Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge Khamis Mwinjuma (Mwana FA) aliwahi kukiri kuwachukia baadhi ya watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Askari wa Jiji)

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,319
Soma pia>>> Do African political activists actually fight for democratic change or they simply keep alive a well-known old saying that "It's Our Turn to Eat"?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ndugu zangu watanzania;

Ninapenda kuchukua wasaa huu kumpongeza kwa dhati na kwa moyo mkunjufu kabisa ndugu yangu, kaka yangu na binamu yangu Khamis Mwinjuma (Mwana FA) kwa kuteuliwa kuwa mgombea ubunge kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) katika jimbo la Muheza. Mungu akuongoze na kukupigania katika harakati zako binamu.

118966735_10158220352551001_8925057089718232475_o.jpg


Sasa binamu, ingawa sisi waswahili tuna kamsemo ketu kanasema kwamba "ya kale hayanuki" pia "yaliyopita si ndwele, tugange yajayo" kwa miaka kadhaa iliyopita katika harakati za kazi zako za sanaa ya muziki uliwahi kuimba maneno haya katika wimbo unaoitwa MCHIZI WANGU REMIX;

HAYA NDIO SEHEMU YA MENEO YA MWANA-FA
============
Moyo unanienda mbio kama unaendeshwa na schumacher kila nikiwaza mchizi wangu huenda unateseka kwangu ni zaidi ya pacha binamu wa haswa haswa siwezi kuacha ukichoreka siwezi kuona unanyanyaswa mi ni kivuli chako siwezi kuacha kukufuata na kufeel ile kinoma zaidi ya maelezo si mzuka? I don't deserve you najua we nakuona kama zali we kwangu zaidi ya zawadi imeoshwa na mchanga wa kaburi? naiendesha DSM so wanachonga sometimes zibia masikio vitu vibaya ndo walivyo wanadamu nawachukia kama askari wa jiji.

Mimi kwa ushauri wangu tu kama mshabiki wa karibu kabisa wa kazi zako za sanaa na mtu anayekuombea mema katika maisha yako mapya ya siasa ninaomba utoe maneno kadhaa ya kuomba radhi kwa watu wa hiyo kada husika (askari wa jiji uliokuwa unawachukia), hususan kupitia accounts zako za mitandao ya kijamii kama vile Tweeter, Facebook na Instagram.

118995815_10158220352531001_6154003751919271885_o.jpg


Binamu yangu, kwa sasa umeteuliwa na chama chako cha CCM kwenda kupeperusha bendera yao vema kama mgombea ubunge, hii ikiwa na maana kwamba kama sio wapinzani wako basi ni wewe ndiye utakayekuwa mshindi wa uchaguzi huo na "automatically" utapata nafasi ya kuwa miongoni mwa watu muhimu sana hapo jimboni muheza ukiwa pamoja na viongozi wenigne ngazi hiyo husika (Wilaya) kama vile mkuu wa wilaya (DC), Police OCD, TISS-DSO pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya serikali na chama katika kutekeleza majukumu kadha wa kadha ikiwamo ulinzi na usalama wa Raia wa Muheza pamoja na mali zao.

118908755_10158220352561001_1300639482372447852_o.jpg


Kaka yangu mwana FA, ujana una mambo mengi sana mkuu ikiwa ni pamoja na "hormones" pamoja na hasira kuwa juu. Kuna siku inawezekana hao askari wa jiji walikukwaza katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku, sasa ukaamua kwenda kutoa stress kupitia nyimbo. It's okay kwa maana wewe ni mwanadamu una hasira na wao ni wanadamu vile vile na wana mapungufu yao.

Sasa muda umefika kaka mkubwa kuwa muungwana, be humble kisha OMBA RADHI uwaambie kuwa kijana mwenzao ulijikwaa tu ulimi na yale maneno hayakuwa kusudio lako na vile vile hii pia ibaki kama kumbukumbu kwa watanzania wengine wanaojihusisha na kazi za sanaa kwamba, unapokuwa unaongea ni lazima tuwe na AKIBA YA MANENO. Usiongee kwa hasira ukanena kila kitu kwa maana haujui kesho yako

118916573_10158220352556001_2276724395956752875_o.jpg

Nina imani kubwa sana utaufanyia kazi ushauri wangu kwa maana anayekukosoa kwa njia za kiungwana (Constructive Criticisms) ndiye anayekupenda kwa adhati.

OFF-TOPIC KIDOGO:
Kuna siku moja niliona mwana FA ameweka picha ya binti yake mrembo sana kule Facebook. Mwambieni na mimi Infantry Soldier ninacho kidume changu cha miaka 6 kinaanza darasa la kwanza mwakani na sisi wanaume wa mkoa wa Mara ni wagonjwa sana kwa mabinti weupe wa Kitanga, kwa sababu jeuri ya kulipia ng'ombe wengi tunayo. Hahahahaaaaaaaaa, I am just joking bro...!!!! One Love and have a wonderful night.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

BIASHARA: Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher
 
Ulishawahi kumchukia mtu ambae Hana habari na wewe? Hii chuki huwa inamuumiza mchukiaji kuliko mchukiwaji.

Kwahiyo hain hja ya kuomba radhi kama aliamua aweke wazi hisia zake ndo maana hajashtakiwa kwakua hisia zake hazina madhara na upendo haulazimishwi.
 
Back
Top Bottom