Mgombea CHADEMA Apigwa Kinyama - Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea CHADEMA Apigwa Kinyama - Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Wambugani, Sep 23, 2010.

 1. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mgombea CHADEMA apigwa kinyama

  na Violet Tillya, Arusha


  MGOMBEA udiwani kwa tiketi ya Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Mjini Kati, Salumu Seif Simba, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha - Mount Meru, baada ya kushambuliwa kwa kipigo kikali na askari akiwa mahabusu katika Mahakama Kuu ya mkoa huo.

  Inadaiwa mgombea huyo alifikishwa katika mahakama hiyo jana, baada ya kushitakiwa kwa kosa la kufanya fujo katika stendi ya mabasi kwa kugoma kulipa ushuru wa maegesho ya gari lake alilokuwa ameliegesha katika stendi hiyo.

  Akizungumza kwa taabu na Tanzania Daima jana katika wodi aliyolazwa akiwa hospitalini hapo, alidai baaada ya kufikishwa mahakamani, baadhi ya askari waliokuwa zamu ambao amedai anawatambua kwa sura, walimzonga wakitaka awapatie sh 20,000 ili wasimweke mahabusu.

  Alisema yeye alikataa kutoa kiasi hicho, kitendo kilichosababiwa abebwe mzobemzobe na askari wapatao wanne, waliomwingiza mahabusu, huku mmoja wa askari hao akiamuru mahabusu wengine waliokuwa mahakamani hapo wampige.

  “Mahabusu hao walinishambulia vikali lakini niliweza kuwazidi nguvu, ndipo askari hao waliingia mahabusu na kuanza kunishambulia tena kwa kunipiga huku wakinikaba koo hali ambayo ilisababisha nipoteze fahamu,” alisema.


  SOURCE: Tanzania Daima 23/09/2010
   
Loading...