rais alisema uchaguzi lazima uwe huru matokeo yake hili jimbo litaenda upinzani"Alisema Ngowi


View attachment 1524877
Hawa wanajiita wana demokrasia na ambao pia waliokuwa watia nia,mimi ningewashauri ya kuwa badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari ni vizuri wangepeleka malalamiko yao kwenye vyombo vinavyohusika ili sheria ichukue mkondo wake.
Hii namna waliyokuja nayo yenyewe ni vurugu tupu na wala sidhani kama ni ya kuwapatia majibu wanayoyahitaji kwa sababu kwanza wenyewe hawakubaliki hata kidogo kwa maelezo ya mmoja wao ni kwamba kapata kura mbili tu

yaani wajumbe wooote ni wawili tu wanaomkubali mtu huyu. Ni aibu kwanza hata hiyo miaka tisa yako ya udiwani(yaani vipindi viwili) ulikuwa unachaguliwa kwa sababu kwenye kata yako inaelekea hukuwahi kuwa na mtu wa kumshindanisha na wewe.manaana kama ungekuwa umekisaidia chama na umewasaidia wananchi wako wakati huu ndio wakati ulipaswa kuonekana uking’ra ktk kura za maoni ili upewe bendera ya kwenda kupambana na upinzani na hatimaye uibuke kuwa mbunge utakayelisaidia jimbo na watu wake na hatimaye kuiweka ccm mahali pazuri.

nawashauri mliopata kura chache pamoja na kwamba mchakato bado unaendelea na pengine jina lako wewe uliyepata kura chache linaweza kuja kupita baadaye na ukawa wewe ndiye mgombea rasmi lakini hata hivyo endeleeni kukubali kisaikolojia kwamba mmeanguka kidogo ila wapo waliowazidini kwa kuonekana kwamba wanafaa lakini hata kama mmekata tamaa msikiharibie chama kwa matangazo yasiyokuwa na maana kwamba viongozi wake wa mkoa na hata wilaya ni wala rushwa hii ni picha mbaya sana mnayokiwekea chama kwenye macho ya wanachama wa kawaida na hata wap

sidhani kama wajumbe watakuwa si waelewa kiasi unachofikiri maana hata kama wangepewa rushwa wangepokea lakini mwisho wa siku wangempigia kura yule wanaeamini kuwa ataweza kwenda kupambana na upinzani na mwisho wa siku kuibuka kidedea akiwa mbunge tena aliyechaguliwa kwa kura za kutosha.

nao wajumbe ambao ndiyo waliokuwa wapiga kura pengine wanamfahamu kwa ukaribu zaidi mtia nia waliyempigia kura nyingi zaidi kwa sababu wajumbe hawa ndiyo wawakikishi wa chama ktk ngazi ya wilaya na hivyo ktk majukumu yao ya kila siku ktk kurende kwao kazi wamekuwa mara nyingi wakikutana na waliyeamua kumpa kura na hivyo wanaufahamu utendaji wake wa kazi
Na wanaamini kuwa wakifanya naye kazi au hata kama atafanya na watu wengine wenye nia njema basi chama hakitapata aibu.katika wajumbe waliokuwa wanafikia hesabu inayozidi Mia nne unao wafuasi wawili tu na bado unawapigia kelele za malalamiko watu wenye wafuasi zaidi ya Mia tatu siyo aibu hii?.ni wajumbe wawili tu ambao hawakupata kuwa wala rushwa ama ndo ambao walikula rushwa na kutokumpigia mtoa rushwa? jaribu kidogo kutumia akili yako bila kuwa na chuki.
Kwa kifupi ni kwamba wajumbe wameona kuwa huyu anawafaa wao na wananchi kwa ujumla wake na wakati wa kumpigia kura hawakuuweka ubinafsi unaoufikiri wewe wa kusema kwamba na wewe diwani unayo tamaa ya kushinda basi wakupe kura.

inawezekana kweli kwamba yupo mgombea mnayemtuhumu kwamba alitoa rushwa lakini je ninyi mnaofahamu kanuni na sheria za chama je sheria hizo ama kanuni Kuna mahali zinapowaelekeza mnapokuwa na malalamiko pa kuyapeleka ni kwenye vyombo vya habari?,hapa ndipo haki itakapopatikana? ama mmeamua kuongea kwa maana tu ya kumpaka matope mgombea flani aliyewashinda kwa kura na sasa mmeamua kwa kupitia vyombo vya habari kuvuruga maamuzi ya kura zilizopigwa na wajumb kwa sababu ya chuki zenu na hasira ya kushindwa ktk kinyang’anyiro cha awali.

ni kweli rais aliisafisha safu yote ya wateule wake kwenye ngazi ya mkoa na hata wilaya kwa sababu alizoziona yeye lakini pia hakuacha kutaja ila kabla na hata baada ya kutengua wateule wake hao raisi hakuwahi kuwasema kwamba wasiende tena kwa wananchi kutafuta ridhaa ama fursa za kuwatumikia kwa maana ya ubunge au hata udiwani

acheni kuwatengeneza wanahabari na vyombo vya habari kila upande ili kupaza sauti zenu enyi wabinafsi mlioshindwa kwenye kura za mwanzo na badala yake shikamanani kwa Umoja ili kukisaidia chama cha mapinduzi,tena msisahau kuwa wapo watia nia wenzenu waliokisaidia sana chama katika ngazi ya wilaya na mkoa kwa maana ya kukiimarisha chama dhidi ya upinzani na wajumbe wanawafahamu na ndiyo maana hata mkaona wengine wamewazidi kwa kura kwa sababu ya historia waliyoiandika ktk utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na hasa ktk kukitumikia chama.
hivyo nawashauri acheni majungu,acha michakato iendelee kwenye chama ktk ngazi ya mkoa na taifa ili hatimaye apatikane mgombea atakayeweza kukibeba chama dhidi ya upinzani na hatimaye kuutoa mchango wake wa utumishi kwa watu wa arusha na taifa kwa ujumla.
 
Hahaha sasa kwanini wao hawakwenda huko AICC badala yake nao wakakubali kwenda huko Mt.Meru hotel?!

Mshindi hua mmoja tu, hata wangeenda wapi angeshinda mmoja tu na wangelalamika tu.
 
Mrisho Gambo analalamikiwa na wengi sana.miaka yote ya uongozi wake kama Mkuu wa Mkoa Arusha aliutumia kujijenga kisiasa huku akiwadanganya Wakuu wake eti anaibomoa CDM.

Matokeo yake ndio hayo hakuna wa kumlaumu zaidi ya aliyemteua.RPC,Mkuu wa TAKUKURU waliwekwa mfuko badala ya kupambana na rushwa wakawa walinda mtoa rushwa.

Wajumbe walionunuliwa walilazimishwa kupiga picha karatasi ya kura kama ishara ya ushahidi kwamba walitimiza ahadi yao kwa mtoa rushwa.

Kamati kuu ya CCM inawajibu mkubwa wa kuwaondoa wale wote waliobainika kutoa rushwa ili kujenga heshima ya chama

Wasalamu

Ngongo

Safarini Masasi,kwasasa nimefika Rufiji.
 
Back
Top Bottom