Mgombea Ekuru Aukot aruhusiwa kuwania urais Kenya

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,409
9,183
Wagombea wote wa Rais ruksa kushiriki uchagugazi wa marudio. Dhahiri uchaguzi oktoba 26 kusogezwa mbele.

=====
Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru mgombea urais wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot aliyekuwa ameshiriki uchaguzi mkuu tarehe 8 Agosti ashirikishwe kwenye uchaguzi mkuu mpya unaopangiwa kufanyika tarehe 26 Oktoba.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilikuwa imetangaza kwamba ni wagombea wawili pekee, Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na Raila Odinga wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) wangewania kwenye uchaguzi huo.

Bw Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi huo Jumanne.

Dkt Aukot amesema amefurahia uamuzi huo na kwamba sasa watakuwa kwenye uchaguzi kwani mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alikuwa amejaribu kuwafungia nje

Hata hivyo, amesema chama chake bado kina masuala ambayo kilitaka yashughulikiwe na tume hiyo ya uchaguzi tangu mwezi Agosti na bado hayajashughulikiwa.

Amesema kukubaliwa kwao kuwania kutawafungulia mlango kufanya mashauriano na viongozi wa IEBC.

Dkt Aukot amesema chama chake kitatoa maelezo ya kina kuhusu msimamo wao katika kipindi cha siku mbili hivi baada ya mashauriano zaidi.

Maafisa wakuu wa IEBC walikutana jana kutafakari kuhusu hatua za kuchukua baada ya hatua ya Bw Odinga lakini kufikia sasa bado hawajatoa tamko.

Kujumuishwa kwa mgombea huyo kuna maana kwamba IEBC haiwezi kumtangaza Bw Kenyatta kuwa mshindi wa moja kwa moja hata baada ya kujiondoa kwa Bw Kenyatta.

_98263330_gettyimages-858228056.jpg
Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionWafuasi wa muungano wa upinzani Nasa wamekuwa wakiandamana Mombasa kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi
Ekuru Aukot ni nani?
Dkt Aukot ni mtaalamu wa masuala ya katiba ambaye alikuwa mkurugenzi na afisa mkuu mtendaji wa wa Kamati ya Wataalamu iliyohusika katika kuandika rasimu ya ya Katiba ya Kenya iliyoanza kutekelezwa mwaka 2010.

Alikuwa amesema awali kwamba anataka kuwa rais wa taifa la Kenya kutokana na kile anachosema ni kutoheshimiwa na kuhujumiwa kwa Katiba aliyosaidia kuwepo kwake.

Dkt Aukot alizaliwa miaka 45 iliyopita katika eneo la Kapedo, katika kaunti ya Turkana kaskazini magharibi mwa Kenya.

Alianzisha chama cha Thirdway Alliance katika juhudi za kutoa uongozi mbadala na uongozi wa mageuzi kwa Wakenya.

Anaamini Wakenya hawawezi kuwategemea tena viongozi ambao wamekuwa madarakani kufikia sasa kumaliza ufisadi na ukabila.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na IEBC, Dkt Aukot alipata kura 27,311 sawa na 0.18%, nafasi ya tano kati ya wagombea wanane walioshiriki, katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 August ambao matokeo yake yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu.
 
Wagombea wote wa Rais ruksa kushiriki uchagugazi wa marudio. Dhahiri uchaguzi oktoba 26 kusogezwa mbele.

Kura zitafanyika 26/10/2017 ila jina la Mhe Ekuru litakuwepo kwenye ballot papers! Siyo wote ni yeye kwa hiyo washindani ni watatu Uhuru Ekuru na Raila na sasa kwa sababu Raila ameamua kujiengua mwenyewe watabaki Uhuru na Ekuru!!! Hapo kufa kufaana, kuondoka kwa Mhe Raila ni bahati ya mtende kwa Ekuru hata kama hatashinda ila atapata kura za kutosha kumuwezesha awe anapata mpunga(ruzuku) mpaka 2022.
 
Habari nzuri sana kwa rais Uhuru Kenyatta na hivohivo kwa wanajubilee. Sasa amepata mpinzani, Ekuru Aukot vs. Uhuru Kenyatta. Ingekuwa Aukot ameshindwa kesi kwa mujibu wa katiba uchaguzi ungehairishwa kwa sababu hairuhusu mgombea urais awe mmoja pekee yake kwenye uchaguzi.
 
Back
Top Bottom