Mgombea huyu wa CCM, ana kesi tatu za madai dhidi ya wapiga kura wake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea huyu wa CCM, ana kesi tatu za madai dhidi ya wapiga kura wake!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanaukweli, Sep 5, 2010.

 1. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Narudi tena kwa huyu mgombea ubunge wa Muhambwe, Jamal Tamim!

  Ametajwa huko nyuma kuwa elimu yake ni ya darasa la saba.

  Lakini ametajwa pia kuwa alitumia pesa sana kununua kura za maoni Jimboni mwake, Takukuru wakafumbia macho hilo.

  Lakini ukweli mwingine umefichuliwa dhidi yake kuwa huyu aliongoza kwenye kura za maoni za wahusika na biashara ya viungo wa Albino kule Kibondo, taarifa ambayo huenda vyombo vya upelelezi havikuona ukweli ndani yake.

  Mpaka wakati huu anashinda kura za maoni za ndani ya CCM, mgombea huyu ana kesi tatu za madai dhidi ya wananchi wake wa Jimbo la Muhambwe, wengi wao wakiwa viongozi wa vijiji vya Tarafa ya Mabamba (Tarafa anayoishi Jamal), akidai fidia kwa kuwa Viongozi hao wamesikika wakimtaja Jamal kuhusika na matukio mbalimbali ya Ujambazi. Moja kati ya kesi hizo ni dhidi ya Padre Mmisionari Paroko wa Parokia ya Mabamba ambaye naye anadaiwa alitamka kuwa Jamal ni Jambazi.

  Haya yote yalipelekwa kwenye Tume ya Maadili ya CCM, lakini wameona kuwa ni safi. Mie ningedhani kuwa katika suala kubwa kama hilo la kupata wawakilishi wa Wananchi, ningedhani principle ya "In case of doubt do not act" ingetumika!

  Hapa kwa kweli CCM mmenikwaza, nilikuwa mwanachama wenu, nimeghairi kabisa na sasa naendelea kufanya kampeni dhidi yenu, ili watu wengi zaidi wafahamu uozo wa watu kama wa Jamal wa darasa la Saba mshindi wa kura ya maoni ya Viungo vya Albino, na mpendwa wa CCM kisa PESA
   
 2. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Pesa ni muhimu kuliko maadili kwa CCM. Na ndio maana si tena kimbilio la wanyonge!

  Ndo maana yake!!!!!
   
 3. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2010
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sasa kama wote wako hivyo unashangaa nini? si ni sawa tu nani sasa amwambie mwenzake ana matatizo, CCM karibu wote wana Tabia zinafanana kwa hilo wao sio tatizo.Utaona kama watabisha.
   
 4. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakati wa mabadiliko ni sasa
   
 5. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Ndo maana nimeweka wazi hapa. Najua wana CCM wanasoma posts hizi, kama uongo wakanushe!
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wenyewe hao kwenye NEC majambazi sasa si huyu wanamuona mwenzao...
   
 7. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  shauri ya pesa!
   
Loading...