Mgombea mwenza wa chama kikuu cha upinzani nchini Zambia ameaunga mkono Juhudi za Rais kuogopa kufilisiwa Mali zake

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
MGOMBEA MWENZA WA CHAMA CHA UPINZANI NCHINI ZAMBIA AMEUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS KUOGOPA KUFILISIWA MALI ZAKE.
___________________________________
Makamu wa Rais wa chama kikuu cha upinzani nchini Zambia cha United Party for National Development (UPND) Bw Geoffrey Bwalya Mwamba ameamua kukihama chama hicho na kuhamia chama tawala cha Patriotic Front (PF) kinachoongozwa na Bw Edgar Chagwa Lungu ambae ni Rais wa Sasa wa Zambia.

Ikumbukwe Bwana Mwamba ndio aliokuwa mgombea Mwenza Urais wa chama hicho cha upinzani akiwa na Mgombea wa Urais wa chama hicho Bw Hakainde Hichilema ambapo walizidiwa kwa asilimia 1.66% na Bw Lungu kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.

Kiongozi huyo Mwandamizi wa chama cha Mrengo wa Kati Cha Ujamaa wa kiliberali (Social liberalism) amesema ameamua kufikia uamuzi huo kwa sababu ya upinzani nchini humo kukosa Agenda, Baada ya kile walichokuwa anatamani kukifanya kama mpinzani ndio kinafanywa na Rais Lungu.

Bw Mwamba amesema ameamua kufanya maamuzi hayo ya kuungana na Bwana Lungu ili waweze kuisaidia nchi ya Zambia kupaa kiuchumi akiwa na kauli mbiu inayosema One Zambia one Nation, kwa maelezo yake anasema kuwa Lungu amefanya kazi kubwa sana yeye kama mzalendo anatakiwa kumuunga mkono.

Hatua hii imekuja kipindi Upinzani na Wakosoaji wa Bw Lungu Nchini Zambia umepitia wakati Mgumu baada ya kuwekwa ndani Mara kadhaa Wapinzani na wakosoaji wake kwa makosa ya uchochezi, hivi karibuni Mkosoaji mkubwa wa Bw Lungu Mbunge wa jimbo la Roan Bw Chishimba Kambwili alistakiwa kwa makosa 37 likiwemo na kosa la Uhujumu uchumi.

Bw Chishimba amekutana na kadhia hiyo baada ya kuukosoa utawala wa Kifisadi wa Bw Lungu uliopelekea Nchi ya China kuchukua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka kutokana na nchi hiyo kushindwa kulipa madeni. Vile vile China imechukua Shirika la Umeme Zambia (ZESCO) na Shirika la Habari Zambia (ZNBC).

Washirika wa Karibu wa Bw Mwamba wamesema amehama ili kunusuru kufilishiwa biashara zake, maana amekuwa akizongwa na serikali kwenye Biashara zake, ikumbukwe hivi karibuni akaunti zake za bank zimeshikiriwa na Serikali na vile vile kutozwa kodi kubwa kwenye kampuni zake, Kiongozi mkuu wa upinzani Bw Hakainde Hichilema amemtakia Bw Mwamba safari njema huko aendako.

Ni Mhere Mwita.
FB_IMG_1556088385599.jpeg
 
Waliokuwa wakija kuomba msaada kwetu wanaazima mbinu zetu,SADC kumebakia Kenya na South Africa tu kuwa na demokrasia,wengine ni domoghasia na maigizo ya kuungwa juhudi!!
 
Dah, kumbe jamaa kawa "Blackmailed". Huyo rais, tofauti na watangulizi wake, aliishaonyesha ni mtu mwenye tamaa ya madaraka mno.

Hata kwenye utaratibu wa kuheshimu mihula atasumbua sana.
 
Kule lungu huku anko jiwe, mr mapadlock himself shabash!!!

Ila ndio wanasiasa wengi walivyo wapo kwa ajili ya kuchumia tumbk na sio kwa wote, ndio maana kitu siasa sipend kukifatilia..

Wanasiasa ni km mademu tu, yule demu unaemuaminia anaweza akakupa gono.
 
Back
Top Bottom