Mgombea CCM atishia kuua mtu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea CCM atishia kuua mtu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Sep 10, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,858
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  MGOMBEA wa ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Mpanda Mjini, Sebastiane Kapufi katika Mkoa mpya wa Katavi, anadaiwa kutishia kumuua kada mwenzake kwa tuhuma za kwamba amekuwa akimchafua kisiasa.

  Hayo yalibainishwa jana na kada huyo, John Kikwala (38) wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambapo alisema kuwa Kapufi anadaiwa kutoa wiki moja kwa kumtuhumu kuwashawishi wana CCM kumpigia kura mgombea wa Chadema.

  Kwa mujibu wa Kikwala, Kapufi anadaiwa kutoa tishio hilo la mauaji juzi saa tatu usiku baada ya kuzungumza naye (Kikwala) kwa simu ya kiganjani ambapo inadaiwa alimtaka kada mwenzake huyo kuacha mpango wake wa kumchafua kisiasa.

  Inadaiwa Kikwala amekuwa akiwaambia wanachama wenzake kuwa Kapufi hafai na hana sifa za kuwa mbunge wa jimbo hilo na kuwashawishi wapige kura kumchagua mgombea Chadema, mbunge aliyemaliza muda wake, Said Arfi.

  "Nimetoa taarifa Polisi ya kutishiwa kuuawa kwa kuwa eti simuungi tena mkono katika harakati zake kugombea ubunge kwenye jimbo hili, amenituhumu kwamba namuunga mkono na kumpigia debe mgombea wa Chadema.

  “Lakini ukweli ni kwamba tangu mchakato wa kura za maoni tulikuwa tukishirikiana mpaka akashinda kwa kishindo.... mie namshangaa kwa tuhuma anazodai," alisema.

  Kikwala alisema amefunguliwa RB yenye namba 3412/2010 dhidi ya Kapufi na kuelezea tuhuma nzito za kutishiwa kuuawa na mgombea huyo wa nafasi ya ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.

  Kapufi alipohojiwa kuhusu tuhuma hizo, alikana kumtishia maisha Kikwala lakini alikiri kufanya mawasiliano na kada huyo wa CCM kwa njia ya simu usiku huo wa juzi na kueleza kuwa kwa muda mrefu amekuwa hana uhusiano mzuri na Kikwala.

  Mgombea ubunge huyo aliendelea kusema kuwa Kikwala anamsononesha kwa kuendelea na jitihada zake za kumchafua kisiasa na kumuunga mkono mgombea wa Chadema .

  " Huyu Kikwala ni mtu wa ajabu sana, kama ndugu yangu amekuwa akinifuata mara kadhaa na kuniomba msaada wa mafuta na pesa lakini cha kushangaza amekuwa akitumia msaada huo kunichafua kisiasa na kumpigia debe mgombea wa chama kimoja cha upinzani.
   
 2. MAWANI

  MAWANI Member

  #2
  Sep 10, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo mbunge analo......, hata makada wengine hapa dar wanampigia kampeni Dr. Slaa. Hata mimi ni CCM damu damu, lakini nimeona hakuna kinachoendelea, naendelea kuwa mwanachama lakini napenda mabadiliko. Kitu kimoja cha kufahamu ni kuwa Tanzania Siyo ya CCM wala CHADEMA bali ni ya watanzania. Dr. Slaa na JK ni watanzania lakini JK amechuja ndani ya miaka mitano. sasa ni zamu ya Mtanzania mwingine ambaye anaungwa mkono na kila Mtanzania. hata Nyerere alisema, Usimchague fulani kwa sababu ni kabila lako (au chama chako) bali kwa vile ana uwezo na sifa kwa mujibu wa sheria.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Sourceeeeee???///
  Habari nzito kama hii lazima iwe na chanzo cha kuaminika
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwaka huu watamalizana wao kwa wao!
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Post deleted by Msanii
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huo ndo utamu wa siasa za makundi na watamalizama. Uzuri ni kwamba siasa za makundi zimeasisiwa na wana mtandao na ndo wamekishika chama, wakichemsha kwenye uchaguzi itakuwa ni matunda ya kazi yao ... wanavuna kile walichopanda! Ukifuga nyoka halafu akaja kukurudi wewe mwenyewe, wala huna haja ya kulia/kulalamika au kulaumu mtu mwingine.

  Njia nyeupe hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kurudi mjengoni!
   
 8. S

  Sylver Senior Member

  #8
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  How police they going to treat this ?
  kutishia kuua is serious issues ,ila jamaa kafanya vema kuripoti maana dunia ilipofika watu hufanya hiyo for power or money.
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Khaaa!!!
   
 10. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 810
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 80
  Jamani Kiswahili kinaelelweka vizuri zaidi ya ulichoandika hapo,Duh !!!!
   
 11. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,450
  Likes Received: 782
  Trophy Points: 280
  Tumesikia upande mmoja wa mlalamikaji kada wa CCM John Kikwala kupitia kwa mwandishi wa habari hizi ,mlalamikiwa mgombea ubunge CCM Sebastiane Kapufi bado.Tusipende kutoa maamuzi mepesi bila kuwa na vielelezo vinavyojitoshereza.
   
Loading...