Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,952
- 4,325
Sasa, sasa: kama kweli Mgombea huyu wa Upinzani ni jasiri wa kutosha na mwenye uchungu na sisi wavunja jasho na walipa kodi wa nchi hii, atuahidi hadharani katika kampeni zake kwamba tukimchagua atafyekelea mbali mishahara na maposho manono manono ya wabunge na wanasiasa. Na kwamba atafuta ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa mara atakapochaguliwa.
Akiweza kufanya hivyo anaweza kupata kura nyingi. Hili linawezekana, linahitaji tu utashi wa huyu mgombea. Manufaa yake ni makubwa sana kwa ustawi wa taifa letu. Ila akisema hivyo rungu la wanasiasa wenzake na hasa walio ndani ya chama chake lazima atalipata fresh.
Kwani akifanya hivyo ataweza kuokoa matrillioni ya pesa kila mwaka ambayo yatamuwezesha kutimiza hizo ndoto zake za kuongeza mishahara ya watumishi wa umma mara dufu, kutoa bima ya afya kwa wote, kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo na kadhalika.
Maana Lema (mbunge wa Arusha) alishawahi kututambia kwamba mishahara na marupurupu yao ni kiboko. Kwamba posho yao ya kikao kimoja cha masaa machache ni sawa na take home salary ya mwezi ya mtumishi wa umma mwenye elimu ya shahada ya kwanza (bachelor degree). Kuna wakati Zitto alipokuwa bado mzalendo aligomea posho hiyo kwa sababu aliiona siyo fair. Lema alishatutambia kuwa gratuity yao kila baada ya miaka mitano nayo ni kiboko. Yaani wanaishi kama malaika.
Ndiyo maana uchaguzi mkuu unapofika tumekuwa tukishuhudia maelfu kwa maelfu ya watu wakigombania kinyang'anyiro cha kuwa wabunge. Tumekuwa tukishuhudia maprofesa, madaktari, ma engineers, maaskofu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na kadhalika wakiacha kazi zao na kwenda kugombania kinyang'anyiro hicho!
Enzi za Mwalimu wawakilishi wetu hawa (wabunge) hawakuwa na mshahara wo wote kwani walitakiwa kuwa ni watu ambao wana kazi zao. Sifa moja wapo ya kuomba kuwa mbunge ilikuwa ni lazima uwe ni mtu uliye na kazi inayokupatia kipato halali kuendeshea maisha yako. Uwakilishi/ ubunge ilikuwa siyo ajira bali ni ya kujitolea or just an extra community duty. Vikao vya bunge vilikuwa wala havichukui siku nyingi kihivyo. Serikali iligharimia tu transport warrant na perdiem za wabunge hao wakati wa vikao vya bunge. Hakukuwa na sitting allowances wala mfuko wa mbunge.
Sasa, sasa: huyu mgombea asitufanyie sisi danganya toto ya kuambiwa mkinichagua, mabomba yote ya maji yatatoa pia maziwa na asali. Anatuambia eti kwamba tukimchagua:
1. Hatawasumbua wakwepa kodi, mafisadi, wabadhilifu wa pesa za umma, watakasishaji fedha, wanaoshindwa kurejesha mikopo ya mabenki, watuhumiwa wa ugaidi( upasho), ujangiri na ujambazi. Wote hawa anasema atakuwa mpole sana kwao. Anasema ataifumua TRA ili isibughudhi wafanyabiashara. Matokeo yake ni kuwa lazima makusanyo ya kodi yatatelemka kutoka huu wastani wa sasa wa sh 1.5 trillion kwa mwezi hadi kuwa kule tulikotoka kwa wastani wa billion 500 kwa mwezi sawa na payroll ya watumishi wa umma ya sasa kwa mwezi!
2. Atapandisha mishahara ya watumishi wa umma mara dufu. Watu wote watapewa bima ya afya bure. Wanafunzi wa vyuo wote watapewa mikopo ya masomo na hawatabughudhiwa kuirejesha wamalizapo masomo yao. Sasa hizo pesa atazitoa wapi?
3. Vyombo vya habari ataviruhusu kusema cho chote hata kama kinakiuka maadili ya taaluma hiyo. Hata matusi na kudhalilisha wengine itakuwa ni ruhusa. Na haki za faragha zitazingatiwa hata kama ni za jinsia ile ile.
4. Eti atabadili na kutunga sheria mbali mbali zinazompendeza wakati anajua fika kuwa chama chake hakitakuwa na idadi ya kutosha kutunga hizo sheria anazozitaka. Maana yake atatumia udikteta (presidential decrees) kutunga sheria hizo za kuendesha nchi kwa matakwa yake.
Masikini watanzania ambao wengi wao hawana uelewa wa kutosha, wanafurika kwenye hizo kampeni wakiamini kuwa kile wanachoambiwa ni cha kweli. Watanzania tusifanywe danganywa toto. Atamke wazi kwamba atafyekelea mbali mishahara na marupurupu manono ya wabunge na wanasiasa ili nao wateremuke kutoka kuishi kama malaika hadi kuishi kama tunayoishi sisi maisha ya ki.... Atamuke wazi kuwa atafyekelea mbali ruzuku ya serikali kwenye vyama vya siasa. Vyama hivi vinapaswa kujitengemea.
Sasa hivi vina umri wa miaka 30, havipaswi tena kubebwa na serikali. Pesa hiyo iende kuboresha maisha ya watanzania. Vyama vya siasa ambavyo hadi sasa havijaweza kujitegemea viachwe vife kifo cha mende. Yaani chama kinapewa mabilioni ya pesa kila mwaka lakini kinashindwa kujenga hata jengo la ofisi ya makao makuu yake kwa miaka 30, kinaendelea kutembeza bakuli kwa walala hoi -hili halikubaliki hata kidogo. Vyama hivi ambavyo haviko serious viachwe vifwe. Serikali inavipa ruzuku halafu vinaitukana hiyo serikali. Hapana.