Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge CUF Arumeru Magharibi, madiwani watakaonunuliwa kufikishwa Mahakamani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Chama cha wananchi (CUF) Jimbo la Arumeru Magharibi, Mkoa wa Arusha kimempitisha kwa kishindo Bi. Arafa Muya kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Arumeru Magharibi.

Akitangazwa rasmi Leo na kamati tendaji ya CUF, Muya amesema kuwa anajisikia faraja kubwa kujiona mwanamke pekee aliyethubutu kushiriki kinyang'anyiro hicho cha Ubunge na ameahidi kushinda kwa kishindo.

Aidha amewataka wagombea wengine wa nafasi za udiwani ambao wamepita bila kupingwa ndani ya chama hicho kujiamini ,kuwa ngangali na kuacha woga wakati wa kujinadi kuomba kura majukwaani.

Muya ambaye pia ni mwenyekiti wa CUF halmashauri ya Arusha DC,amewaonya baadhi ya wagombea wa chama hicho wenye tabia ya kujitoa nyakati za mwisho iwe kwa kurubuniwa au utashi wa mtu binafsi,kwamba.

Mgombea huyo atachukuliwa hatua kali na chama hicho ikiwemo kufikishwa mahakamani ili kulipa gharama za usumbufu na hasara waliokipatia chama hicho.

Chama hicho kimejipanga kusimamisha madiwani katika kata zote 27 za Jimbo la Arumeru Magharibi na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano.

IMG_20200711_142033.jpg
IMG_20200711_140525.jpg
 
Waanze Kumfikisha Mahakamani Mwenyeketi wao Lipumba kwa Kununuliwa na SISIEMU.
 
Back
Top Bottom