Mgombea ubunge CCM anusurika kuuwawa na jambazi aliyetumwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea ubunge CCM anusurika kuuwawa na jambazi aliyetumwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mchokonozi, Aug 13, 2010.

 1. M

  Mchokonozi Member

  #1
  Aug 13, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmoja wa wagombea ubunge wa CCM aliyeshinda nafasi hiyo kwenye kura za maoni amenusurika kuuwawa na jambazi aliiyetumwa kummaliza baada ya jambazi huyo kumwambia kwamba yeye ni mtu mwema asiyestahili kufanyiwa unyama huo.

  Akisimulia ndugu na jamaa zake, mgombea huyo (jina limehifadhiwa) alisema kwamba jambazi huyo alivamia nyumbani kwake wakati wa usiku, siku chache zilizopita, na alipofanikiwa kuingia ndani alimtambua mgombea huyo, ndipo alipoamua kuweka chini silaha yake na kutoa kitita cha fedha na kumwonesha akisema: "Mzee hunikumbuki, lakini wakati nilipokuwa jela ulitusaidia kwa kutupatia suruali, mashati na viatu".

  "Nimetumwa na (jina limehifadhiwa) nije kukumaliza kwa kuwa unaonekana mkaidi kwao na kwamba utawaharibia ukirudi bungeni. Lakini siwezi kukuua kwa kuwa wewe ni mtu mwema. Wamenipa milioni sita (akamwonesha) lakini hata kwa milioni mia mimi sitakuua. Hustahili adhabu hii, wewe ni mtu mwema," alinukuu mgombea huyo.

  Mgombea huyo ambaye amekuwa machachari kwenye bunge lililopita, alisema kwamba alimwomba muuaji huyo kutoa tamko kwenye mkanda wa video, ambapo alikubali na kusema: "Mimi siogopi kufa. Mke wangu aliuwawa majuzi akipora benki kule (jina limehifadhiwa). Kwa hiyo hata kama wakiniua, niko tayari, siogopi."

  Mgombea huyo amesema kwamba anatafuta siku na muda muafaka kutoa taarifa rasmi kwa umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari. Amesema kwamba anahofia kwamba akitangaza mapema tukio hilo, machafuko makubwa yanaweza kutokea nchini, kwani kilichojaribiwa kwake ni dhahiri kwamba mpango huo uliwalenga watu wengine zaidi yake yeye, na tayari amekwishachukua hatua za kuwatahadharisha watu wengine ambao anadhani waliwekwa kwenye kundi moja na yeye, yaani, kundi la kuuwawa na kupelekwa mapema kuzimu.

  -----------------------------------

  Haya, Mchokonozi nimechokonoa tena. Sasa mjadala uanze rasmi!

  Kweli, mwaka huu ni wa mabadiliko! Kama CCM wanafikia kutaka kuwauwa Watanzania wazalendo, wadilifu, ambao wanataka CCM iwe ya Watanzania wote, basi tumefika pabaya! Tusifike pabaya zaidi!

  >>> Mchokonozi <<<
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hii kitu inaweza kuwa ya kweli na pia inaweza kuwa si ya kweli, labda anataka sympathy
   
 3. B

  BENSON MSEMWA Member

  #3
  Aug 13, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu atakuwa mpinga ufisadi wa kyela
   
 4. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  :welcome::glasses-nerdy:ingekuwa vyema jina lake likajulikana huyo mheshimwa
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tunakoelekea ni kubaya. Nchi kama Mexico hivi leo mafisadi wa madawa ya kulevya wana nguvu kuliko serikali. Inatisha na tuombe Mungu isitokee Tanzania.
   
 6. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Nataka kujua huko Bungeni kuna nini? Maana watu wamekuwa wakatili mpaka kutaka kutoa Roho za wenzao kwa sababu tu ya kuutaka Ubunge. Ni juzi tu nilikuwa kwenye mazungumzo na Kamanda mmoja wa Polisi huko Singida,na akanieleza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Dr.Athuman Rashid Mfutakamba yupo kwenye Hospitali ya Mkoa huo baada ya kunusurika kuuwawa na Majambazi huko Itigi (Manyoni).Kamanda huyo alisema wazi kuwa Majambazi hayo yalitumwa kumfuatilia Dr.Mfutakamba baada ya kushinda kura za maoni katika Jimbo la Igalula Mkoani Tabora.
  Siku ya Tukio hilo majambazi yalitega magogo njiani kwa minajili ya kuzua gari la Mkuu wa Wilaya huyo,Dereva wa Mkuu wa wilaya alijaribu kushuka ktk gari ili akaondoe Magogo hayo,lakini ghafla kukasimama gari nyuma na watu wakamvamia Dr.Mfutakamba na kumshambulia na vitu vyenye ncha kali kichwani.Ilikuwa majira ya usiku,Dereva wa DC alifanikiwa kuponyoka ktk mikono ya watu hao,Lakini DC alishambuliwa na kuibiwa baadhi ya mali zake.Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
  Mkuu wa Wilaya huyo alishawahi kudai mara tu baada ya matokeo ya kura ya maoni huko Igalula kwamba anapata message za vitisho kutokana na ushindi huo.Katika Uchaguzi huo Dr Mfutakamba aliongoza kwa kura nyingi.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hiii habari kama ni ya kweli kwa kuna chumvi ndani yake. Hivi inawezekana majambazi yalikuja kukuua yakajieleza yamekusamehe .Na bado mlengwa ukapa ujasiri wa kuwaaambia unaomba uwarekodi . Unless aliyetaka kuuliwa naye ana damu ya kijambazi au huo mkanda wa video aliureodi siku tofauti na tukio
   
 8. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hayo ni mazingaombwe tu, inawezekana huyu mgombea anataka tu kujidhihirisha kwa wapiga kuwa wake kuwa ni wa muhimu sana. Mie naona kama ni sinema na mawazoni tu, hakuna lolote.
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Aug 13, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ni mgombea yupi machachari ambaye alikuwa na uhusiano na wafungwa huko siku za nyuma kiasi cha kuwapa suluari? Waziri wa mambo ya ndani, askari wa magereza, kamishna wa magereza, mwanasheria - advocate?
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Utafiti wabaini maajabu ya wabunge machachari
  Na Joseph Mwendapole  13th August 2010

  Taasisi ya utafiti ya Tunaweza imeelezea kushangazwa kwake na kuanguka vibaya kwa wabunge wengi machachari wa CCM katika kura za maoni ambao wamekuwa wakitoa michango mingi ya kuichachafya serikali ndani ya Bunge.
  Vile vile, imeelezea kushangazwa kwake na ushindi wa kishindo waliopata wabunge ambao hawana kawaida ya kuchangia bungeni wala kuuliza maswali.
  Hayo yamo katika ripoti ya uchunguzi wa Taasisi hiyo uliofanywa kati ya mwaka 2005 &#8211; 2010 kuhusu utendaji wa wabunge.
  Meneja wa taasisi hiyo, Hans Hoogeven, aliliambia NIPASHE kuwa hawakutarajia wabunge wengi wanaotoa michango bungeni kuanguka na wale wasiochangia kitu kupata ushindi mkubwa.
  Alisema kati ya wabunge 10 wa CCM ambao walikuwa wanaongoza kwa kuuliza maswali mengi, ni watatu tu wamefanikiwa kupita kwenye kura za maoni.
  "Tulitarajia kuwa wananchi wanathamini mchango wa wabunge machachari ambao wanatoa michango mingi ya kuikosoa serikali bungeni, lakini hali imekuwa tofauti kabisa na tunashindwa kuelewa kwa nini imekuwa hivyo&#8230;
  "Ina maana wananchi wanawapenda wabunge wanaokwenda kule kupumzika tu?" alihoji Hoogeven.
  Alisema Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, ndiye anaongoza kundi la wabunge 10 wa CCM ambao huwa hawaulizi maswali bungeni.
  Alisema wameshangazwa na ushindi wa Rostam ambaye takwimu za tangu mwaka 2005, zinaonyesha kuwa hajawahi kuuliza hata swali moja.
  Aliwataja wabunge wa CCM walioanguka kwenye kura za maoni ingawa wamekuwa wakichangia kwa wingi bungeni kuwa ni Mgana Msindai (Iramba Mashariki) aliyeuliza maswali 222 kwa kipindi hicho cha miaka mitano.
  Wengine na idadi ya maswali waliyouliza na majimbo yao kwenye mabano ni George Lubeleje (Mpwapwa -197), Juma Kilimbah (Iramba Magharibi -196), William Shellukindo (Bumbuli -187), Profesa Benedict Mwalyosi (Ludewa -171), Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini -162) na Mohamed Rished Abdalah (Pangani -147).
  Alitaja majina ya wabunge wa CCM ambao wanaongoza kwa kutouliza maswali tangu Bunge lianze kazi 2005 na ambao wameshinda kuwa ni Rostam Aziz (Igunga- 0), Mossy Suleiman Mussa (Mfenesini -3), Salum Khamis Salum (Meatu- 4), Juma Suleiman N'hunga (Dole-5), Lolesia Bukwimba (Busanda -5), Hassan Rajabu Khatib (Amani - 6), Omar Sheha Musa (Chumbuni -7), Abdalah Sumry (Mpanda Magharibi -7), William Kusila (Bahi -9) na Mohamed Dewji (Sindiga Mjini -10).
  Kwa ujumla, Hoogeveen, alisema aliyekuwa Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, ndiye anaongoza kwa kuichachafya serikali kwa maswali ya msingi na nyongeza.
  Alisema mbunge huyo aliuliza maswali 33 ya msingi tangu mwaka 2005, maswali 268 ya nyongeza na ametoa michango kadhaa bungeni mara 129.
  Alisema Dk. Slaa ni miongoni mwa wabunge ambao wamekuwa wakitimiza wajibu wao ipasavyo kuiwajibisha serikali ili isimamie masuala ya maendeleo.
  "Bila wabunge machachari kama Dk. Slaa tusingejua kashfa kadhaa kama ufisadi wa Benki Kuu, EPA, Richmond na maovu mengine mengi ambayo yaliibuliwa bungeni&#8230;Bunge linatumia gharama kubwa kujiendesha hivyo lazima watu wafanye kazi, kule bungeni si sehemu ya kupumzika," alisema Hoogeveen.
  "Maana ya mbunge ni kuchangia kuikosoa serikali inapoonyesha udhaifu katika utendaji, sasa kama mbunge haulizi maswali amekwenda kufanya nini bungeni?" alihoji na kuongeza kuwa wameshangazwa na anguko la wabunge waliochangia kwa wingi na waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali.
  Alisema matokeo hayo ya uchunguzi yanaacha maswali mengi kuhusu wajibu na kazi za Bunge na chaguo la wana CCM ambao walipiga kura kwenye kura za maoni hivi karibuni.
  Alisema ripoti hiyo inaacha swali kuwa ni kwa vipi wabunge wa CCM wanatathiminiwa katika kazi ya kuiwajibisha serikali ndani ya Bunge.


  Ukisoma hii taarifa na kama una akili zako timamu huitaji kuambiwi hiki chama ni cha ajabu na ni cha kuogopewa kama ukoma.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  CCM baba la makashkash! nani anabisha?
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu muhusika kama angekuwa ameshindwa kura za maoni tungesema kuwa pengine kweli anataka sympathy, lakini huyu alishinda hizo kura za maoni angetaka sympathy ya nini? Nchi hii siku hizi imefikia nchi nyingine zinazoitwa NARCO_REPUBLICS kwani hao wenye fedha ambazo wanazipata kwa njia za haramu lakini hawathibitiwi ndio hao hao wanausaka ubunge kwa udi na uvumba na mara wanapoukosa kwa njia zinazoonekana halali lazima watatumia njia haramu kama kuua ili waweze kuupata huo ubunge unaowawezesha kuendeleza hizo biashara haramu za ujangili na kuuza madawa ya kulevya!! I am 100% sure kuwa watu wengi watapoteza maisha yao wakati wa uchaguzi wa mwaka huu na dalili ziko wazi na polisi watashindwa kuwathibiti wauaji!!
   
 13. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  pumba@ best!
   
 14. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna Jina hakuna sehemu ya tukio, hakuna sources.
  Mtiririko haueleweki, unatishiwa kifo, huripoti popote, unachukua mkanda wa video, eti kisa muuaji mlipeana suruali jela.
  It does not add up. more evidence please.
   
 15. A

  August JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Tatizo linakuja katika jambo moja, mfano mimi nikipewa kandarasi ya kumuondoa mtu X, ni wazi nitataka kujua huyo mtu anafanya shughuli gani , anakaa wapi, anapendelea kutembelea wapi, na mahali pazuri pa kumpata ni wapi.
  sasa kama hilo lilifanyika basi utakuwa una mfahamu huyu mtu hata kabla hujaenda kutekeleza hilo jambo, sasa katika riwaya hii, inaonyesha mtekelezaji hakumjua x mpaka alipofika katika hatua ya utekelezaji, ndipo alipo pataka kigugumizi cha utekelezaji.
  kwa kuona huyu ni mtu anae mfahamu na alikuwa akiwapatia suruali nk.
  labda ikiwa niliielewa vibaya hiki kisa.
   
 16. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna watu kama mafia wako serikalini. Kuna watu design hiyo wako bungeni. Ukiwa Mexico huwezi kufeel hali ya madroguero kuwa na nguvu, kama hujafuatilia kwenye media. Hapa Tanzania hakuna tofauti kubwa, tayari tupo wenye hali hiyo unaweza kuona jinsi siasa zinavyoendeshwa na jinsi kesi zinavyoendeshwa mahakamani. Tumefikia mahali hata mahakama kuu inapotosha tafsiri ya katiba, ndio hali hiyo yenyewe.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Katika CCM hili si suala la ajabu sana. Mbona wengi wameisha uwawa kwa style hii na kusingizia majambazi?. Tanzania si nchi ya amani kama tunavyoambiwa. Ukitaka kuijua kuwa si nchi yenye amani ingilia shughuli la mafisadi na wahujumu uchumi. Kama Mkapa ambaye analindwa usiku na mchana aliogopa kusema ni maamuzi gani magumu aliyowahi kuyafanya mbele ya waandishi na kudai kuwa bado anapenda kuishi, iweje wewe kapuku tu usihofu. Akili kama za Akina Bihondo ndizo zilizotawala watu wengi ndani ya CCM hasa katika kupigania nafasi za ulaji.

  Tunahitaji kupitia hatua moja ndipo tutaweza kuendelea. Nayo ni kupata rais dikteta wa kutetea masilahi ya umma asiyeogopa kupoteza maisha kwa ajili ya watanzania masikini.
   
 18. M

  MSAUZI JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 228
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna kitu hapo..Pumba tu.Hapa JF tunapenda story za kutumwa,kila kitu katumwa,
   
 19. M

  Mutu JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hatari kuba!
  ngoja tusubiri habari zaidi maana kila mwenye subra hula vitamu.
   
 20. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Machafuko gani????? Mbona tunawaogopa binadamu walioumbwa kwa nyama na damu kama yetu? kwani wao hawawezi kuuwawa?
   
Loading...