Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema awekewa pingamizi na Mgombea kwa tiketi ya CUF

habariyamujini

JF-Expert Member
May 16, 2013
3,094
456
Pingamizi lililowekwa na Mgombea wa CUF kwa Mgombea wa Chadema Ubunge Chalinze.
Posted by: TZA two March 13, 2014 Siasa37 views
Hii ni ya leo March 13 2014 ambayo inamuhusu Mgombea ubunge kwa tiketi ya Cuf jimbo la Chalinze kwenda kwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo hilo wa Chadema.
Mgombea huyo ni Fabian L. Skauki ambaye ni anagombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la CHALINZE kwa kumuwekea Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mathayo Torongey kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea.
Sifa alizozitaja Fabian anazozihusisha na kupoteza kwa sifa ya kugombea kwa Mathayo M. Torongey ni kuwa amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni Bishara ambapo amesema Sio kweli kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi na pia hajulikani anafanya kazi gani.
Pingamizi lingine ni kwamba katika fomu yake amejaza kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza,taarifa ambazo Fabian amesema ni za uongo na kwamba mgombea huyo hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.
Pingamizi la tatu alilowekewa Mathayo ni kusemekana medanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea,ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika na Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.
Pingamizi la mwisho aliloliweka Fabian dhisi ya Mathayo ni kile kinachosemekana kushindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25 na badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la CHALINZE na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni

JINA LA MDHAMINI NAMBA YA KADI KURA

HABIBU ALLY SAIDI * 16886275*
MOHAMMED RAMADHANI *30376567*
ABDULKADIR ALLY *49264905*
SHABANI SULEYMAN *16984045*
JUMA MRISHO *48759563*
RAJABU ALLY *16872368*
MANENO MIRAJI *16872059*

Wananchi wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo ambayo wamejazwa wanatokea.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakidhi vigezo vya kuwa wadhamini.
Kingine kilichosemwa na Fabian ni kusema mgombea ubunge huyo kupitia Chadema Mathayo amedanganya uraia wake na kwamba yeye si Mtanzania wa kuzaliwa ndio maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia wake na hivyo anakosa sifa ya kuwa mgombea.
Hivyo ameiomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ndugu MATHAYO.M.TORONGEY kwa kuwa anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa mgombea.
millardayo.com kesho itatoa nafasi ya kuusikiliza upande wa pili ambao haujapatikana baada ya hizi habari kusambazwa kwenye vyombo vya habari.
 
Ati mgombea ubunge kwa tiketi ya CDM hajuwi kuandika wala kusoma pia hajuwi kiingereza! Biashara yake haieleweki wala maisha yake pia amekuwa mtu wa kuunga unga!

Wapinzani at work!
 
Kama kweli basi kosa sio lake ni la wakuu waliomkubali awe mgombea wao ,hapo hakuna cha upinzani wote wanatafuta tonge kupitia vyama vyao ,sasa kila mmoja anatumia ubavu wake ili kupata nafasi ,kusema sisi ni wapinzani tusiekeane pingamizi hilo halikubaliki.

Wakubanwa hapa ni wakuu wa CDM waliomuachia mtu aliekuwa hajui kusoma wala kuandika kumpitisha wakati huko mbele kila mtu anatafuta kosa ili akukwamishe ,sidhani kama wakuu wa CUF walikwenda kuyachunguza hayo madudu ya mgombea wa CDM ila ni mgombea mwenyewe katika jitihada zake za kutafuta rizki.

Mtu hajui kusoma wala kuandika halafu mnataka kupiga makelele ,kama ni hivyo inaonekana mpo wengi aina ya akina Sendeka.

Na mwisho jamaa kapiga msumari kasema huyo mgombea wa CDM si Mtanzania ,Chadema hamkuyajua hayo au mmeingizwa mjini ??? Mchunguzeni ili mara ya pili msifanye kosa.
 
Ati mgombea ubunge kwa tiketi ya CDM hajuwi kuandika wala kusoma pia hajuwi kiingereza! Biashara yake haieleweki wala maisha yake pia amekuwa mtu wa kuunga unga!

Wapinzani at work!
Hiyo ni kweli kabisa wakazi wengi wa Chalinze hawajui kusoma wala kuandika na hii imesababishwa na utawala dhalimu wa CCM. Mfano kiingereza cha mwenyekiti wa CCM taifa ndio kichekesho zaidi
 
kama wenje na masha pale nyamagana mwisho wa siku waziri akatulia bila kufanya kampeni alf mwanaume akaja na speed ya ajabu akamzunguka mala 2 kwenye sanduku la kura, stay tune
 
Hiyo ni kweli kabisa wakazi wengi wa Chalinze hawajui kusoma wala kuandika na hii imesababishwa na utawala dhalimu wa CCM. Mfano kiingereza cha mwenyekiti wa CCM taifa ndio kichekesho zaidi

Kiingereza cha Mbowe ni sawa na cha mtoto wa kimangati mwenye miaka minne anayejifunza kihindi
 
kiingereza cha mbowe ni sawa na cha mtoto wa kimangati mwenye miaka minne anayejifunza kihindi
. Nakuambia koma tena koma usilete dharau zenu za makabila ya wenzenu na dini. Hayo ya kutolea mf kabila naomba ukome. Usilete tabia za kisimbe humu
 
ati mgombea ubunge kwa tiketi ya cdm hajuwi kuandika wala kusoma pia hajuwi kiingereza! Biashara yake haieleweki wala maisha yake pia amekuwa mtu wa kuunga unga!

Wapinzani at work!

hiyo ni janja ya nyani kula hindi bichi ya ccm kupitia cuf ambao imewanunua tangu muda kuanzia zenji. Hapo bilionea mfanya biashara ikulu keshapita kwa stahili hii.
 
. Nakuambia koma tena koma usilete dharau zenu za makabila ya wenzenu na dini. Hayo ya kutolea mf kabila naomba ukome. Usilete tabia za kisimbe humu

Kwi kwi kwiiii ,mkuu sasa wewe ni muhindi au mangatii?
 
Wapinzani wenyewe hamupatani mmegawanyika sana kila mtu na chake! Vita vya panzi hivyo......
 
Back
Top Bottom