Mgombea Ubunge John Pallangyo adakwa na TAKUKURU mkutanoni akigawa Mapesa

Status
Not open for further replies.

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Arumeru Mashariki John Palangyo ama John D jana tarehe 18 July 2020 alikamatwa na kuhojiwa na maafisa wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa takribani masaa 5 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya Rushwa na kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM jimboni humo ili kuwashawishi waweze kumchagua.

Palangyo alichukuliwa akiwa katika kikao cha wagombea wa ubunge kilichokuwa kinaendelea kwenye ofisi za CCM wilaya ya Meru zilizopo kwenye mji mdogo wa Usa-River. Hivyo alilazimika kuacha kikao kikiendelea baada ya maafisa wa TAKUKURU kumpiga pingu.

Taarifa zaidi kutoka kwa Mkuu wa Takukuru wilayani humo,Deo Mtui alidai kuwa ni jambo la kawaida kwa taaisisi hiyo kumhoji mtu yoyote iwapo inataarifa za ukiukwaji wa sheria,hata hivyo alisema msemaji Mkuu wa jambo hilo ni Mkuu wa Takukuru mkoa wa Arusha

Hatua ya mbunge huyo kukamatwa na kuhojiwa na maafisa wa taasisi hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa si. Mara ya kwanza katika.kipindi hiki cha uchaguzi

Kura za maoni kwenye jimbo hilo zinatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumatatu 20/07/2020

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mkewe mdogo (hawara yake) aitwaye Lilian Mtiro maarufu kama Mama Urassa alishikiliwa na maafisa wa taasisi ya TAKUKURU kwa takribani siku siku tatu kwa madai ya kukutwa akijihusisha na vitendo vya rushwa na kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT mkoa.

Hata hivyo inadaiwa kuwa katika mahojiano hayo ya siku tatu Mama Urasa alikana kufahamiana na John D wakati kila mtu anajua kuwa sio tu hawara Bali ni kama mke mdogo .

=====

UPDATES:

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, James Ruge ameiambia JamiiForums kwamba habari hii haina ukweli. Amesema Wagombea wote wa Ubunge wa Arusha, waliitwa kupewa maelekezo na taratibu za Kisheria ambazo wanatakiwa kufuata wakati wa Uchaguzi, ili watakapokamatwa wasilalamike kwamba hawajapewa Elimu ya Rushwa wakati wa Uchaguzi.

Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kwa Rushwa Arusha.

John Palangyo ama John, hajahojiwa na TAKUKURU.
 
Ccm na rushwa ni dam dam
Ile ahadi yao ya mwanatanu waiandike kwa kinyume chake..
Mwenyekiti wao anagawa milungula barabarani mbele ya kamera
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom